Waziri Mwakyembe: Azam, Zuku na DSTV walirusha maudhui ya ndani kinyume na leseni zao! Lazima warejeshe fedha zote walizowatoza Wananchi

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Waziri wa Habari, Harrison Mwakyembe amesema suala la ving'amuzi lisingefika hapa lilipo kama watu wa sekta binafsi ya habari wangekuwa wanakiri makosa ili kurekebishana

Azam, DSTV na Zuku vilirusha maudhui ya ndani kinyume na leseni zao na pia walifanya hivyo ikiwa mitambo yao haipo nchini

Amesema tulipohama kutoka Analojia kwenda dijitali Serikali ilitenganisha kazi za kutengeneza maudhui na kazi ya kurusha matangazo ili zisifanywe na mtu mmoja

Kazi ya kutengeneza maudhui inafanywa na vituo vyote vya runinga kama ITV, TBC, Clouds TV na vituo vingine huku wanaorusha matangazo wakiwa wa aina mbili; Aina ya kwanza ni wale watakaorusha matangazo ya watanzania ambayo ni bure na pili ni wale wanaorusha matangazo kwa kulipwa(Subscription)

Aidha, leseni zenyewe pia zinatofautiana namna ya kulipia, anayechukua leseni ya kurusha matangazo bure(free to air) analipia dola za kimarekani laki 4 na anayechukua leseni kwa ajili ya kulipwa analipia leseni dola za kimarekani laki 1

Sasa hawa waliingilia leseni za wengine na kukiuka leseni zao na walivyoambiwa walienda Mahakamani, kwa vile wizara, TCRA na mamlaka nyingine zinaheshimu utawala wa sheria ziliwaacha.

Asema "Hivyo kwa miaka kama mitatu hivi tunawaangalia tu ambapo ingekuwa nchi nyingine wangepelekwa mahakamani"

Mahakama iliwaambia kuwa wameenda sehemu sio na kuwataka waende kwenye tribunal of competition kama sheria itakavyo ambapo huko walishindwa kesi. Waliposhindwa kesi hiyo sasa ndipo walipoambiwa waondoe maudhui hayo kama leseni zao zinavyotaka

"Baada ya kuziondoa ndio wanaanza kupia kelele kwamba channel zimeondolewa bila kusema ukweli ulivyo. Ting, Continental, Digitek na Startimes alichukuwa hizi channel na kuzirusha bure ambapo wao walisema kuwa hela yao wataipata kwenye matangazo tu. Ila watu naona wang'angania na kulilia tu Azam, DSTV na Zuku" amesema Mwakyembe

Maudhui ya kitanzania yanatakiwa kuwa bure sio kwa kuwa tumependa yawe bure ila ni kwa mujibu wa kikatiba ambapo mwananchi ana haki ya kupata habari kitu ambacho sio kipya bali ni toka uhuru. Na wanaorusha maudhui ya ndani lazima mitambo yao iwe imesimikwa ndani ya nchi yenyewe na ndio utaratibu duniani kote

Digitek, Ting, Startimes na Continental mitambo yao ipo hapa nchini ila Azam mitambo yao haipo hapa nchini ipo Mauritius lakini sasa hawasemi ukweli. Kwa namna hiyo serikali haina uhuru wa kuambia Azam wabadili chochote kama mambo yakiharibika mpaka wao wasiliane na mamlaka za huko mitambo ilipo ili zikubali au zikatae.....sasa huwezi kuendesha nchi namna hiyo. DSTV wapo Dubai na Zuku wapo Kenya

Waziri Mwakyembe amesema kuwa tamthilia, mpira na vitu kama hivyo wanaweza kuendelea kuonesha kwa kuwa vipo kwenye leseni zao ila kile ambavyo Mtanzania lazima akipate; Taarifa ya Habari na Matukio muhimu mengine ikiwa ni hotuba za viongozi na mengine hatakiwi kulipia

Ameongeza kuwa "Kwa sasa mimi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali tunaangalia ni kiasi gani walipata na sakata hili likiisha lazima warejeshe fedha hizo"
 
Kwakifupi wizara zote za tanzania ubunifu wao sio kuwasaidia wananchi..ikiangalia kwa jicho moja unaweza fikiri wamebuni mbinu flani kusaidia raia ila ukiebda ndani zaidi msaada au faida ya walichobuni huwa ni wa muda mfupi sana baada ya hapo wanaanza.kukukamua.hakuna wizara inayobuni kusaidia raia nyingi zinbuni kuumiza na kuwabana raia saana..mfano hai ni hili la bunge kutokurushwa matangazo live..walilalalmika hawana pesa na walipojitokeza wadhamini wakawanyima..hapo ndo unagundua lengo kao sio kusaidia ni kutubana tu
 
It is too late ...Waziri kusema "watu naona wang'angania na kulilia tu Azam, DSTV na Zuku" ni kutukosea heshima Watz ambao hatuna kosa kwa mikataba ambayo taasisi zake zilisaini kwa niaba ya wananchi...wamewaacha AZAM na DSTV wamejitanua na kutumia hizo channel local kujitangaza kama sehemu ya huduma na wananchi wakahamasika wakanunua hivyo ving'amuzi. Aombe radhi tu kwa serikali kukosea kwa kushindwa kuwasimamisha matokeo yake wamezua tafrani kwa wananchi maana DSTV kwa mfano wengi wamenunua kwanza kwa kutaka burudani lakini pili baada ya kuanza kuonyesha channel za nyumbani na ndio maana unaona ma-dish kibao siku hizi ya DSTV hivyo asiwashambulie wananchi kwa kuwaambia wanang'ang'ania AZAM, DSTV na ZUKU

Yeye apambane tu kutoa taratibu za kisheria kwamba ni kinyume na leseni zao ndo maana wamesimamisha kuliko kuhamishia mashambulizi kwa wananchi
 
Serikali ya awamu hii imejaa mazingaombwe. Inafanya ujinga huu ikidhani ndiyo itapendwa. Naionea huruma sana. Maana inagombana na kila kundi...
Wafugaji
Wakulima
Waandishi wa habari
Wenye media
Wasanii

Hivi bado nani hajagombana na serikali hii?
 
Ujinga mtupu ... Kwaiyo TBC one yenyewe maudhui yake kurushwa nisahihi kwenye DSTV..??

Hawa watu mbn wanafanya watu kama wajinga .

Haya, hata km nikinyume na sheria, Hao wananchi hiyo huduma walofaidika nayo kwa muda wotee,huo wao wasiilipie???.

Tatizo lakufikiria kwa Tumbo nakumfurahisha mtu .

*I shall kindly Knee to leave my Pride*
 
It is too late ...Waziri kusema "watu naona wang'angania na kulilia tu Azam, DSTV na Zuku" ni kutukosea heshima Watz ambao hatuna kosa kwa mikataba ambayo taasisi zake zilisaini kwa niaba ya wananchi...wamewaacha AZAM na DSTV wamejitanua na kutumia hizo channel local kujitangaza kama sehemu ya huduma na wananchi wakahamasika wakanunua hivyo ving'amuzi. Aombe radhi tu kwa serikali kukosea kwa kushindwa kuwasimamisha matokeo yake wamezua tafrani kwa wananchi maana DSTV kwa mfano wengi wamenunua kwanza kwa kutaka burudani lakini pili baada ya kuanza kuonyesha channel za nyumbani na ndio maana unaona ma-dish kibao siku hizi ya DSTV hivyo asiwashambulie wananchi kwa kuwaambia wanang'ang'ania AZAM, DSTV na ZUKU

Yeye apambane tu kutoa taratibu za kisheria kwamba ni kinyume na leseni zao ndo maana wamesimamisha kuliko kuhamishia mashambulizi kwa wananchi
Suala la kujiuliza sasa kwanini TBC ibakie, tena kwa kulazimisha?
 
Naona rangi sielewi. Anasema wananchi waliolopishwa warejeshewe mbona hata sasa ikiwa chanel za nyumbani hazipo tunalipia kiasi hichohicho?

Ni zaidi ya siasa. Je ni kiasi gani tunapaswakurejeshewa? Kwa nini basi mara baada ya chanel za local kuondolewa gharama zisipungue?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga mtupu ... Kwaiyo TBC one yenyewe maudhui yake kurushwa nisahihi kwenye DSTV..??

Hawa watu mbn wanafanya watu kama wajinga .

Haya, hata km nikinyume na sheria, Hao wananchi hiyo huduma walofaidika nayo kwa muda wotee,huo wao wasiilipie???.

Tatizo lakufikiria kwa Tumbo nakumfurahisha mtu .

*I shall kindly Knee to leave my Pride*
Soma taratibu na sheria za nchi utaelewa kama unataka kuelewa ila kama unataka kuendelea kuwa mbumbumbu basi endelea kutoa mapovu ya OMO!
 
Back
Top Bottom