Waziri Mkuu wangu yu wapi??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu wangu yu wapi???

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KakaKiiza, May 18, 2011.

 1. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,258
  Trophy Points: 280
  Nchi yangu haina waziri Mkuu!
  Niwapi nitapata waziri Mkuu kama E.Moringe??
  Wapi nitapata Naibu waziri Mkuu Kama A.Lyatonga??
  Waziri mkuu umepwaya sisikii ukikemea kwa vitendo zaidi yakukemea kwa maneno bila kuweka vitendo!!
  Waziri Mkuu umekataa Sahangingi nilitegemea waliochini yako watapanda Prado wapi bwana Hata Wakurugenzi wanapanda kama lako ulilolikataa!!!
  Hapa nchi ilipo fikia ndipo E.Moringe alisema naliwe nabadrika siasa za hawa ni wenzetu akaziweka kando!!wafujaji wa mali yaumma wakafukuzwa!!
  Je wewe unasubiri Nini??
  Kama wewe nimtoto wamkulima Vaa viatu vya E.Moringe leo uikwamue hii nchi!!
   
 2. m

  mwacheni77 JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 764
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  La kuvunda.....
   
 3. s

  sawabho JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkuu anajitahidi sana isipokuwa tatizo lipo kwa wale wanaomzunguka na wale waliotarajia kumpa nguvu ili aweze kutekeleza majukumu yake vizuri. Waziri Mkuu kama Kiongozi hatendi majukumu pekee yake yake, yuko ndani ya mfumo wa utendaji kuanzia Mtendaji wa Kijiji hadi ngazi za juu kabisa na kuunganishwa na mfumo wa Kimataifa (Globalization). Kama mfumo huo wote hauko pamoja naye, atamkemea nani na ni nani atamsaidia kutekeleza? Hebu angalia Mawaziri Wakuu uliowataja ambao kwa nyakati fulani kweli walikuwa na nguvu za kuamua, kutenda na kusimamia, aidha angalia mfumo uliokuwepo wakati huo na angalia mwisho wa Mawaziri Wakuu hao waliishia wapi kwa maana hiyo naona baadhi ya viongozi wanaojitahidi kutetea maslahi ya Taifa, mfumo uliopo hauwapi nafasi ya kutenda majukumu yao kwa uhuru.
   
 4. m

  msambaru JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Kaaaaaaaaazi kweli kweli Pinda kapindishwa ndg yangu, unakumbuka mwanzo wa uongozi wake alifumua baadhi ya halmashauri ila ndo hivo wenyewe walimnyooshewa kidole kuwa anawabughudhi vijana wao.
   
 5. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,258
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkuu haitaji kutegemea waliochini yake yeye nikutoa maagizo na wengine kutekeleza!!
  Unataka kuniambia wale wote waliokwapua pesa za umma ilibidi achekenao na aseme nasubiri mahakama itende kazi yake??Kwanza nikuwawajibisha!
  Watu walishapewa angalizo msifanye manunuzi bila ya idhini yangu mwisho wasiku wamefanya manunuzi anakuja kung'aka baadae eti mimi sipandi shangingi!Nawatu wanaendelea nakazi!Watu wanafanya njama za kumubambika mtu Madawa ya kulevya anashutukia anawataja mnawaamisha kituo wewe kama mkuu wa shughuli za serikali!Umwajibishi waziri wa wizara husika!!Vinachomwa moto vibanda ujasema lolote waziri yupo ujambwajibisha wala kutoa agizo la watu hao kushughulikiwa kwa muda hitaji!Ajari zinakwapua maisha ya watu Kamanda wa trafiki nchi nzima yupo na mshahara anakula hakuna jitihada za waziri kiongozi!!Mimi sikubaliani na wewe!!
   
 6. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  yupo kwenye semina,msubili wakati wa maswali ya papo kwa hapo bungeni utamuona.yeye ni waziri mkuu wa kujibu maswali na sio kuwajibika kwa wananchi,kazi ya kuwajibika ni ya chadema.peace and love cdm
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,434
  Likes Received: 19,764
  Trophy Points: 280
  hata mzee wa semina elekezi anatumia sana mgongo wa huu usemi sasa sjui kwa nini yeye yupo juu au anasimamia waliopo juu yake? kina obama na kina cameruni na kina sarkozy
   
 8. e

  erneus kyambo Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo umenena kweli mkubwa! Pinda ni W. Mkuu wa kutoa matumaini na faraja kwa wananchi ili kuwapooza waliovunjika mioyo angulau wavute subira kwa mambo ambayo hatayatekeleza kamwe hatayatekeleza kamwe,Nakumbuka matumaini aliyotupa wana udom alipokuja chuoni kwetu,la leo wapi! Hakunakitu hata moja alilotekeleza.waswahili walisema, 'ni heri kuishi na mwendawazimu uliyemzoea kuliko kichaa mpya!'
  Toka ailipoteuliwa kuwa W.Mkuu nilijua tu huyu hana uwezo kiutendaji bali amewekwa tuu ili kuonyesha usafi wa serikali juu ya ufsadi ulioiganda serikali.
   
 9. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Kwa mfumo wa utawala tulio nao Bongoland (ambao ni mbovu, tuliurithi kutoka kwa wakoloni na kuufanyia marekebisho ya hapa ni pale), WM ni mtekelezaji wa kile anachoelekezwa na Rais. Kwa hivyo, WM ni kama kioo cha Rais mbele ya umma. Kwa mantiki hiyo kama Rais “anajitahidi sana isipokuwa tatizo lipo kwa wale wanaomzunguka” basi hapana shaka na "Waziri Mkuu anajitahidi sana isipokuwa tatizo lipo kwa wale wanaomzunguka." Bila kufanya mageuzi ya kweli ya katiba, ni ndoto ya alinacha kumpata WM anayefanya kazi kwa uhuru wake.
   
 10. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hatuna waziri mkuu
  Tuna waziri mstaarabu
   
 11. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,757
  Trophy Points: 280
  ni rahisi kwa ngamia kuzama tunduni mwa sindano kuliko magamba kuwa kwenye mstari ulionyooka!
  hata wakiapa kwa viapo vywa damu!never ile inakuwaga ni danganya wadanganyika.
   
 12. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,258
  Trophy Points: 280
  Kwakweli inasikitisha mfumo wa utawala unaanzia kwa Waziri Mkuu akishindwa kuwawajibisha watendaji wake inasikitisha sana kwa nchi hii!!
   
 13. B

  BENTA Member

  #13
  May 19, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kama rasi wa nchi aliyechaguliwa kidemokrasia na ni amiri jeshi mkuu ambaye katiba inampa madaraka makubwa kupita kiasi na bado anaogopa kuwachukulia hatua za kinidhamu baadhi ya watu walio chini yake je unategemea waziri mkuu wake afanye nini cha ziada.Naamini tatizo linajulikana liko wapi naomba niishie hapo.
   
 14. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #14
  May 19, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Kwa kizazi hiki hata km ulikuwa msafi kiasi ganui lakini ukiishaingia ndani ya ccm (chama cha mafisadi) lazima ubadilike na uegemee kwa mafisadi....ndiyo maana waziri mkuu wa sasa anaweza hata kusema uongo mbele ya watz na anaweza kutangaza kuwa mafisadi wameishinda nchi kwa hiyo pamoja na kujulikana hawakamatiki....kitamu zaidi watz km kawa tunaendelea kuwapigia makofi...........
  yani baada ya wale waliothbutu enzi zile kusema kwa uwazi na ukweli kuwa "ccm imekosa dira" hapajatokea mwana ccm mwingine yeyote wa kutetea watz zaidi wote wanatetea mafisadi
   
 15. g

  georgelupembe Member

  #15
  May 19, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  PM wetu ni mwaadilifu na mkweli anayejali mno wananchi-tatizo ni mfumo. Watendaji wakuu wote wanateuliwa na Rais na wanawajibika kwake; yeye afanye nini ! Halmashauri zetu anazijua mno na wengi wa watendaji wake wakuu alishatamka kwamba ni wabovu na wabadhilifu lakini kuwawajibisha ni tatizo la mfumo. Mh Pinda kwa tunayemfahamu ni mfuatiliaji mno wa kero za wananchi lakini mfumo wautawala wetu mtendaji mkuu ni Mkuu wa nchi.
   
Loading...