Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Waziri Wa Fedha na Mipango., Dr. Phillip Mpango amelivuruga Bunge. Ni kama amesababisha vurugu zisizo na tija Bungeni. Ni baada ya 'kulitumia' Bunge kupiga kampeni kwa chama chake cha CCM kuelekea Uchaguzi Wa Serikali za Mitaa, Oktoba mwaka huu.
Kiukweli, Waziri Mpango amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali iliyosheheni matumaini makubwa kwa weledi na umakini mkubwa. Ameiwasilisha kwa kuelewekavyema na kwa umahiri mkubwa. Lakini, alipoingiza 'kampeni kwa CCM' aliteleza.
Alianza vyema kutaja sifa zinazofaa kuwepo kwa viongozi wetu na wanaotaka kuwa viongozi wetu. Sifa ya kwanza hadi ya tisa zilikuwa ni sifa za jumla na njema Sana. Ya kumi iliyoleta mtafaruku ilianza vyema kuwa atokane na chama chenye kupigania maslahi ya taifa. Kuitaja CCM ndiyo kuteleza kwenyewe.
Kimsingi, Waziri Mpango hakupaswa kulifanya Bunge kuwa jukwaa LA kampeni kwa CCM. Alisababisha kelele na vurugu zisizo na maana Bungeni. Bunge Si uwanja Wa kampeni Wa chama chochote! Aliteleza na asamehewe.