Waziri Mkuu: Wahandisi wajenge majengo kwa kusimamisha matofali ili matofali machache yajenge majengo mengi

Hatuwezi kupinga kila kitu, alichoongea kina mantiki, hasa majengo madogo madogo hakuna haja kulaza tofali.
Maadam msingi, beam na tofali zina kiwango
Ujui unacho kiongea yaani jengo la serikali linatakiwa kudumu kwa miaka isiyopungu sitini ijengwa kwa tofari za kusimama, majengo ya serikali niyakudumu siyo kama kujenga kioski.
 
Naona PM anajali zaidi quantity na si quality.....
Haya buana mheshimiwa "political engineer"
 
Ujui unacho kiongea yaani jengo la serikali linatakiwa kudumu kwa miaka isiyopungu sitini ijengwa kwa tofari za kusimama, majengo ya serikali niyakudumu siyo kama kujenga kioski.
Nipe uzoefu wako ktk ujenzi bosi.
Na uniambie kilichosababisha mipasuko kwenye hostel za magufuli..
Ukinijibu nitasema neno.
Siwezi kubishana na nisiyemjua uwezo wake ktk hili
 
Mkuu ujenzi ni taaluma kama taaluma zingine.
Katika ujenzi jambo la muhimu ka kubwa zaidi ni msingi imara.
Unapoona mpasuko a.k.a expansheni jointi, chanzo chake kikuu ni msingi.
Mjenzi makini huandaa msingi kwa kuzingatia Majole case...haya ni matukio tusiyoyaona lkn hutokea, mojawapo ni tetemeko.
Umewahi kujiuliza:
1. Kwanini kuna sehemu wajenzi hutandaza mchanga laini kwenye msingi?
2. Kwanini msingi wa tofali ni bora kuliko wa mawe?
3. Kwanini udongo hupimwa maabara kabla ya ujenzi?
KUSIMAMISHA TOFALI SIO TATIZO
KWA MJENZI MAKINI.
Ukijua utasimamisha tofali utalazimika
Kuimarisha msingi, beam au hata unaweza kulazimika kuweka columns
Hata kama msingi ukiwa imara kiasi gani injinia hawezi kutoa ushauri Wa kusimamisha tofari kwenye majengo ya kudumu kwa muda mrefu kama ya serikali, unataka kumtetea mh lakini kiukweli kajichanganya sana.
 
Hiyo inaitwa political engineering!
Imebidi tu nicheke . Ndio yale ya nyufa tukaambiwa ni expansion joints ....

Hii course ya political engineering inasomewa wapi maana na mimi niukwae u Dkt kwani thesis yake itakuwa rahisi sana.
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari, miongoni mwa maelekezo aliyotoa amesema wahandisi wajenge majengo Kwa kusimamisha tofali na sio kuzilaza ili tofali chache zijenge majengo mengi.
Kila la heri wahandisi
Ushauri mzuri.
Lakini tuende mbali zaidi na kusema tutumie hollow blocks.
 
Wakuu,

Ujenzi ni engineering, nadhani inaitwa Civil Engineering. Kuna sheria inayoambatana na mambo ya engineering hii hapa chini.
- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
Regulation 66(1) of “Engineers Registration Regulations, GN. No. 35/2010” states,

All engineering materials, products and processes shall have their specifications and standards ascertained by relevant authorities”.

- - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - - -
Hivyo, tofali (brick) lina engineering standards zake, na huyo engineer asipofuata standards za engineering kifungu hiki na vingine vinavyofanana vitamshughulikia.

Huwezikujenga kitu sub-standard
 
Nipe uzoefu wako ktk ujenzi bosi.
Na uniambie kilichosababisha mipasuko kwenye hostel za magufuli..
Ukinijibu nitasema neno.
Siwezi kubishana na nisiyemjua uwezo wake ktk hili
Mimi ni engineer na nimejenga majengo mengi ya kudumu punguzeni propaganda kwa mambo msiyoyajua, rules za civil engineering matofari ya kusimamisha durability ya unacho kijenga ni ni ndogo sana na haishauliwi kabisa kwa majengo ya kudumu. Unless uweke double row kama majengo ya zamani ya mjerumani ambapo utachukua tofari nyingi zaidi.
 
Hata kama msingi ukiwa imara kiasi gani injinia hawezi kutoa ushauri Wa kusimamisha tofari kwenye majengo ya kudumu kwa muda mrefu kama ya serikali, unataka kumtetea mh lakini kiukweli kajichanganya sana.
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari, miongoni mwa maelekezo aliyotoa amesema wahandisi wajenge majengo Kwa kusimamisha tofali na sio kuzilaza ili tofali chache zijenge majengo mengi.
Kila la heri wahandisi
Kuna muda naona bora siye tusiyesoma shule za darasani naona elimu ya mtaani inatosha kabisa
 
Back
Top Bottom