Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ahamia upinzani Rasmi - Agosti 22, 2015

Nawapenda sa UKAWA ila hotuba ya SUMAYE ilikua ni mbaya kuliko hotuba zote anajiona yeye ni mjuaji kuliko viongozi wa UKAWA yaani kanichefua mno ningekua ukumbini ningeinuka kumpinga baadhi ya maneno yake aache dharau maramoja na hilo jambo aambiwe asijifanye anjua kuliko viongozi wa ukawa.

Kipi kilikuudhi pale ndiyo mwisho wa upeo wake
 
Sumaye katusaidia make tunaelewa na anachokifanya ni kuwabomoa Ukawa ..kwanza kaanza kwa kuwadharau ila wenyeji hawajajishutukia, kasema mwenyewe kaja kuiimarisha CCM ila wameshindwa kumsoma na sasa imewasaidia watu kutegeu, ukawa wanageuka CCM B ..hawana sera wala ilani wanasubiri kuletewa na wana CCM waliokaa CCM maisha yao yote, hawa leo ndo wanageuka injini wakati wao ni sehemu ya waliouweka mfumo wa CCM mnaoulaumu ..huko kwenu wanaleta jipi jipya?
 
Najaribu kukumbuka alichoongea sumaye jana alipokuwa akitangaza kujiunga ukawa naona kama hakujiandaa vizuri kulikuwa na reverse nyingi. maana sjui hata katika huo ukawa atachukua kadi ya chama gani kati ya vyama vinavyounda ukawa ingawa amesema atajua mbele kwa mbele.

Kubwa ni hili la kupeleka uzoefu huko ukawa kwa madai ya kuwa waziri mkuu kwa muda mrefu. wakati wa uwaziri mkuu wake TAMISEMI iliondolewa kwenye ofisi yake baaba ya miaka mitano ya kwanza, na kupelekwa ofisini kwa rais. sasa ni kwanini TAMISEMI iliondolewa kwenye ofisi ya waziri mkuu wakati wake, majibu anayo yeye.

Mkapa alipoondoa TAMISEMI ofisini kwa waziri mkuu na kuipeleka ofisini kwake maana yake Mkapa alikua anafanya mpaka kazi za waziri mkuu. sumaye alibaki na kazi ya kuisimamia serikali bungeni na kuwa katibu wa baraza la mawaziri tu.

Sasa huu uzoefu anaotaka kuupeleka ukawa sijaujua ni upi kama alishindwa kumsaidia Mkapa wakati wa uwaziri mkuu wake

Waosha vinywa bana....

Kwahiyo ulikuwa unasubiri mpaka Kikwete ajikanyage pale jangwani ndio useme...

Huwezi kuelewa kwasababu hata mwenyekiti wako hakumwelewa
 
Watanzania tunataka kujua ni kwa nini uliuza nyumba za serikali? Haukuwa na uchungu na nchi hii tukuaminije sasa hivi?
 
Sumaye ameongea vizuri tu na ameweka bayana sababu za kujiunga na UKAWA. Rudia kuangalia video clip ile kwa utulivu na " Utamuelewa'
 
Hii ni kashfa kwa UKAWA sio Sumaye tena. Hii ilikua ni pointi kubwa sana ya kummaliza Pombe Magufuli. Sumaye alikua bosi wa Magufuli, sijui atalizungumziaje hili? Kitakachomuokoa hasa baada ya kusemwa sana leo pale Jangwani inabidi naye aje na ushahidi kwamba amri "ilitoka mamlaka za juu". Hapa atakua ametuokoa.
 
Yani umeandika haya baada ya kumsikia Kikwete?
Mbona kabla Kikwete hajaongea hukuyasema haya?

Mkuu hao ndo watu wenye akili za ku-pump (mpaka asikie wengine wamesema ndo na yeye anakurupuka), yaani jamaa sijui alikuwa wapi kuileta hii hoja hiyo jana?
 
Najaribu kukumbuka alichoongea sumaye jana alipokuwa akitangaza kujiunga ukawa naona kama hakujiandaa vizuri kulikuwa na reverse nyingi. maana sjui hata katika huo ukawa atachukua kadi ya chama gani kati ya vyama vinavyounda ukawa ingawa amesema atajua mbele kwa mbele.

Kubwa ni hili la kupeleka uzoefu huko ukawa kwa madai ya kuwa waziri mkuu kwa muda mrefu. wakati wa uwaziri mkuu wake TAMISEMI iliondolewa kwenye ofisi yake baaba ya miaka mitano ya kwanza, na kupelekwa ofisini kwa rais. sasa ni kwanini TAMISEMI iliondolewa kwenye ofisi ya waziri mkuu wakati wake, majibu anayo yeye.

Mkapa alipoondoa TAMISEMI ofisini kwa waziri mkuu na kuipeleka ofisini kwake maana yake Mkapa alikua anafanya mpaka kazi za waziri mkuu. sumaye alibaki na kazi ya kuisimamia serikali bungeni na kuwa katibu wa baraza la mawaziri tu.

Sasa huu uzoefu anaotaka kuupeleka ukawa sijaujua ni upi kama alishindwa kumsaidia Mkapa wakati wa uwaziri mkuu wake
Maneno ya wakosaji tuelezeni kwanza ela ya escrow na gesi yetu inarud lini
 
Watanzania tunataka kujua ni kwa nini uliuza nyumba za serikali? Haukuwa na uchungu na nchi hii tukuaminije sasa hivi?

Makufuri na Mkapa ndiyo waliyouza nyumba za serikali, Sumaye alitoa ushauri baraza la mawaziri, lakini MKAPA kwa kumtumia Magufuri ndiyo waliyouza Nyumba Za Serikali, Mkapa akashinikiza,Makufuri akamalizia. Uliza Kwanza Usibweteke
 
Back
Top Bottom