Waziri Mwigulu Nchemba mpaka leo hajui maana ya Bajeti?

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,545
41,050
Hivi viongozi wamepatwa na Uwendawazimu gani?

Nimepita sehemu nikamwona Mwigulu anahutubia. Mwanzoni sikujua ni tukio gani. Baadaye, nikashangaa kuona watu wengi wanasonya. Nilipouliza, nikaambiwa kuwa eti Waziri anasoma bajeti! Hapo nikaungana nao katika kupuuza takataka ile ambayo haina sifa ya kuitwa bajeti, maana kila baada ya paragraph moja au mbili, ni sentensi ya kumsifia Rais!! Sasa hiyo ni bajeti au mapambio ya kinafiki ya kumsifia Rais?

Rais Samia akemee huu ujinga. Hawa wanamlisha rushwa ya sifa ili wazidi kumlewesha na kumdidimiza. Kama ni mtu mwenye tafakari nzuri ajiulize kama kweli hizo sifa ni halisia au wanamdihaki kwa sababu wameujua udhaifu wake, kuwa anapenda sifa!!

Na wale wabunge batili wanaolipwa kwa kugonga meza na kusema ndiyo, wameendelea na uhayawani ule ule.

Tusitegemee lolote kwenye hivi vioja vya Mwigulu na wenzake. Kodi zetu zinaliwa na wabunge batili wasio na msaada wowote kwa nchi.
 
Tukiachana na Bajeti, hilo la kumsifia Rais sio siri limekithiri sana awamu hiii ya huyu mama.

Mwanzo alipoingia niliona kawaida kwasababu ni mwanzo hatujazoea Rais Mwanamke.

lakini naona tabia imeendelea kwa viwango vya juu sana,hamna Kiongozi wa Ccm anaweza ongea sentensi hata 1 akaimaliza bila msifia Rais.

Kwa mwigulu ni mwendelezo tu wa zile sifa zisizo na sababu.

Rais pekee anaeongoza kwa kusifiwa na ukiuliza wanaomsifia hawajui sababu zinazowafanya wamsifie,ni kama ka utaratbu kapya CCM.
 
Huu utamaduni wa kumsifia rais kwenye kila jambo muasisi wake ni Magufuli. Matokeo yake sasa hivi watu wanaojitambua hawana muda tena wa kufuatilia bajeti, maana hiyo tabia imekithiri, huku hilo bunge halina ridhaa ya wananchi.
 
images (10).jpeg

Bajeti yangu ya mwisho
 
Back
Top Bottom