Waziri Mwakyembe: Msanii anayetaka kuzungumzia siasa, akagombee ubunge au udiwani

Sheria zake kashindwa kuzitumia kwenye wizara yake ya awali, sasa amezileta kwenye sanaa. Hii nchi Yangu jamaaani.
Ndo kusema kwenye kampeni hakuna Kuimba tena mbele kwa mbele?
Raisi karuhusu watu waimbe yeye amekataza!!!
 
''......Anaetaka kuoa lazima awe na cheti cha kuzaliwa.... .'
''........Kama mwenyekiti wa tume sikumuhoji Mh. Waziri Mkuu (Lowassa) kwani ushahidi unajitosheleza hivyo ajipime mwenyewe.........''

''........Siwezi kuifanyia kazi tume iliyo undwa na Mh. Nape Nnauye kwa sababu haikumhoji Mh. Paul Makonda......''

''........Hakuna msanii yeyote kuimba nyimbo za siasa..........''

Harisson Mwakyembe Mb. (Phd)
 
Taifa limeingiliwa inasikitisha sana, kauli hii kutoka kwa Waziri mwenye dhamana wasanii wetu wana kazi kubwa sana
 
Chama chetu cha mapinduzie chajenga nchi×2

hii inakubalikae...watu bana....nchi yao sisi wasindikizaji...sawa.
 
ule umaarufu wa kujiamini, ujuzi, uhodari, uchapakazi wake woooteeee anaugeuza zero
Nakumbuka alipo mwagiwa tindikali na kuwa ktk hali mbaya nilikua namuombea kuliko kujiombea....leo najuta...bora ange 想广 kabisa tu.
 
Bob Marley ana mafanikio mengi na amejiwekea heshima kubwa sana ulimwenguni. Theme ya nyimbo za Bob ni Liberation accross the world! Leo, Bob ni mfalme wa mziki wa Raggae, the same to Lucky Dubey, Alfa Brond, Spears na wengine wengi ambao wameshiriki kupigania uhuru na haki za wanyonge tena wakipingana na serikali za kidhalimu na kibaguzi na mabepari! So, kuwa succicceful sio lazima iwe kununua ndege tuu..kujiwekea heshima ya kiutu duniani ni zaidi ya hizo fedha na mali!
Anyway, kwenye hyo video, hakuma mahali ampapo waziri amepiga marufuku kuimba nyimbo za sasa, ni kama ametoa ushauri ila asijaribu kuwahadaa wasanii, asiwapangie waimbe nini, awaache wawe huru kufanya wayapendayo!.....after all chama tawala ndio cha kwanza kuwatumia wasanii kuimba siasa wakati wa kampeni!!
 
nadhani ni wakati muafaka huyu nae atumwe india kwa matibabu.
ndio maana aliropoka kuwa wanaotaka kufunga ndoa wawe na vyeti vya kuzaliwa.
atuambie kuwa TOT ya ccm walikuwa ni wachezaji wa kandanda?
 
Kachelewa sana mbona. Bushoke, Marlaw, Flora Mbasha, Diamond, TMK nk wameimba sana nyimbo za kuisifu CCM n kukandia upinzani, hioo sio siasa? Ama inaonekana ni siasa ikiwa zitaimbwa na Nay na Roma pekee!
Yaani amemsahau hata Bob Marley, kweli ulevi wa madaraka mbaya
 
Akijibu hoja ya Profesa Jay kuwa wasanii wakiimba nyimbo za siasa kuhihoji serikali wamekuwa wakinyanyaswa ila wakiimba nyimbo za kuisifia tu wanaachwa Mwakyembe amejibu kuwa wasanii hawatakiwi kuimba nyimbo za siasa na kama wanataka kuzungumzia siasa basi wagombee udiwani au ubunge.

Amesema hakuna mwanamuziki yoyote duniani aliyefanikiwa kwa kuikandia serikali, ametembelea nchi kama Nigeria na wasanii waliofanikiwa kama wakina P Square,Tiwa Savage, Davido ni wasanii wenye mafanikio lakini hawajapata mafanikio hayo kwa kuitukana serikali.

Muziki ni entaritainment industry na sio political Indusrty na hata Afrika Mashariki wasanii kama Chamilione na akina Diamond na Ali Kiba wana mafanikio lakini hawaimbi siasa.

Amemtolea mfano msanii mmoja Fella Ramson Kuti aliyeimba siasa na akaishia pabaya.


Amenikumbusha mbali .Fela Ramson Kuti na wimbo wake Wa Takuta Jamhuri .kwa maana hiyo serikali ndio ilimshindilia madawa ya kulevya mpaka akawa kichaa na kufa .tena na wakati huo huo kaka yake fela kuti kwa jina Ramson kuti snr alikuwa Waziri Wa afya Nigeria .inawezekana kweli au imetoa mfano usio sahihi ? kwani mbali ya kukamatwa na kuachiwa ilikuwa aimtetereshi kupigania siasa .au serikali ilimloga baada ya kumshindwa !!?? Huyu Waziri sio mzima bado sumu aijaisha kichwani .uwezi tenganisha muziki na harakati katika maisha .au amesahau Ccm ina bendi ya mziki na inaimba siasa au kwakuwa John komba amekufa
 
Huu ni ushahidi tosha Serikali ilihusika na kutekwa na kuteswa kwa Roma Mkatoliki na wen. Serikali dhalimu katika ubora wake.

Akijibu hoja ya Profesa Jay kuwa wasanii wakiimba nyimbo za siasa kuhihoji serikali wamekuwa wakinyanyaswa ila wakiimba nyimbo za kuisifia tu wanaachwa Mwakyembe amejibu kuwa wasanii hawatakiwi kuimba nyimbo za siasa na kama wanataka kuzungumzia siasa basi wagombee udiwani au ubunge.

Amesema hakuna mwanamuziki yoyote duniani aliyefanikiwa kwa kuikandia serikali, ametembelea nchi kama Nigeria na wasanii waliofanikiwa kama wakina P Square,Tiwa Savage, Davido ni wasanii wenye mafanikio lakini hawajapata mafanikio hayo kwa kuitukana serikali.

Muziki ni entaritainment industry na sio political Indusrty na hata Afrika Mashariki wasanii kama Chamilione na akina Diamond na Ali Kiba wana mafanikio lakini hawaimbi siasa.

Amemtolea mfano msanii mmoja Fella Ramson Kuti aliyeimba siasa na akaishia pabaya.

 
Wasanii uliotolea mifano ni wa chama kimoja vipi vile vya upinzani? Ney wa mitego ana maendeleo gani?msanii yupi ana maendeleo kisa alishabikia upinzani? Sanaa huwa na mwanzo na mwisho wake,ikibuma imebuma tu. Shamsa ford yupo cdm kitambo ila movie anazocheza hazina mafanikio,kuja wema nae ndo wale wale.

Ubunifu ziro kwenye sanaa zao
Peleka huko u CCM wako, jamaa mbona kaeleweka vizuri tu ! Mifano hiyo inatosha , unataka aorodheshe wasanii wote ili iwe nini sasa !
 
ule umaarufu wa kujiamini, ujuzi, uhodari, uchapakazi wake woooteeee anaugeuza zero
Ndio maana kila wizara akipelekwa hadumu anabadilishwa. Nashangaa sijui mwenyewe hajitambui!!!!! Hata hivyo nadhani isingekuwa kuiepusha serikali ya awamu ya nne isianguke (kama alivyodai mwenyewe katika ripoti ya Richmond), muda huu angekuwepo kijijini akishiriki kuumia uchungu wa hali ya maisha.
 
Ndo maana ukaguzi wa vyeti kwa wanasiasa hamna wana siasa wanapowageuza watanzania wote milioni 50 wajinga hila wao ndo wenye akiri tu kwanza ukaguzi wa vyeti kutowagusa wanasiasa alafu watanzania wakabaki kimya ndo walipotudharau zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom