Waziri Mkuu Mstafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Edward Lowassa azungumzia kustaafu siasa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa amekanusha taarifa zinazosambaa mtandaoni zikidai kuwa ametangaza kustaafu siasa kutokana na chama chake cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupoteza jimbo la Monduli ambalo amewahi kuliongoza.

Lowassa amesema, hana taarifa za matokeo ya uchaguzi wa Monduli kwa kuwa yuko safarini akitokea Arusha kuelekea Dar es salaam wala hajazungumza chochote kuhusiana na kustaafu siasa.

Nani kasema maneno hayo? Mimi niko safarini sijapata 'document' yoyote kuhusu matokeo ya uchaguzi wala sijaongea popote”, amesema Lowassa.

Mapema leo yaliibuka majadiliano kwenye mitandao ya kijamii yakihusisha baadhi ya viongozi pia akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akidai kuwa amepata taarifa kuwa Mjumbe huyo wa kamati kuu ya CHADEMA amestaafu siasa.

Eti nimesikia kuwa Mzee wetu ameamua kuachana kabisa na siasa. Mh Gambo naomba uhakika wa hizi taarifa kwa sababu wewe upo karibu na Monduli”, ameandika Makonda.

Uchaguzi wa marudio katika majimbo ya Ukonga na Monduli umefanyika jana Septemba 16, ambapo aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Monduli kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Julius Kalanga amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Ubunge wa Jimbo hilo kwa kupata ushindi wa kura 65,714 huku mpinzani wake Yonas Laizer wa (CHADEMA)akipata kura 3,187.
 
Makonda na Gambo mbona mnafuatilia maisha binafsi ya Mzee Lowassa? Kawakosea nini? Kwanini hamumuachi akajisemea mwenyewe? Kuweni na Heshima kwa Mzee Lowassa mbona nyinyi hajawasemea mambo yenu?
 
Frederick Sumaye alituambia wameenda CHADEMA ili kuisaidia CCM kuimarika!

Edward Lowassa atastaafu siasa baada ya CCM kuimarika. Au anadhani kwa sasa CCM imeimarika?
Tulionywa kwamba mzee alikuwa na hasira sana na chadema kwa kumchafua lakini hatukusikia. Wacha amalize hasira zake kwa kukisambaratisha kabisa. 2020 wakipata wabunge 5 wamshukuru Mungu sana.
 
Tujifunze kuchambua..ila nadhani wengi tunapenda siasa za kujifurahisha ndio maana kuna jamaa wanataka kutupeleka wanavyotaka kitu ambacho so kizuri haijalishi wewe ni CCM au CDM
 
Back
Top Bottom