Queen Esther
JF-Expert Member
- Apr 5, 2012
- 2,195
- 1,417
Mhe. Kassim Majaliwa anaendelea na ziara Mkoani Morogoro. Mkoa ambao mpaka sasa ndani ya miaka mitatu Wakurugenzi sita tayari wametumbuliwa kutokana na matumizi mabaya ya fedha.
Jambo hili linaleta sintofahamu kwanini wakurugenzi wanatumbuliwa hivi? Je! Tatizo ni viongozi wa Mkoa? Hawa Wakurugenzi wanasimamiwa na RC & RAS. Inakuwaje mpaka viongozi wa Kitaifa ndio wanakuja kutoa maagizo na kufichua wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka?? Wataalamu wa mambo ya utawala karibuni mshauri Mkoa huu unaotumbukia na kuporomoka kila kukicha. Hata kwenye kilimo ulikuwa Mkoa wa kwanza sasa umetupiliwa mbali.
Mojawapo ya kauli za Mhe. Majaliwa hivi leo ni hii hapa;
"Taarifa zangu Zinaonyesha Mkoa wa Morogoro Kuna Walaji Pamoja na Jitihada za Kukusanya Mapato lakini Kuna Wajanja Wachache. Halmashauri ya Ifakara zaidi ya Milioni 700 Hazijapelekwa Benki zimeishia mikononi mwa Wajanja Wachache".
Hivi mil 700 hazijapelekwa Bank? Ulanga kumeibwa 2.9 bilioni kwa mujibu wa Mhe. Jafo na Mkurugenzi akatumbuliwa. Moro vijijini pesa za ujenzi hosp ya wilaya zimechapwa, dawa ya mchwa mil 60 nk. Wakurugenzi wawili tayari wametumbuliwa. Hivyo hivyo Kilosa, Malinyi nk
Hosp ya Wilaya na Kituo cha Afya Malinyi kuna shida kubwa.
Lazima tukae chini tujiulize shida iko wapi?? Hongera Mhe. Kassim Majaliwa kwa uchapa kazi uliotukuka usiomuogopa mtu. Tuna imani na wewe. Endelea kufukua.
Queen Esther
Updates....
Morogoro : PM amtaka DED na wenzake kulipa Bil 1
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika Halmashauri mbili za Wilaya ya Kilombero, kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha zaidi ya Sh. Bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani.
Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi ha leo (Jumapili, Septemba 15, 2019) wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.
Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Watumishi hao ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Fransis Ndulane anayedaiwa sh. milioni tano alizoingiziwa katika akaunti yake bila maelezo yeyote.
Amesema “Mkoa mzima wa Morogoro umekuwa na tatizo la upotevu wa mapato, fedha zinakusanywa zinapita mikononi mwa watu hazifiki benki, hii ni shida, hatutavumilia.”
Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi juni 2019, Katika mji wa Ifakara makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7 ambapo fedha iliopelekwa bank ni shilingi bilioni 1.9 na kwamba kiasi cha shilingi milioni 727 hazijulikani zilipoenda.
Katibu wa CCM Moro Mhe. Shaka amwambia Mhe. Majaliwa hali hii haikubaliki ktk Mkoa wake. Lazima maamuzi magumu yafanyike.
Updates...
DC na DED Wilaya ya Malinyi wametumbuliwa. Ulanga watumishi waliohusika na ubadhirifu kusimamishwa kazi na kupelekwa mahakamani. Mhe. Majaliwa anaendelea kutema chechheeee... stay tuned Moro Vijijini Mbunge amechomoa betri.