He! Kumbe Naibu Waziri wa kuporomoka kwa Elimu na yeye ni chakachua. Hapo unategemea nini? Kumbe hawa watu ambao huwa wanapenda publicity na media covarage wana mengi waliyoyaficha. Ajabu mtu ulimi unateleza badala ya kusema Zanzibar unasema Zimbabwe, utashindwa kugundua kama umekosea na kuwaomba radhi hadhira? Hapana Mulugo ana tatizo kubwa zaidi ya tunavohisi au hata anavojifahamu mwenyewe. Halafu speech unayokwenda present kimataifa haiwezekani ikasomwa au kueditiwa na mtu mmoja au mara moja tu. Kitu kinachoandaliwa kimataifa kinapaswa kuwa na hadhi ya kimataifa, kama Obama anaweza kufanya rehearse ya kitu atakacho present, sembuse Amim Augustino?