kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,872
Kwa unyenyekevu mkubwa napenda kutoa heshima zangu zote kwako kama waziri na kama baba. Najua mimi naweza kuwa mwanao kwa umri, na kwa vile kwa mila na desturi zetu mtu mwenye watoto wa rika lako ni sawa na baba yako. Pamoja na hayo kwa utulivu kabisa naomba niseme nawe kidogo hasa kuhusu hoja yako ya jana juu ya wasanii kuimba nyimbo zenye mrengo wa kisiasa.
Mheshimiwa waziri kwanza naomba utambue kuwa kila raia wa nchi hii ana haki ya kutoa maoni. Katiba inatoa ruhusa ya raia kutoa maoni kuhusu jambo lolote liwe la kisiasa, kidini, kijamii ili mradi tu katika kutoa maoni hayo asivuke mipaka. Wasanii kama raia wana haki ya kutoa maoni yao juu ya mustakabali ya nchi yao, na kwa vile ni wasanii basi njia bora ya wao kutumia ni kupitia tungo zao. Si busara kuwapangia wasanii wetu nini cha kuimba kama mheshimiwa Rais wetu alivyosema hapangiwi na mtu cha kufanya nakushauri nawe usitupangie cha kuimba.
Umesema umefanya utafiti ukagundua hakuna msanii duniani aliyefanikiwa kwa kuimba nyimbo za siasa. Kwanza nimeshangaa sana msomi mkubwa kama wewe baba yangu mwakyembe una definition hafifu ( narrow definition) ya neno mafanikio. Muheshimiwa mafanikio hayapimwi kwa hela tu. Si lazima tupime mafanikio ya watu wetu kwa idadi ya mali walizonazo. Everyone has its own definition on success , mwingine hata kujulikana ni mafanikio. Wewe pamoja na usomi wako mahali unapoweza kukusanya watu wakalipa kukusikiliza hakupo si kwenye jimbo lako wala hata hapo bungeni lakini hawa wasanii unaosema hawana mafanikio wanakusanya mamia ya watu tena kwa pesa halafu badala ya wao kuimba wanaweka DC zao na watu wanachizika kwa kuimba wenyewe, je kwako wewe msomi na hawa watu nani ana mafanikio?
Umeninyong'onyesha uliposema kama mtu anataka siasa akagombee udiwani huko, hv waziri mzoefu na msomi wa kiwango chako hujui kuwa siasa ni maisha na kwamba hakuna kwenye katiba yetu mahali panaposema mtu mwenye ruhusa ya kuongea kuhusu siasa na mwenye mamlaka ya kuikosoa serikali lazima awe diwani au mbunge?. Unataka kutufunga mdomo tusiseme kupitia majukwaa huru kama sanaa, au kwenye hizi forums eti tukitaka kuwakosoa basi sharti kwanza tukagombee udiwani na ubunge. Hakika mzee wangu hapa umeteleza na inabidi utuombe radhi.
Lakini naomba niulize mbona miaka yote TOT imekuwa sehemu ya CCM, imekuwa chombo cha propaganda cha CCM wala hukuweza hata kusema wakae kimya. Mbona kampeni zote mmewatumia wasanii hawa hawa wa muziki kuzunguka nchi nzima kusaka nao kura iweje leo iwe haramu wasanii kukosoa serikali yao?. Nakuonea huruma sana maana kwa mtiririko huu huenda tamko hili nalo likatenguliwa kama lile la cheti cha kuzaliwa wakati wa kufunga ndoa.
Niseme tena, naombeni mtupe nafasi tuacheni tupumue jamani, mbona mnataka tuishi kama tuko syria jamani. Kwenye mitandao hamtaki tuseme, kwenye sanaa pia tusiseme mbona mtatuua? Kama unataka tusiimbe kuhusu siasa ili tusitekwe basi acheni tutekwe tu maana mkiwateka kina ROMA na NEY watazaliwa wengine wengi tu. Mheshimiwa waziri naomba usituogopeshe na kutufunga mdomo, jamani hii nchi yetu sote.
MUNGU IBARIKI TANZANIA