Waziri Mwigulu Nchemba na Mkuu wa Majeshi haya yanayoendelea Kibiti yana Baraka zenu..?

nanjinji

Senior Member
Mar 23, 2017
151
250
Wasallam wakuu..!

Pamoja na uharifu uliotokea au unaondelea kutokea Mkoa wa Pwani hasa maeneo ya Kibiti na Ikwiriri kwa kuuwawa Watanzania wenzetu, lakini kinachoendelea sasa hivi si haki na kinapaswa kukemewa na watu wote na kwa mtindo huu sidhani kama tunaweza kufanikiwa kuwapata wahalifu.

Ipo hivi, kwa sasa eneo la Ikwiriri kuna ukaguzi unaendelea wa abiria na ukaguzi huo unaendeshwa na askari wa jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ) kwa mabasi na magari mengine yote yanatoka na kuelekea Kusini yakitokea Dar Es Salaam na kinachofanyika kwa mabasi ya abiria ni kuwa gari inasimamishwa anaingia askari ambaye amevaa kiraia kwenye basi wakati huo nje kuna gari ya jeshi na wanajeshi wamesimama. Baada ya kuingia ndani ya basi anaamrisha abiria wote wazime simu na anawaambia mteremke chini kutoka ndani ya basi na mnapangwa mistari miwili au mitatu halafu wakati huo huo mnaambiwa mkono wa kushoto shika tikiti “ticket” yako na mkono wa kulia shika eidha kitambulisho cha uraia au cha kupigia kura na ikitokea hauna vyote viwili basi unabakizwa wakati wenzako wakiondoka na kudumbukizwa kwenye kibwawa kidogo mnaogolea na wakati mwingine mnapigwa na kufungwa kamba.

Wanaume na wanawake mnapekuliwa mpaka kwenye sehemu za siri na sijui huko sehemu za siri ni kitu gani kinatafutwa, ni kweli wahalifu wanaotafutwa wanaweza kuwamata kwa aina hii upekuzi ambayo inapelekea udhalilishaji na mateso kwa raia, kuna rafiki yangu ameshindwa kuhudhuria msiba wa baba yake mzazi ambayo yamefanyika jana saa kumi kwa mambo kama haya. Yeye alipata taarifa ya msiba juzi usiku na katika ile hali taharuki na kuchanganyikiwa akawa amesahau pochi yake “Wallet” ambayo ilikuwa ina kila aina ya kitambulisho chake akaenda rangi 3 akapata private car imefika Vikindu gari ikaharibika mara kidogo inafika basi akapanda kwa TZS 15,000/= ambayo ni nauli pungufu na hakupata ticket amefika Ikwiriri akabakizwa amepata ruhusa leo hii asubuhi.
Je, ni haki kisheria kwa mtu asiye na kitambulisho cha mpiga kura au cha "URAIA" kuteswa namna hii..?
 

Cheche Mtungi

JF-Expert Member
Nov 14, 2010
2,573
1,250
Ndio ulinzi wenyewe,acha wahalifu watafutwe,mhalifu anaweza kutumia chombo chochote cha usafiri kuingia au kutoka eneo alilofanyia uhalifu,kama bda bda zinakaguliwa kwnn mabasi yasikaguliwe?tuviache vyombo vya usalama vifanye kazi,ukitaka kwenda kusini,beba kitambulisho,kama huna tuliza mshono,ama sivyo utabaki usaidie kazi!
 

pecial

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
638
500
haya watu walisema humu kweny jukwaa kama tynafurahi jeshi kupelekwa kule lakini litaenda kunyanyasa watu wasio na hata kweli Leo yanatokea,, basi kama ni hvyo serikali ingetoa tangazo kwa wasafiri wa njia hiyo kubeba vitambulisho vyao vya uraia au vote identity ili kuepukana na usumbufu huo wa JWTZ.. na hawa jamaa hawaelew kama usipokuwa na kitambulisho hawasikilizi hoja yaan ni adhabu kwenda mbele na kipigo hawaangalii jinsia, umri wala afya ya mtu,, hii iliwahi kutokea Tanga maeneo ya Maramba kipindi kulipotokea wale jamaa wa Amboni cave lilipelekwa jeshi kule kwa ajili ya doria asee kilichofanyk kule watu waliteseka sana so inabidi wizara husika iliangalie hili
 

kijani11

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
6,268
2,000
Inabidi itolewe elimu ya kuwa watu wawe walau na kitambulisho kimoja wakati wote.

Watanzania wengi hawana utamaduni wa kubeba vitambulisho hasa hasa wale ambao hawako kwenye mfumo rasmi wa ajira au elimu.

Pole kwa waliokumbwa na masahibu haya natumai kama kuna uvunjifu wa haki za raia hatua stahiki zitachukuliwa.
 

okaoni

JF-Expert Member
Jun 25, 2011
1,396
2,000
Hao wahalifu mnaishi nao, na ni wachache sasa wanafanya mnaishi bila amani,,,,cha msingi watajeni hao wahusika,,, maana haki za binadamu mnazozisema sasa hazitakubalika wakati kuna watu miongoni mwenu wanauwa watu kwa mtutu na hamuwataji.
 

Mr. Bigman

JF-Expert Member
May 7, 2011
2,557
2,000
Liberia ilianzaga hivi hivi. Leteni mashara yenu. Hizo bundiki hata sisi tutaweza kuzitumia
 

Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,883
2,000
Yanayotokea kama ni kweli ,sio kitu cha kuchukuliwa kama masihara hapa,pls mtoa mada weka facts ili ututhibitishie hayo madai ambayo jeshi letu linatuhumiwa kufanya hayo mambo ambayo ni ukiukwaji wa kisheria na haki za binadamu,hivi nchi yetu ina ID au wengine wanaita LIFE BOOK?,PLS any family member anaweza kukiweka hapa ili name nikione?halafu why uwe na vitu viwili yaani id na kitambulisho cha kupigia kura,bcs ninachoelewa mimi bila ID huwezi kufanya chochote kile ,kama upigaji kura,kufungua account bank,huduma kwenye mahospitali,polisi,kazi,social grants,elimu etc etc ,naomba nielimishwe hapa.
 

Maxmizer

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
4,824
2,000
kwan mhalifu anakua hana kitambulisho na ticket??

hawa nao njia yao sijaielewa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom