Waziri Mwigulu kuapishwa Chato: Magufuli amezingatia Ibara ya 56 ya Katiba ya Tanzania

Lindela Escape

New Member
May 4, 2020
1
8
WanaJamii, heshima kwenu.

Kumekuwa na minong'ono mingi na miluzi kibao from opposition die hard fans kufuatia jemedari mkuu Rais John Magufuli kumuapisha Mh waziri Mwigulu Nchemba mjini Chato.

Kimsingi hawana hoja, bali wanashangaa tu na kulalamika eti why Rais afanye majukumu yake kiofisi from Chato?!! Lalamiko mufilisi kabisa hili na limejaa ignorance of basic public administration issues at Presidential level.

Nitafafanua mambo kadhaa ninayofahamu kuhusu Viapo vya mawaziri; na majukumu ya kiofisi ya Mh Rais.

1. KATIBA ya Tanzania. Hii ndiyo Sheria mama katika nchi. Mh Rais alikula kiapo kuzingatia na kuilinda Katiba ya nchi.

Ibara ya 56 ya Katiba imeelezea kuhusu Kiapo kwa Mawaziri. Nainukuu...

"Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka
awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia
kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake
kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge".


Wataalaamu wa Sheria mtusaidie kuitafsiri hiyo Ibara. Ila kwa tafsiri iliyo wazi ni kuwa Ibara tajwa inaeleza 'kiapo cha Waziri kifanyike mbele ya Rais.' Ni popote pale penye Ofisi rasmi ya Rais, ilimradi kuna uwepo wa Rais wakati wa Kiapo hicho. Katiba haisemi Kiapo cha Waziri kifanyike Ikulu ya Magogoni, au Chamwino, hapana! Ministerial Oath itafanyika "mbele ya Rais". Tusome Katiba.

2. The Official Oaths Act Cap 266.

Hii ni Sheria ya Viapo vya kiserikali Tanzania. Kifungu cha 5 cha Sheria hii pia kinaelezea the same kuwa Viapo vya mawaziri vitakuwa tendered "before the President". Sheria haisemi Viapo vya mawaziri vifanyike Ikulu ya wapi au wapi, no! Bali ni 'mbele ya Rais'.

3. The Presidential Affairs Act Cap 9.

Hii ni Sheria inayoeleza kuhusu affairs za kirais ikiwemo makazi yake, Ofisi yake, n.k

Sheria hii, katika Kifungu cha 9(2), inataja na kutambua 'State House' au 'State Lodge' kuwa ndiyo Office or Official residence for the President.

Wapo walioandika humu kwamba Mwigulu ameapishiwa kwenye jengo la Hotel. Hata kama ni kweli kwamba Kiapo kilifanyika kwenye jengo la Hotel, bado haiondoi validity na legality ya Kiapo hicho coz kilifanyika 'mbele ya Rais' kama Katiba ya nchi inavyoelekeza, pia kukiwa na Bendera ya Taifa; na Bendera ya Rais ambayo ni symbol ya President's Office impliedly mahali hapo wakati wa tukio husika.

Lakini pia, yawezekana hiyo Hotel ndiyo 'State Lodge' yenyewe rasmi kwa ukanda huo wa Chato.

Tanzania tumepata Rais ambaye anaelewa anachokifanya. Hakurupuki. Anazingatia Sheria Taratibu na Kanuni.

Mh Mwigulu chapa kazi kiongozi.

Mh Rais Dkt John Joseph Magufuli endelea kukaza, endelea kunyoosha rula.

Nchi ipo kwenye msitari, na watanzania walio wengi wapo pamoja nawe. Huu ndiyo uhalisia huku mtaani.

#Twende na Magufuli20/25#
 
Sisi Watanzania, tumekosa akili zetu wenyewe za kupaisha Taifa letu kiuchumi zaidi? Mambo gani hayaaa na yanasaidia nini? Ahhhh
 
Lindela escape,
Tafsiri ya Rais, taasisi ya urais / ikulu :
Kwa mujibu wa katiba, taasisi ya Urais na Ikulu inatakiwa itambulike kwa kufuata katiba, sheria, utaratibu na mazoea yatakayoonesha mbele ya macho ya wananchi kuwa taasisi ya Urais na Ikulu / Makao makuu yataonesha kuheshimu utaifa, kutoonesha upendeleo au kujibainisha na anapotoka Rais.

Isipokuwa ktk hali ya hatari basi taasisi ya Urais inaweza kuhamisha kwa muda taasisi hiyo au makao makuu ya nchi sehemu nyingine ambayo haijazoeleka

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) ibara ya 72 inaelekeza na kutaja majukumu ya Rais kama, Mkuu wa nchi na kama kiongozi wa serikali.

Ibara ndogo ya 4 ya Katiba hiyo inasema kwamba, katika kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Ibara hii Rais ataepuka kujinasibisha, kwa namna yoyote ile, na chama chochote cha siasa au kundi lolote kwa namna ambayo inaathiri umoja wa wananchi.

Kwa mujibu wa Katiba na ibara hiyo inaonyesha wazi kwamba rais ameivunja Katiba aliyoapa kuilinda kwa kujinasibisha kwamba yeye ni mwana CCM kindakidaki.

Magufuli amesahau kabisa majukumu yake kikatiba kwamba kiongozi wa nchi hakutakiwa kutumia Ikulu kufanya sherehe za kushukuru ushindi na wenyeviti, makatibu wa mikoa, wilaya wa Tanzania bara na Visiwani wa CCM.
 
Ndiyo maana wimbo huu wa Paschal Cassian unaoitwa " Turudi" unaiasa Tanzania na wenye mamlaka wajirudi kwani Mungu amekasirika ameleta vilio vingi, mafuriko, Corona na mikasa mingi kwa taifa akipeleka ujumbe kwa serikali ya CCM Mpya ijirudi.
 
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

  1. Katiba ni nini?Katiba ni waraka wa kisiasa unaowawezesha wananchi kujitambua kama Taifa. Pia katiba ni waraka wa kiutawala unaelezea mgawanyo wa madaraka na majukumu ya vyombo mbalimbali vya dola. Ni waraka wa kisheria unaongoza shughuli zote kisheria ambao ndio chimbuko la sharia zote nchini na pia ni muafaka wa kitaifa juu ya namna ya kuendesha mambo katika nchi.
  2. Lengo la Katiba ni lipi?Ibara 9 inasema kuwa lengo la katiba ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au wa chochote kati ya vyombo vyake na udugu na amani kutokana na kufuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambayo inasisitiza utekelezaji wa misingi ya kijamaa kwa kuzingatia mazingira yaliyomo katika Jamhuri ya Muungano.
  3. Misingi ya Katiba ni ipi?Kwanza katiba ni lazima iwezeshe wananchi kuridhiana kitaifa. Katiba lazima iwe ya kipekee kutokana na historia ya nchi husika. Katiba lazima isiruhusu ubaguzi wa aina yeyote miongoni mwa raia wake na katiba ni sheria mama katika nchi kwaiyo hakuna sharia inayotungwa itaruhusiwa kukinzana nayo.
 
Lengo la katiba siyo kumpatia mtu kujibainisha, kujimilikisha au kuhodhi nchi mara baada ya kuapishwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bali Rais anaapishwa baada ya kuchaguliwa kwa kuapa kuilinda na kuiheshimu katiba bila kusahau lengo la katiba na misingi yake ya kujenga utaifa kwa matendo, kauli na mazoea yaliyojengwa mara baada ya nchi kuwa huru na iendelee kuwa huru yaani isitawaliwe kwa matakwa na utashi wa mtu au watu wachache waliopo ktk chama cha kisiasa.
 
Mabeberu I love you the most 🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐
 
Mabeberu I love you the most 🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐🐐
Sio watu wazuri. Maana Pompeo alikuwa anatetea mash...
 
Back
Top Bottom