Waziri Muhongo asimamisha kazi na kukamata vifaa vya kampuni ya Off Route Technology, Mbeya

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
Serikali imesimamisha shughuli za uchimbaji wa Makaa ya Mawe ya Kampuni ya Off Route Technology iliyopo Kyela ikiwemo kukamata vifaa vya uchimbaji na kuhakikisha kuwa vinakuwa chini ya uangalizi wa Mkoa wa Mbeya hadi hapo uchunguzi dhidi ya uhalali wa kampuni hiyo kuchimba makaa utakapokamilika.

Hatua hiyo inafuatia ziara ya Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo kutembelea mgodini hapo na kubaini kuwa, kampuni hiyo inachimba makaa bila kuwa na leseni halali ya uchimbaji madini.

Aidha, Prof. Muhongo ameitaka kampuni hiyo kulipa kodi zote za Serikali ikiwemo inazodaiwa na Halmashuri tangu ianze kufanya shughuli za kuchimba. Aidha, ili kujua undani wa suala hilo, Prof. Muhongo ameitisha kikao kifanyike kati ya mgodi huo, Wizara ya Nishati na Madini, Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania ( TMAA), Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini Magharibi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kyela, tarehe 18 Januari, 2016 chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini.

"Hawa watu wamechimba makaa, wameuza bila kuwa na leseni na tunawadai kodi zetu. Uongozi hakikisheni katika kikao hicho mnakuja na madai yenu. TMAA pia mje na madai yenu", ameongeza Prof. Muhongo.

Prof. Muhongo pia amezitaka pande zote kuwasilisha nyaraka muhimu kuhusu suala hilo, ili iamuliwe kwa kufuata sheria na taratibu stahili, "hakuna mtu atakayeonewa, kila upande uje na nyaraka zote na sisi Wizarani huko ndani kwetu tutaulizana wenyewe kuhusu jambo hili halafu tutalitolea taarifa", amesema. Prof. Muhongo.

Akifafanua kuhusu suala hilo , Afisa Mfawidhi wa TMAA, Mhandisi Jumanne Mohamed amesema kuwa, awali Wakala ilifanya ukaguzi na kubaini kuwa kampuni hiyo hailipi kodi na kuwa yapo malimbikizo ya madai ambayo yalipaswa kulipwa na kuongeza kuwa baada ya mawasiliano juu ya suala hilo, kampuni iliahidi kulipa kwa awamu jambo ambalo halijafanywa hadi sasa.

Kampuni ya Off Route Technology, ipo katika Kijiji cha Ngana Wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya.
 
Kwa mwendo huu kuna mahala tutafika nchi hii imeoza mpaka vidonda visafishwe ipakwe yusso pana kazi khasa sekta ya madini kuna watu wanapiga sana fedhwa si wageni wala wenyeji wote wanapiga.
 
Prof. hongera kwa kazi nzuri
 
Kweli nimeamini Profesa Muhongo alikuwa jembe sema kuna mfumo ulikuwa unambana...sasa naona under JPM katoa makucha yake.....ila naomba aangalie na yale mapendekezo ya PAC ahakikishe kila mikataba inayovujisha mapato na kuligharimu taifa inavunjwa.....Ingawa kuvunja mikataba kunaweza kugharimu faini ila kama muda ukiisha mikataba isiongezwe na kukiwa na mbadala wizara ichukue hatua ya haraka....

Hongera Muhongo.....kaza buti sekta ya nishati ni chafu mno.....wasafishe wote watanzania tunakutegemea....maana wanatuibia sana
 
Halafu kuna kuna mtu bila hata ya aibu anasema eti profesa muhongo hakufaa kupewa uwaziri, kabla ya mtu hakafikiria kuandika utumbo wake afanya research ndogo tu la sivyo atajidharaulisha mbele ya watu makini
 
Kwa mwendo huu kuna mahala tutafika nchi hii imeoza mpaka vidonda visafishwe ipakwe yusso pana kazi khasa sekta ya madini kuna watu wanapiga sana fedhwa si wageni wala wenyeji wote wanapiga.
Kama mikataba inasainiwa kwa siri huyo mbunge anajuaje?
 
Halafu kuna kuna mtu bila hata ya aibu anasema eti profesa muhongo hakufaa kupewa uwaziri, kabla ya mtu hakafikiria kuandika utumbo wake afanya research ndogo tu la sivyo atajidharaulisha mbele ya watu makini
Ndugu huo utafiti unaotaka ufanyike ni upi? tambua kuwa kampuni hiyo imeanza kufanya kazi zake mwaka 2013 na ilikuwa haina leseni tangu wakati huo na hailipi chochote, kitu cha msingi ninachotaka nikufahamishe kuwa Muhongo hafai ni vema ukatambua huyu huyu Muhongo alikuwa waziri wa wizara hii kabla ya kutimuliwa na sakata la ESCROW je wakati huo akuliona hili? kinachofanyika sasa ni unafiki tu.
 
Kweli nimeamini Profesa Muhongo alikuwa jembe sema kuna mfumo ulikuwa unambana...sasa naona under JPM katoa makucha yake.....ila naomba aangalie na yale mapendekezo ya PAC ahakikishe kila mikataba inayovujisha mapato na kuligharimu taifa inavunjwa.....Ingawa kuvunja mikataba kunaweza kugharimu faini ila kama muda ukiisha mikataba isiongezwe na kukiwa na mbadala wizara ichukue hatua ya haraka....

Hongera Muhongo.....kaza buti sekta ya nishati ni chafu mno.....wasafishe wote watanzania tunakutegemea....maana wanatuibia sana
Hiyo kampuni ulianza kazi mwaka 2013. Wakati huo mhongo ndo alikua waziri wa hiyo hiyo wizara. Atuambie hii kampuni iliwezaje kufanya kazi bila vibali halali? Bado bongo muvi inaendelea
 
Ndugu huo utafiti unaotaka ufanyike ni upi? tambua kuwa kampuni hiyo imeanza kufanya kazi zake mwaka 2013 na ilikuwa haina leseni tangu wakati huo na hailipi chochote, kitu cha msingi ninachotaka nikufahamishe kuwa Muhongo hafai ni vema ukatambua huyu huyu Muhongo alikuwa waziri wa wizara hii kabla ya kutimuliwa na sakata la ESCROW je wakati huo akuliona hili? kinachofanyika sasa ni unafiki tu.
Huyo Muhongo sio malaika kama wewe usivyokuwa malaika pia. Ukiishia kumhukumu mtu kwa kosa moja ukumbuke na yale mema kumi anayoyafanya kwa faida ya taifa (na wewe ukiwemo pia). Kwa mawazo yako unafikiri waziri anao uwezo wa kuona kila kinachofanyika nchini na kuchukua maamuzi ndani ya muda huo huo?. Muhongo anafaa hiyo wizara, yatazame mambo kisomi zaidi, usiyatazame kwa kufuata mkumbo eti kwa sababu fulani hampendi Muhongo na wewe unabebwa na mawazo hafifu ya mtu mwingine. Badilika Mtanzania mwenzangu.
 
Ndugu huo utafiti unaotaka ufanyike ni upi? tambua kuwa kampuni hiyo imeanza kufanya kazi zake mwaka 2013 na ilikuwa haina leseni tangu wakati huo na hailipi chochote, kitu cha msingi ninachotaka nikufahamishe kuwa Muhongo hafai ni vema ukatambua huyu huyu Muhongo alikuwa waziri wa wizara hii kabla ya kutimuliwa na sakata la ESCROW je wakati huo akuliona hili? kinachofanyika sasa ni unafiki tu.
Lowassa alikuwa waziri wa ardhi miaka ya nyuma, unajua rushwa ilikuwa kubwa kiasi gani pale wizarani?. Mbona amekuja kupata kura milioni sita mwaka jana kwenye uchaguzi mkuu?. Sumaye aliitwa Mr. Zero wakati akiwa waziri mkuu, unajua ushawishi wake ulikuwa ni muhimu kiasi gani katika upatikanaji wa hizo kura milioni sita?. Nchi haziongozwi na malaika, zinaongozwa na binadamu wenye kila aina ya udhaifu. Bill Clinton alifanya ufuska na Monica Lewisnky ndani ya white house, lakini unajua kila Clinton anapotoa hotuba akiwa kama mwalikwa analipwa kiasi gani cha dola?. Achana na maisha ya kukariri matukio ya miaka nyuma.
 
Back
Top Bottom