Waziri Mkuu Pinda amjulia hali Zitto

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
[h=3][/h]

Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana alifika hospitalini Muhimbili kumjulia hali mbunge Mh. Zitto Kabwealiyelazwa hospitalini hapo akisumbuliwa na malaria. Picha: Hillary Bujiku wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
 
Mbona Slaa, Mbowe wameshindwa kwenda kumjulia hali Zitto, sio bure kuna kitu
 
Kama unakijua hicho kitu si ukiweke wazi, kuliko kuweweseka kuna kitu??

Hivi kweli inaingia akili Zitto Kabwe anaumwa kalazwa siku siku 4 hospital hakuna hata kiongozi mmoja wa CDM aliokwenda kumjulia hali!...

Sasa jiulize kwa nini Dr Slaa, Mbowe, Lissu, Mnyika, hawakwenda kumuona Zitto
 
Katika tasnia ya habari kuna huu msemo: Tembo kumuua sisimizi si habari bali sisimizi kumuua Tembo. Labda niongeze na wa kwangu: Mama kumnyonyesha mtoto si habari labda kichanga kumnyonyesha Mmama!
 
hawawezi kwenda, nafsi zinawasuta kwa walichomfanyia mwenzao.
Mzee,

Tuandike vitu vyenye uhakika, kwenye kuugua mtu msiingize propaganda, haijalishi ni CCM au CUF hata CDM.

Slaa alienda Aga Khan hosp, Mutemelwa alikuwa hosp full time, Dr. Kitila kila siku alikuwapo.

Mbowe sijajua, ila hao niliowataja nina uhakika maana Dr. Kitila alitufahamisha afya ya ZK inavyoendelea akiwa hosp na mwandishi wetu ndo alitoa taarifa ya awali juu ya ZK kuugua na kusema kuwa atapelekwa India japo baadhi ya watu wakaongea via Clouds kuwa haendi na sasa tunaona kapelekwa.

Tuliandika hapa kuwa tatizo la ZK lilikuwa ni kichwa kwa zaidi lkn bado uchunguzi unaendelea, akatokea mtu akasema kuwa ZK anaendelea vema na anaachiwa, hii ilikuwa inapelekea watu kudhani labda ZK si mgonjwa wakathubutu kudai yuko zake twitter tunamchulia.

Ila, ZK kama member wa JF tumtendee haki, tusimwingize kwenye siasa za namna hii, tumwombee apone kama mwana JF na akishapona tuendelee na siasa zetu, mawe yarushwe lakini si kwa fujo, bali kiungwana na tumkome nyani giladi mchana kweupe!
 
Hongera sana Invisible!
Naona umepewa cheo cha msemaji mkuu wa Chadema.
 
Unajuaje kama hawajaenda?!.
Hivi kweli inaingia akili Zitto Kabwe anaumwa kalazwa siku siku 4 hospital hakuna hata kiongozi mmoja wa CDM aliokwenda kumjulia hali!...

Sasa jiulize kwa nini Dr Slaa, Mbowe, Lissu, Mnyika, hawakwenda kumuona Zitto
 
Katika tasnia ya habari kuna huu msemo: Tembo kumuua sisimizi si habari bali sisimizi kumuua Tembo. Labda niongeze na wa kwangu: Mama kumnyonyesha mtoto si habari labda kichanga kumnyonyesha Mmama!
Mchango mzuri mkuu.

Nadhani Mbowe hayupo nchini/jijini. Dr. Kitila anaweza kutufahamisha juu ya hili.

Hosp ZK alikuwa analindwa na vijana wa CDM (sijui ndo red brigade?) na Mhonga alikuwepo katika waliomsindikiza Airport wakati anaelekea India.

ZK hakutaka kwenda India, alitaka atibiwe Muhimbili lkn wakamsisitizia kuwa kichwa wataalam wazuri wapo India.
 
Hongera sana Invisible!
Naona umepewa cheo cha msemaji mkuu wa Chadema.
Poor thinking, and sad to say that.

Mnapenda spinning mpaka mnapitiliza mkuu.

Naongelea ZK kama JF member, sasa wewe kama ni mbunge wa CCM njoo hapa na real name! Tutakupa ushirikiano, mwulize HK, pamoja na kuwa yupo CCM apatapo tatizo tunajitahidi kuwa karibu naye ili kujua anaendeleaje na kama angependa umma ufahamu.

Mkuu, tunapokuwa kwny issues za misiba, magonjwa wekeni pembeni propaganda, haifurahishi na wengine wanadhani ndo watu wa JF walivyo.

Uungwana ni vitendo, hapo nimekupa mfano wa mbunge mmoja wa CCM mwenye guts za kuingia JF kwa jina na kujibu hoja. Namfananisha na ZK ingawa yupo CCM. ZK amekuwa mvumilivu sana humu, japo watu hufikia kumrushia maneno yasiyofaa.

Nirudie, siasa kwny ugonjwa tuweke kando!
 
Hili la viongozi wa Chadema kutokwenda kumjulia hali Zitto lazima likemewe kwa nguvu. Huu unafiki wa kutetea makosa ya wazi hausaidii kitu.
 
Issue imeishakuwa kubwa mpaka Invisible kajitokeza...

Mkuu Invisible, tunashukuru kwa kutujuza
 
Mbona Slaa, Mbowe wameshindwa kwenda kumjulia hali Zitto, sio bure kuna kitu

As a nation we have reached so low hata kwenda kumuona mgonjwa lazima tuite vyombo vya habari! Mufilisi.

Kingine, kama kuna mtu aliyekaribu na huyu mtoto wa mkulima (Pinda) basi amkumbushe ili awe anatazamana na mtu wakati wanasalimiana. Pinda ana tabia ya kutomwangalia mtu machoni wakati ana-shake hands. Tafsiri ya hii ni mbaya sana na kwenye jamiii nyingine ataonekana kama sio mtu mkweli. Nilidhani viongozi wetu wanapata tuition kidogo kuhusu 'etiquette'.
 
Wewe ukijakuzeeka lazima utakuwa mganga wa kienyeji unaonekana mshirikina sana wewe...

Unazijua mpaka tabia za Pinda kuwa akimpa mkono mtu anatizama pembeni du!! wewe kiboko
 
Back
Top Bottom