Waziri Muhongo na Mawaziri wa Rwanda na Burundi, Wazindua mradi wa Umeme wa Maji Rusumo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,689
55,661
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kushirikiana na mawaziri wenzake wa kutoka Rwanda na Burundi leo wanatarajiwa kushuhudia uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa maji wa megawati 80 katika eneo la Rusumo katika Mto Kagera wilayani hapa.

Mradi huo wa kuzalisha na kusambaza umeme katika maporomoko ya maji ya Rusumo katika Mto Kagera utanufaisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi.

Ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme unagharimiwa na Benki ya Dunia ilhali ujenzi wa njia ya umeme kuunganisha katika Gridi za Taifa za nchi hizo tatu unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na waandalizi wa uzinduzi huo.

Wadau wengine wanaotarajiwa katika uzinduzi ni wawakilishi kutoka Benki ya Dunia, AfDB na wajumbe wa Bodi ya Mradi wa Umeme wa Rusumo kutoka nchi hizo tatu.

Kupitia kwa mpango huo kabambe, kila nchi itapata nyongeza ya megawati 26.6 katika gridi zao za taifa na hili linatarajiwa pia kuimarisha uunganishwaji umeme wa kikanda baina ya nchi hizo tatu ambazo pia ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

“Kukamilika kwa mradi huu kutanufaisha kaya elfu saba (7,000) kupitia mpango wa maendeleo katika serikali za mitaa na kaya nyingine 188 zinazozunguka mradi huu,” ilisema taarifa hiyo na kuongeza kuwa inategemewa pia wakati wa utekelezaji wa mradi huu kabambe wa kikanda katika eneo la Afrika Mashariki, kutakuwa na ajira kwa zaidi ya wafanyakazi 500 wenye weledi, weledi wa kati na vibarua kutoka nchi tatu zitakazonufaika na mradi huu.

Ujenzi wa mradi unatarajiwa kutekelezwa kwa miaka mitatu na utakamilika mwaka 2020. Makandarasi wawili kutoka China, CGCOC Group Ltd na Jiangxi Water & Hydropower Construction Company Ltd (CGCOC - JWHC JV) watajenga bwawa la maji pamoja na miundombinu mingine.

Kwa upande mwingine, muunganiko wa makandarasi wawili Rusumo Falls Andritz Hydro GmbH ya Ujerumani na Andritz Hydro PVT Ltd ya India watahusika na ufungaji wa mitambo ya kuzalisha na kusambaza umeme.

Mradi wa kuzalisha umeme wa maji wa Rusumo unasimamiwa na taasisi ya Nile Equatorial Lakes Subsidiary Action Program Co-ordination Unit (NELSAP-CU) iliyopewa jukumu hilo na nchi tatu wanufaika kupitia Kampuni ya Rusumo Power Ltd (RPCL), inayomilikiwa kwa pamoja na mashirika ya umeme katika nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi

======

UPDATE; 30th March 2017

Mradi wa nchi tatu wa ujenzi wa umeme wa maporomoko ya Rusumo wazinduliwa rasmi wilayani Ngara.

Serikali za nchi tatu za Rwanda, Burundi na Tanzania leo zimezindua rasmi mradi wa pamoja wa ujenzi wa umeme utakaotokana na maporomoko ya mto Rusumo yaliyoko kwenye eneo la wilayani ya Ngara iliyoko mkoani Kagera katika mpaka unaotenga nchi za Rwanda na Tanzania ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha kiasi cha umeme wa megawati 80 ambapo kila nchi itapata mgao wa zaidi ya megawati 27.

Uzinduzi huo umeongozwa na waziri wa nishati na madini wa nchi ya Tanzania, Profesa Sospiter Muhongo na umehudhuriwa na waziri wa nishati na madini wa nchi ya Rwanda Jemsi Msoni, waziri wa nishati wa nchi ya Burundi , Come Manirakiza pamoja na viongozi wa mbalimbali wakiwemo wafadhili wa mradi huo ambao ni pamoja na benki ya dunia na benki ya maendeleo ya Afrika, akizungumza wakati akielezea gharama za mradi huo Profesa Muhongo amesema nchi ya Burundi haitachangia gharama yoyote katika ya mradi na nchi Rwanda itachangia asilimia 50 ambapo nchi ya Tanzania itachangia asilimia 100.

Kwa upande wake, Mhandisi Johakim Joseph ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni itakayojenga mradi huo ya Rusumo power company limited amesema huo utagharimu dola za kimarekani zaidi ya milioni 340 ambazo ni kwa ajili ya ujenzi wa mtambo wa kufua umeme na fidia kwa wananchi wataoondolewa kwenye maeneo ya mradi.

Naye, meneja wa TANESCO katika mkoa ya kanda ya ziwa , Amos Maganga amesema zaidi ya megawati 27 ambazo Tanzania itazipata kutokana na mradi huo zitaongezwa na zitaunganishwa kwenye gridi ya taifa, huku Deodatus Kinawilo mkuu wa wilaya ya Bukoba ambaye amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Mstapha Kijuu katika uzinduzi wa mradi akisema kuwa mradi huo utakuwa chachu ya maendeleo kwa kuwa utaongeza ajira na mahusiano.
17457854_1260279277361284_2705922028366522657_n.jpg
17523519_1260279334027945_7172792729994943899_n.jpg
17425173_1260279374027941_1007189696626092757_n.jpg
17554399_1260279300694615_5620119124637384201_n.jpg
17554108_1260279284027950_3844971399019067961_n.jpg
10420760_1519060075029066_5207771064713007959_n.jpg

Chanzo: ITV
 
mimi hua napenda tu hao wanyarwanda wanavyocheza hio ngoma yao ...utapenda kwakweli imekaa vizuri sana....km mtindo wa nyoka fulani hivi
 
Umejuaje kama ni wanyarwanda?
angalia kwenye picha ambayo wakinamama wanacheza halafu kuna bendera 3 ...angalia ya rwanda ipo kati kati rangi zake na wao walivyovaa..mara nyingi wanyarwanda kwenye shughuli za kitaifa/Kimataifa hua wanapenda kuvaa mavazi yanayoendana na bendera ya nchi yao...halafu angalia wanavyocheza...km huamini nenda youtube katafute video zao halafu urudi hapa
 
angalia kwenye picha ambayo wakinamama wanacheza halafu kuna bendera 3 ...angalia ya rwanda ipo kati kati rangi zake na wao walivyovaa..mara nyingi wanyarwanda kwenye shughuli za kitaifa/Kimataifa hua wanapenda kuvaa mavazi yanayoendana na bendera ya nchi yao...halafu angalia wanavyocheza...km huamini nenda youtube katafute video zao halafu urudi hapa
Hapo sawa.
 
Nasubiri tamko kutoka Misri.

Bora wangetamka ikaeleweka, wanaweza fanya huo mradi usisimame. Watasambaza pesa watu wachanganyikiwe.

Hivi maofisa wa uhamiaji upande wa Tanzania wameshahamia Ofisi za pamoja pale mpakani Rusumo?
 
Taarifa haijagusa kuhusu umeme huo wa ziada utakaoingia ktk gridi ya Taifa Tanzania itasaidia vipi nchi kutimiza ndoto ya viwandavikubwa, vya kati na vidogo maeneo hayo ya Magharibi mwa Tanzania. Naona mkazo ktk taarifa ni i ngazi ya kaya ngapi zitaweza kunufaika na umeme huo kwa matumizi ya kijamii, si haba pia siku moja mahitaji viwanda vitapewa uzito wake .
 
Pongezi kwa serikali ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA CHINI YA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI. waziri huyu anapiga kazi vizuri sana.
Wale wanywa sifongo wa ufipa huwezi kuwaona kwenye hbr kama hizi.utadhani ni wabelgiji.
Wao wasikie umbea na habari mbaya tuu.utawaona kama mijusi imekurupushwa shimoni.
 
Mpenda sifa kilevi masikini hii imempita...hongera sana kikwete kwa mipango yako madhubuti,maisha bora kwa kila mtanzania..!!
 
Pongezi kwa serikali ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA CHINI YA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI. waziri huyu anapiga kazi vizuri sana.
Wale wanywa sifongo wa ufipa huwezi kuwaona kwenye hbr kama hizi.utadhani ni wabelgiji.
Wao wasikie umbea na habari mbaya tuu.utawaona kama mijusi imekurupushwa shimoni.
We nni wewe unakua kama umetoka jela juzi,huu mradi haujaanza jana au juzi,hiyo kilevi wako wala usimtaje hapa,kuna wanaume walipambana Uko nyuma..!!
 
Wanachezea Maji ya Egypt... nadhani hawazijui F-16 zinaboa kwa secunde kadhaa tu na kurejea Cairo
 
We nni wewe unakua kama umetoka jela juzi,huu mradi haujaanza jana au juzi,hiyo kilevi wako wala usimtaje hapa,kuna wanaume walipambana Uko nyuma..!!

Kwa wivu wako huu.utapata sschzophrenia kwa kujitakia.relax majita.
By the way nina anaye uendeleza kwa sasa?
 
We nni wewe unakua kama umetoka jela juzi,huu mradi haujaanza jana au juzi,hiyo kilevi wako wala usimtaje hapa,kuna wanaume walipambana Uko nyuma..!!

Kwa hiyo na lile daraja la Kigamboni apongezwe Nyerere aliyekuwa na idea hiyo 1970 na si Kikwete aliyetekeleza?

Hii nchi ina tatizo la utekerezaji na siyo mipango na ahadi,kwa hiyo ni ujinga kumpongeza aliyeahidi tu bila kumtambua anayetekeleza hizo ahadi.
 
Back
Top Bottom