WAZIRI MKUU RAILA ODINGA aombwa kwenda kusuluhisha IVORY COAST!

Pasco_jr_ngumi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,802
282
Jamani wana JF,
Nimefungulia BBC SWAHILI nimeskia kuwa bwana Odinga ameombwa aende kusuluhisha bwana Gnagbo na Ouattara kule Ivory Coast.
Mwageni maoni, itawezekana kweli akafanikiwa? Je huyu Raila Odinga ni bora kuliko Tabho Mbeki aliyeshndwa? Na vp Kikwete angefaa au! Maana angekwenda Raisi wetu angepewa U-Profesa. Mnasemaje?
 
It all depends on Peoples' Power. Gbagbo aliwekwa na umma, baada ya maandamano kibao wakati aliposhinda uchaguzi, halafu Robert Guei akachakachua na kujidai kuwa yeye ndiye mshindi. Sasa pale Ikulu patamu, sio rahisi kuachia kienyeji. Nguvu ile ile ya umma ndio itamwondoa na wala sio blablah za akina mabwana wadogo hawa akina Raila sijui Thabo na wengineo.
 
Hawezi maana alishasema nguvu ya jeshi itumike kumwondoa Laurent kwa hiyo hataweza kuwa neutral
 
Atakachofanya Odinga ni kumwambia aliyeshinda (Alassane) kukubali "serikali ya umoja wa kitaifa" na kumruhusu aliyeshindwa (Gbagbo) kuendelea kutawala - Crazy african politics!
 
Kwa kusema kweli hii kazi ingekua ni saizi yake JK tu, kwisha kazi.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kwa hapo tusimnyime maksi zake JK namkubali sana ila kwa UFISADI, UDINI na UCHAKACHUAJI hatuko pamoja.

Hakika, sijui kulikotokea wapi hii kashfa ya uchakachuaji wetu huu mpaka mheshimiwa akashikwe na ngozi red-handed AKIHUJUMU DEMOKRASIA sasa ni taabu kweli kweli!!!

Wanadiplomasia wetu siku zote hua hawababaishi kazini!!! Hebu mfikirie Mama Mulamula, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Mkapa na hata JK mwenyewe.
 
wote ndio wale wale labda tumuombe dk slaa raisi wawatanzania aliyoko kwenye mioyo ya watanzania akawasuluhishe
 
wote ndio wale wale labda tumuombe dk slaa raisi wawatanzania aliyoko kwenye mioyo ya watanzania akawasuluhishe

Wazo zuri kwa sababu kwa busara zake adimu sana kashinda moyo wake na machungu yote ya kuibiwa kura ki-sanii ili taifa letu lisiingie kwenye machafuko.

Hata hivyo hizo busara zake Dr Slaa CCM wameanza kuzichukulia for granted kiasi kwamba gear namba moja may, at some point, be inevitable especially on the part of the wananchi ourselves.
 
Wacha nicheke mie! Hivi mnadhani uteuzi wa Raila umekuja hivi hivi? Watu wanaangalia international appeal na respect anayo-enjoy na katika hilo Raila ana wapinzani wachache hapa Afrika na saizi yake katika hilo ni Rais wetu ambaye naye ana heshima ya kutukuka sana. Sasa kuleta ushabiki kwamba Dr. Slaa anafaa kwa sababu tu lilikuwa chaguo la baadhi yetu kwenye uchaguzi ni kuleta utani usio na sababu maana conflict resolution na management ni skills ambazo si kila mtu anazo. In ama zinasomewa au zinatoka na uzoefu wa muda mrefu wa kusuluhisha migogoro. Raila amekuwa victim wa migogoro na alifanikiwa sana kuleta suluhu. JK ameshiriki mashauri mengi ya usuluhisi akiwa Waziri na sasa Rais na mfano ni mgogoro wa Kenya na ile ya Burundi na Comoro. Tuukubali ukweli ili tuheshimike.
 
Nimeshangaa sana, Raila alishasema kuwa njia sahihi ni kutumia nguvu za kijeshi kumwondoa Gbago, sasa huyo huyo ndio awe msuluishi hebu tuone ....!
 
Odinga??, mngefanya la maana kunituma mie tabutupu maana hata ghabo hanijui. Nitakacho mshauri ni kuachia ngazi, aje tumpe hifadhi tanzania. Hata ikulu akitaka nitamfanyia mpango apate room moja kali pale state house.
 
Crazy politics za africa hawana jipya zaidi ya kudanganganyana kwa kuunda serikali ya muungano.Wote hawana jipya wote ni wachakachuaji tu
 
Profes JK anaweza kabisa
Hamna kuwasuluhisha wote wawili kwa pamoja zaidi ya kumwomba anayelazimisha aachie ngazi, la sivyo demodrasia iheshimiwe na atolewe kwa nguvu.
JK wala hawezi, hawezi kwa misingi kua ataleta Serikali ya Kitaifa tu ambapo ni sawa na kubaka demokrasia. Msuluhishi wa kweli pia anatakiwa kuwa na nguvu za uwezo wa kumlazimisha mtu kuachia ikibidi kwa lazima.
 
Back
Top Bottom