Karibuni masijala
JF-Expert Member
- Sep 13, 2012
- 409
- 135
sio kama anajifanya anajua..ni anajua na kichwa ile mbaya..mbona zitto anamkimbia?!?
Kujua mtu anajua mpaka akimbiwe na zk wa masalia
sio kama anajifanya anajua..ni anajua na kichwa ile mbaya..mbona zitto anamkimbia?!?
..wewe tutakuweka kwenye kundi la Mulugo......muda si mrefu....ukiendelea na hiyo nadharia yako kuhusu Prof
Mbona wewe tayari upo katika kundi hilo la Mulugo?
......dogo huu mwaka mpya 2013 tuuanze vyema.......acha matusi.......Ukiwa hujui halafu hujijui kuwa hujui matokeo yake ndio kama unavyofanya hivi sasa.........
Hustahili kuendelea kujibiwa!!
Hapa na mimi sijakuelewa? Umewahi kufika Rukwa na Mpanda ukaona mazao yanaoza? Serikali ilinunua mahindi kule ikayakimbia! Soko halipo kule na la mbali unalifikiaje bila barabara? Na pia usimguse Sospeter Muhongo, ana vyeti na ameelimika waulize Germany tena ilikoanza shule walimpa PhD. Google kazi zake za jiolojia worldwide utaamua mwenyewe. Muhongo ni tofauti na vilaza wengi wa CCM[/QUOTE]Anaeleza kuwa tatizo la Tanzania sio uzalishaji (kilimo cha mazao ya chakula) bali tatizo ni masoko. Ni nchi gani iliyowahi kuzalisha ikakosa masoko katika dunia ya leo?
.
Tuanzie na kaburi la marehemu Philip Mulugo kama kweli lipo ndio tutarejea mezani kujadili maana ndugu zake watakuwa wanaumia wakisikia jina la ndugu yao likitamba kwenye media ilhali wakijua ndugu yao alishatangulia mbele za haki zamani hizo!!
na Angelica Sullusi, Mbeya
SIKU chache baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), kumtolea uvivu Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, akidai ana elemu ya kuunga unga, sakata hilo limeendelea kuibua mambo mapya.
Mbilinyi maarufu kama Sugu, alidai kuwa Mulugo hawezi kumbabaisha kwa vile ameunga elimu akiwa amesoma kwa kutumia jina la mtu mwingine aliyeitwa Amim.
Alisema kuwa anamfahamu sana naibu waziri huyo kwa vile alisoma naye sekondari ya Mbeya Day akiwa anamtangulia madarasa mawili, lakini wakati huo alikuwa akijulikana kama Amim si Philipo Mulugo.
Wakati Mulugo akiwa amejitetea kwa madai kuwa mwenye shaka na wasiwasi wa elimu yake aende akatazame rekodi zake Chuo Kikuu Huria, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), naye ameibua tuhuma mpya dhidi yake.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara juzi mjini Mbeya eneo la Sido Mwanjelwa, Msigwa alisema kuwa si jambo la kushangaza kwa Mulugo kushindwa kuelewa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulitokana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Alisema kuwa Mulugo aliwahi pia kuchemka bungeni na kuwekwa kwenye kumbukumbu za Bunge mambo ya ajabu.
Jamani katika mfumo wa elimu kuna vitu vinaitwa K tatu ambazo ni Kusoma, Kuandika na Kuhesabu, lakini yeye alitueleza kuwa K hizi zinatafsiriwa kwa lugha ya Kiingereza kwa R tatu yaani Reading, Writing and Arthematic, kitu ambacho si kweli, alisema.
Mchungaji Msigwa aliongeza kuwa Mulugo alipewa unaibu waziri kwa fadhila na kwamba ni bora akanyamaza kabisa na kuamua kufanya kazi ya kuwatetea wananchi jimboni kwake Songwe juu ya mikataba mibovu wanayoingia ya madini.
Madai ya Sugu na Msigwa juu ya Mulugo yameibuliwa baada ya naibu waziri huyo kusema kuwa CCM itayakomboa majimbo yaliyoko mikononi mwa CHADEMA mkoani humo likiwemo pia la Mbeya Mjini.
Awali akizungumza katika mkutano huo, Sugu alisema hana sababu ya kuendelea kumjibu Mulugo kwa kuwa tayari wananchi wa Mbeya wamekwishakumjibu kwa kujitokeza kwa wingi kumsikiliza mbunge wao tofauti na ilivyokuwa katika mkutano wa CCM aliohutubia naibu huyo.
Hivi tu mlivyojitokeza wengi mnanipa faraja kuwa tayari Mulugo ujumbe umemfikia sina sababu ya kuendelea kusema kitu, nawashukuru sana Wanambeya wenzangu kwa kuniunga mkono.
source: Tanzaniadaima
Mulugo anaumbuka kwa sababu ya kiherehere chake. Ninafahamu wapo mawaziri wengi sana ambao hawana kitu kichwani ila tofauti yao na Mulugo ni kuwa wao wanaficha ujinga wao kwa kukaa kimya. Mfano ni Shukuru kawambwa ambaye ni bosi wa Mulugo. Mwingine atakayeumbuka muda si mrefu ni Sospeter Muhongo, jamaa anajidai much know vibaya sana ila hakuna la maana analoongea.