Waziri Mkuu Unawaonea Wadogo

Waziri Mkuu Unawaonea Wadogo

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,202
Reaction score
8,781
Waziri Mkuu Bwn MKPP ametoa muda hadi 01.04.2013 kwa wafanyakazi wa Wilaya ya Bahi wanaoishi Dodoma mjini kuwa wawe wamehamia Wilayani kwao Bahi.

Amesema kuwa kwa kuhamia Wilayani humo wataharakisha maendeleo ya Wilaya hiyo na kuwatumikia wananchi kwa ufanisi.
Wafanyakazi hao walijibu kuwa wangeshahamia wilayani humo, lakini hawajapata barua za uhamisho, wala kusainishwa makubaliano ya uhamisho.

Mtazamo wangu:
Serikali ya MKPP nayo imeshindwa kuhamia Dodoma, na hivyo kuruhusu mpango huo uliodumu kwa zaidi ya miongo mitatu, kugonga mwamba!

Kuna sababu gani ya kuwalazimisha wadogo kuhamia Wilaya mpya, wakati yeye na serikali yake wanafanya kazi remotely kutokea Dar na kuisababishia serikali hasara ya ajabu ya kugharamia misafara, posho za safari na spea za magari bila sababu, huku wakiwa wamejengewa makazi fully furnished Dodma?

Kweli Nyani haoni makalio yake!

Sosi: Newz bulletin 0700 am RFA.
 
jamani kumbukeni mkubwa hakosei ila pengine ana sababu ya msingi zaidi "shadow doesn't force an individual to step"
 
Back
Top Bottom