Waziri Mulugo azidi kuandamwa

Waziri Mulugo azidi kuandamwa

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110

na Angelica Sullusi, Mbeya

SIKU chache baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), kumtolea uvivu Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, akidai ana elemu ya kuunga unga, sakata hilo limeendelea kuibua mambo mapya.

Mbilinyi maarufu kama Sugu, alidai kuwa Mulugo hawezi kumbabaisha kwa vile ameunga elimu akiwa amesoma kwa kutumia jina la mtu mwingine aliyeitwa Amim.

Alisema kuwa anamfahamu sana naibu waziri huyo kwa vile alisoma naye sekondari ya Mbeya Day akiwa anamtangulia madarasa mawili, lakini wakati huo alikuwa akijulikana kama Amim si Philipo Mulugo.

Wakati Mulugo akiwa amejitetea kwa madai kuwa mwenye shaka na wasiwasi wa elimu yake aende akatazame rekodi zake Chuo Kikuu Huria, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), naye ameibua tuhuma mpya dhidi yake.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara juzi mjini Mbeya eneo la Sido Mwanjelwa, Msigwa alisema kuwa si jambo la kushangaza kwa Mulugo kushindwa kuelewa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulitokana na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Alisema kuwa Mulugo aliwahi pia kuchemka bungeni na kuwekwa kwenye kumbukumbu za Bunge mambo ya ajabu.
"Jamani katika mfumo wa elimu kuna vitu vinaitwa ‘K' tatu ambazo ni Kusoma, Kuandika na Kuhesabu, lakini yeye alitueleza kuwa ‘K' hizi zinatafsiriwa kwa lugha ya Kiingereza kwa ‘R' tatu yaani Reading, Writing and Arthematic, kitu ambacho si kweli," alisema.
Mchungaji Msigwa aliongeza kuwa Mulugo alipewa unaibu waziri kwa fadhila na kwamba ni bora akanyamaza kabisa na kuamua kufanya kazi ya kuwatetea wananchi jimboni kwake Songwe juu ya mikataba mibovu wanayoingia ya madini.

Madai ya Sugu na Msigwa juu ya Mulugo yameibuliwa baada ya naibu waziri huyo kusema kuwa CCM itayakomboa majimbo yaliyoko mikononi mwa CHADEMA mkoani humo likiwemo pia la Mbeya Mjini.

Awali akizungumza katika mkutano huo, Sugu alisema hana sababu ya kuendelea kumjibu Mulugo kwa kuwa tayari wananchi wa Mbeya wamekwishakumjibu kwa kujitokeza kwa wingi kumsikiliza mbunge wao tofauti na ilivyokuwa katika mkutano wa CCM aliohutubia naibu huyo.

"Hivi tu mlivyojitokeza wengi mnanipa faraja kuwa tayari Mulugo ujumbe umemfikia sina sababu ya kuendelea kusema kitu, nawashukuru sana Wanambeya wenzangu kwa kuniunga mkono.

source: Tanzaniadaima
 
Wana JF,

Itakumbukwa kuwa mwaka 1996 ziliibuliwa tuhuma juu ya aliyekuwa mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CCM, Mh. Kihiyo kuwa alikuwa amegushi vyeti na hivyo ukweli juu ya elimu yake ukawa na walakini. Baada ya ufuatiliaji wa karibu na kwa kufuata taratibu za kisheria ilithibitika kuwa alikuwa amegushi na ikapelekea kuvuliwa ubunge na kuleta msamiati 'kihiyo'

Leo hii kuna malumbano juu ya elimu na uwezo wa naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, Mh. Mulugo, hali inayopelekea wengi kuwaza kuwepo mazingira ya kugushi vyeti. Akina Masumbuko Lamwai waliokomaa na Kihiyo mpaka kikaeleweka, leo hii wako wapi? Wapo watu waliosoma na Mh. Mulugo, hebu wajitokeze kuweka mambo wazi ili kuokoa mustakabali wa elimu ya nchi hii ambayo bila kumumunya maneno, hali yake si nzuri hata kidogo.
 
Tuanzie na kaburi la marehemu Philip Mulugo kama kweli lipo ndio tutarejea mezani kujadili maana ndugu zake watakuwa wanaumia wakisikia jina la ndugu yao likitamba kwenye media ilhali wakijua ndugu yao alishatangulia mbele za haki zamani hizo!!
 
amim alitakiwa kujiuzulu kulekule sauz mara baada ya kuitia aibu nchi mkutanoni pale. km naibu waziri wa elimu elimu yake ina utata unategemea elimu ya wananchi itakuwaje? hivi mamlaka ya uteuzi huwa inafanya veting kweli? majaji yale yale khaaa! only in tz.
 
Aibu kubwa itakua kwa jahkaya wala sio huyo mulugo feki,
intelijensia ilikua ya nyerere hii ya jahkaya ni genge la wezi na majambazi tu.twiga anapanda ndege,alafu unaambiwa intelijensia iko makini, tembo wanauawa,bado unaambiwa kuna intelijensia.

Watetea haki za wafanyakazi na wnanchi wanauawa na kuteswa(Mwangosi,Ulimboka) bado tunaambiwa kuna taasisi ya kulinda usalama wa nchiTISS.

Ndege ya kivita,ya jeshi inatua kwenye nchi yako na kufanya uhalifu alafu bado unaambiwa kuna intelijensia,
ahahaaaaaa.....mkwereh ni nouma..!!!!
 
hahahahahaha na Lowasa afuatiliwe Jamani, mi nawasiwasi nae sana.
 
Mulugo hajiwezi jamani!

Mulugo anaumbuka kwa sababu ya kiherehere chake. Ninafahamu wapo mawaziri wengi sana ambao hawana kitu kichwani ila tofauti yao na Mulugo ni kuwa wao wanaficha ujinga wao kwa kukaa kimya. Mfano ni Shukuru kawambwa ambaye ni bosi wa Mulugo. Mwingine atakayeumbuka muda si mrefu ni Sospeter Muhongo, jamaa anajidai much know vibaya sana ila hakuna la maana analoongea.
 
Mulugo anaumbuka kwa sababu ya kiherehere chake. Ninafahamu wapo mawaziri wengi sana ambao hawana kitu kichwani ila tofauti yao na Mulugo ni kuwa wao wanaficha ujinga wao kwa kukaa kimya. Mfano ni Shukuru kawambwa ambaye ni bosi wa Mulugo. Mwingine atakayeumbuka muda si mrefu ni Sospeter Muhongo, jamaa anajidai much know vibaya sana ila hakuna la maana analoongea.

sio kama anajifanya anajua..ni anajua na kichwa ile mbaya..mbona zitto anamkimbia?!?
 
sio kama anajifanya anajua..ni anajua na kichwa ile mbaya..mbona zitto anamkimbia?!?

Siku za karibuni nimekuwa nikimsikia akizungumzia kuhusu uzalishaji na masoko. Jamaa hana analofahamu bali kujitutumua tu. Anaeleza kuwa tatizo la Tanzania sio uzalishaji (kilimo cha mazao ya chakula) bali tatizo ni masoko. Ni nchi gani iliyowahi kuzalisha ikakosa masoko katika dunia ya leo? Kama unamuunga mkono unanipa sababu za kukuhofia na wewe pia.
 
Binafsi nilimstukia muda mrefu sana , Kwa namna alivyokuwa anawadhalilisha Wawekezaji wazalendo wa Elimu haikuhitaji ujuzi mkubwa kuona kwamba hafai kuwa kiongozi , Badala ya kurekebisha kasoro , yeye alizifunga shule ambazo pamoja na mapungufu yake bado zilikuwa bora kuliko hizi zao za kata ! Hana uwezo wa kusimamia wizara , Amekosa heshima , hekima na busara , Naunga mkono hoja , achunguzwe .
 
amim alitakiwa kujiuzulu kulekule sauz mara baada ya kuitia aibu nchi mkutanoni pale. km naibu waziri wa elimu elimu yake ina utata unategemea elimu ya wananchi itakuwaje? hivi mamlaka ya uteuzi huwa inafanya veting kweli? majaji yale yale khaaa! only in tz.

Kujiuzulu hawa jamaa utamaduni huo ni ndoto kwao, lakini hata Baba Riz naye si atengue tu uteuzi wake mtu kutoka AMIM AUGUSTINO hadi Philipo Mulugo si wizi wa waziwazi huu?
 
amim inabid uwe mpole :confused2::confused2: maana huu ukweli unaumaaa
 
Back
Top Bottom