Wasallam wakuu..!
Pamoja na uharifu uliotokea au unaondelea kutokea Mkoa wa Pwani hasa maeneo ya Kibiti na Ikwiriri kwa kuuwawa Watanzania wenzetu, lakini kinachoendelea sasa hivi si haki na kinapaswa kukemewa na watu wote na kwa mtindo huu sidhani kama tunaweza kufanikiwa kuwapata wahalifu.
Ipo hivi, kwa sasa eneo la Ikwiriri kuna ukaguzi unaendelea wa abiria na ukaguzi huo unaendeshwa na askari wa jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ) kwa mabasi na magari mengine yote yanatoka na kuelekea Kusini yakitokea Dar Es Salaam na kinachofanyika kwa mabasi ya abiria ni kuwa gari inasimamishwa anaingia askari ambaye amevaa kiraia kwenye basi wakati huo nje kuna gari ya jeshi na wanajeshi wamesimama. Baada ya kuingia ndani ya basi anaamrisha abiria wote wazime simu na anawaambia mteremke chini kutoka ndani ya basi na mnapangwa mistari miwili au mitatu halafu wakati huo huo mnaambiwa mkono wa kushoto shika tikiti “ticket” yako na mkono wa kulia shika eidha kitambulisho cha uraia au cha kupigia kura na ikitokea hauna vyote viwili basi unabakizwa wakati wenzako wakiondoka na kudumbukizwa kwenye kibwawa kidogo mnaogolea na wakati mwingine mnapigwa na kufungwa kamba.
Wanaume na wanawake mnapekuliwa mpaka kwenye sehemu za siri na sijui huko sehemu za siri ni kitu gani kinatafutwa, ni kweli wahalifu wanaotafutwa wanaweza kuwamata kwa aina hii upekuzi ambayo inapelekea udhalilishaji na mateso kwa raia, kuna rafiki yangu ameshindwa kuhudhuria msiba wa baba yake mzazi ambayo yamefanyika jana saa kumi kwa mambo kama haya. Yeye alipata taarifa ya msiba juzi usiku na katika ile hali taharuki na kuchanganyikiwa akawa amesahau pochi yake “Wallet” ambayo ilikuwa ina kila aina ya kitambulisho chake akaenda rangi 3 akapata private car imefika Vikindu gari ikaharibika mara kidogo inafika basi akapanda kwa TZS 15,000/= ambayo ni nauli pungufu na hakupata ticket amefika Ikwiriri akabakizwa amepata ruhusa leo hii asubuhi.
Je, ni haki kisheria kwa mtu asiye na kitambulisho cha mpiga kura au cha "URAIA" kuteswa namna hii..?