Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,677
Jambo Mkuu....Naongea nikiwa timamu wa mwili na akili.
Hii ni kwako Waziri wa Mambo ya Ndani,mwenye dhamana ktk Jeshi la Polisi Tanzania.Ninakuandikia kama askari wa ngazi ya chini kabisa niliye muhanga wa "Mfuko wa Kufa na Kuzikana" wa Jeshi la Polisi Tanzania.
Ninakuandikia hapa,nikiwa na imani kabisa kuwa wewe u msikivu na mmoja kati ya mawaziri mnaotumia mitandao ya kijamii kwa njia nzuri ya kuwafikia vyema na kwa urahisi raia wenye shida mbalimbali,ambao kwa sbb za itifaki na utaratibu ni ngumu kukutana na kusikia kilio hiki.
Hiki ni kilio cha askari wengi wa Jeshi la Polisi Tanzania.Ambapo kama ilivyo utaratibu uliowekwa na wakuu huko juu,kila mwezi ktk "salary slip" zetu tunakatwa shilingi 5,000 kwa ajili ya kuchangia "Mfuko wa kufa na kuzikana".Pesa hii hukatwa moja kwa moja huku juu na kuingia ktk mfuko huu wa "hiyari" ulionanzishwa na polisi.
Lengo la mfuko huu linaweza kuwa zuri hapo awali,lakini matokeo ya mfuko huu ni ufisadi mkubwa kwa sisi polisi.Kawaida mfuko huu ulianzishwa ili kutoa "mkono wa pole" pindi askari polisi anapopatwa na majanga ya kufiwa na mke/mume,mtoto,wazazi na wakwe.
Hapo awali,askari aliyepatwa na majanga haya alikuwa anapewa shilingi milioni moja (1,000,000) kama mkono wa pole,lkn ktk mazingira yasiyo ya kawaida kiasi hicho kikaounguzwa bila hata kueleweka mpaka kuwa shilingi laki tano (500,000).Wakati huo huo kiwango cha kuchangia kikabaki vilevile bila kupunguzwa.
Tatizo kubwa,ambalo hata leo ukiwaita askari ktk kikao cha "siri" na kuwaauliza juu ya upatikanaji wa pesa hii,watakuambia jinsi ilivyo rahisi kwa askari kuchangiwa na wenzke kuliko kupata pesa kutoka katika mfuko huu ambao wahusika ni huko makao makuu Dsm.
Kuna askari mwenzetu ambaye mwaka 2013 alifiwa na wazazi wake wawili ktk ajali ya moto kijijini,mwaka 2015 alipoteza mkewe wakati wa kujifungua pamoja na mtoto na hivyo kuhitaji kusafirisha mwili toka mkoa mmoja kwenda mwingine hajapewa hela hiyo ya "Kufa na Kuzikana" mpaka kesho.
Licha ya kuambatanisha hati ya kifo ya wazazi na baadae kwa mkewe kuwasilisha hati ya kifo,hakuna pesa iliyofika na wakati huohuo anakatwa na kuchangia Tsh 5,000/= kila mwezi.Mkuu Waziri mwenye dhamana,suala hili si kwa askari mmoja tu,bali imekuwa kama "jipu" kwa maaskari wengi wanaopatwa na misiba.
Ukitembelea Tabora,Singida,Arusha,Manyara,Kigoma na Rukwa,Mtwara,Lindi na Ruvuma kilio hiki kwa askari ni kikubwa sana sana sana.Tatizo ni kuwa hatuna mahali pa kueleza.Katika vikao vyetu huwezi kuhoji sana...Maana huku kwetu ukiambiwa "Kaa Chini" unakaa hata kama hoja yako ilikuwa na mashiko.
Amri na agizo toka kwa mkubwa linalohitaji kukubali bila shuruti.Ni utii wa amri bila shuruti.
Lakini hata sisi ni binadamu.Tunapofiwa tunahitaji kiasi fulani ili kuwezesha misiba ya familia zetu.Kwa mishahara yetu na hali yetu duni,kukosa pesa hizi ni majanga makubwa zaidi.
Mfuko huo hatudhani hata kama una auditing,kama mlivyotisaidia kwa kuamua kuondoa maduka ya "Duty Free" sababu ya harufu ya ufisadi na hivyo kuamua kutuingizia pesa ktk akaunti zetu,Litazameni pia hili la "Mfuko wa Kufa na Kuzikana".Lengo sio ufutwe,bali tutendewe haki.
Maana kuna habari kuwa kuna watu wanatafuna pesa hizi na askari polisi anaonekana kuwa amechukua "rambirambi" zake.
Tunakuomba Waziri Mwigulu,utupie macho suala hili.Uwekwe mchakato wa uwazi wa askari kupata pesa yake pindi apatapo majanga.Haiwezekani ndani ya miaka minne mtu meshazika na kuanza maisha mapya bado rambirambi haijafika.Nakufikishia jambo hili kwa njia ya mtandao sbb bado naipenda kazi yangu,sina namna nyingine ya kukufikia na kuelezea jambo hili.Lakini ni jambo ambalo ni kilio cha askari wengi walio mijini na hasa wa vijijini.
[HASHTAG]#UsalamaWaRaiaNaMalizao[/HASHTAG]
[HASHTAG]#UtiiWaSheriBilaShuruti[/HASHTAG]
[HASHTAG]#AskariNayeNiBinadamu[/HASHTAG]