Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aibua madudu mazito Mkoa wa Morogoro

Queen Esther

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
2,195
1,417
Mhe. Kassim Majaliwa anaendelea na ziara Mkoani Morogoro. Mkoa ambao mpaka sasa ndani ya miaka mitatu Wakurugenzi sita tayari wametumbuliwa kutokana na matumizi mabaya ya fedha.

Jambo hili linaleta sintofahamu kwanini wakurugenzi wanatumbuliwa hivi? Je! Tatizo ni viongozi wa Mkoa? Hawa Wakurugenzi wanasimamiwa na RC & RAS. Inakuwaje mpaka viongozi wa Kitaifa ndio wanakuja kutoa maagizo na kufichua wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka?? Wataalamu wa mambo ya utawala karibuni mshauri Mkoa huu unaotumbukia na kuporomoka kila kukicha. Hata kwenye kilimo ulikuwa Mkoa wa kwanza sasa umetupiliwa mbali.

Mojawapo ya kauli za Mhe. Majaliwa hivi leo ni hii hapa;
"Taarifa zangu Zinaonyesha Mkoa wa Morogoro Kuna Walaji Pamoja na Jitihada za Kukusanya Mapato lakini Kuna Wajanja Wachache. Halmashauri ya Ifakara zaidi ya Milioni 700 Hazijapelekwa Benki zimeishia mikononi mwa Wajanja Wachache".

Hivi mil 700 hazijapelekwa Bank? Ulanga kumeibwa 2.9 bilioni kwa mujibu wa Mhe. Jafo na Mkurugenzi akatumbuliwa. Moro vijijini pesa za ujenzi hosp ya wilaya zimechapwa, dawa ya mchwa mil 60 nk. Wakurugenzi wawili tayari wametumbuliwa. Hivyo hivyo Kilosa, Malinyi nk
Hosp ya Wilaya na Kituo cha Afya Malinyi kuna shida kubwa.

Lazima tukae chini tujiulize shida iko wapi?? Hongera Mhe. Kassim Majaliwa kwa uchapa kazi uliotukuka usiomuogopa mtu. Tuna imani na wewe. Endelea kufukua.

Queen Esther

Updates....
Morogoro : PM amtaka DED na wenzake kulipa Bil 1

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika Halmashauri mbili za Wilaya ya Kilombero, kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha zaidi ya Sh. Bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani.

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi ha leo (Jumapili, Septemba 15, 2019) wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Watumishi hao ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Fransis Ndulane anayedaiwa sh. milioni tano alizoingiziwa katika akaunti yake bila maelezo yeyote.

Amesema “Mkoa mzima wa Morogoro umekuwa na tatizo la upotevu wa mapato, fedha zinakusanywa zinapita mikononi mwa watu hazifiki benki, hii ni shida, hatutavumilia.”

Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi juni 2019, Katika mji wa Ifakara makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7 ambapo fedha iliopelekwa bank ni shilingi bilioni 1.9 na kwamba kiasi cha shilingi milioni 727 hazijulikani zilipoenda.

Katibu wa CCM Moro Mhe. Shaka amwambia Mhe. Majaliwa hali hii haikubaliki ktk Mkoa wake. Lazima maamuzi magumu yafanyike.

Updates...
DC na DED Wilaya ya Malinyi wametumbuliwa. Ulanga watumishi waliohusika na ubadhirifu kusimamishwa kazi na kupelekwa mahakamani. Mhe. Majaliwa anaendelea kutema chechheeee... stay tuned Moro Vijijini Mbunge amechomoa betri.
 
Watu walishazoea Moro ni kuja, kupiga hela na kutoweka! Miradi mingi sio endelevu. Ndio mana Bosi wa ardhi na nyumba aliwaharibia maafisa ardhi kwa kuwatawanya sehemu mbalimbali.
 
Kebwe Steven Kebwe naona kakalia kuti kavu maana kila siku Morogoro yanaibuliwa madudu kwenye Halmashauri zake

Yawezekana pia na suala la kuteuwa Wakurugenzi wa halmashauri za miji manispaa na majiji bila kuwafanyia vetting, kuwapa semina elekezi hasa juu ya misingi ya uongozi,mbinu, maarifa, kanuni na taratibu za kusimamia miradi na fedha za umma ndio zinapelekea uvujaji huu wa kutisha wa fedha za umma
 
Shida RC, tumbua RC Steven Kabwe na RAS wake, mambo yatakuwa mazuri kabisa, alafu wamtafute mtendaji kama mm, Jay One uone mambo ya moto, mkoa wa Moro utaongoza kwa chakula Tanzania
 
Kwa bahati mbaya vyombo vya dola vimefungwa mdomo na vinatakiwa kusifia tu, hayo ndio madhara ya kudhibiti vyombo vya habari ambavyo vingeweza kuripoti huo ubadhirifu. Na ifahamike hilo tatizo sio Morogoro tu bali mikoa yote, na wapigaji wameshajua vyombo vya habari siku hizi haviripoti wizi hivyo watu wanapiga tu. Halafu hao wezi wameshajua kula na kipofu, kazi yao ni kuimba sifa za awamu ya tano, kumbe ni kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa. Huo mwenendo wa kusubiri waziri mkuu afike ndio aibue wizi watu watapiga mpaka tuchanganyikiwe.
 
Eti suluhu ni kufukuza watu kazi
Believe me hata mkibadilisha kila wiki wizi hautaisha nchi hii maana ipo kwenye damu
 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika halmashauri mbili za wilaya ya Kilombero na kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha zaidi ya sh. bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani.

Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Watumishi hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Fransis Ndulane anayedaiwa sh. milioni tano alizoingiziwa katika akaunti yake bila maelezo yeyote.

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi ha oleo (Jumapili, Septemba 15, 2019) wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

Amesema “Mkoa mzima wa Morogoro umekuwa na tatizo la upotevu wa mapato, fedha zinakusanywa zinapita mikononi mwa watu hazifiki benki, hii ni shida, hatutavumilia.”

Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi juni 2019, Katika mji wa Ifakara makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7 ambapo fedha iliopelekwa bank ni shilingi bilioni 1.9 na kwamba kiasi cha shilingi milioni 727 hazijulikani zilipoenda.

Amesema katika mitambo kumi ya ukusanyaji wa mapato iliokaguliwa imeonyesha kiasi cha shilingi milioni 348 zilizokusanywa hazikupelekwa bank na hivyo kuishia mikononi mwa watu.

Waziri Mkuu amesema katika uchunguzi huo ilibainika kuwa fedha hizo ziliingizwa katika akaunti mbalimbali za watumishi wa halamshauri hizo kutoka kwa mtendaji wa Kata ya Viwanja 60 katika Mji wa Ifakara aitwaye Gregory Midas.

Watumishi hao ni Reina Mrema ambaye anadaiwa kuchukua kiasi cha shilingi 298, Haile Njitango milioni 73 , Linus Mdembo kiasi cha shilingi milioni 2 kwa kushirikiana na mtendaji huyo wa Kata.

Hata hivyo Waziri Mkuu ameagiza Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika halmashauri ya Mji wa Ifakara, John Mvanga ambaye ndiye alibaini kuwepo na ubadhilifu wa fedha hizo na badae kusimamishwa kazi, arejeshwe kazini mara moja na asibugudhiwe.

“Mlimsimamisha kazi kwa sababu mlijua amegundua madudu yenu, lakini haisaidi, arejeshwe kazini naagiza apewe ulinzi wakutosha.”

Kwa upande wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero, Waziri Mkuu amesema zaidi ya sh. milioni 600 hazijulikani zilipo huku kiasi cha shilingi milioni 98.5 zikidaiwa kuingizwa katika akaunti za watumishi wa halamshauri hiyo bila maelezo yeyote.

Waziri Mkuu amewataja watumishi hao kuwa ni Devid Onyango aliyechukua kiasi cha milioni 51, Elakada Kanongole milioni 36, Fork Karunde milioni 8 na Charlse Chali milioni 2.5.Amesema kati ya milioni hizo 600 kampuni ya Kilombero Plantation LTD (KPL) ambao wanadaiwa kiasi cha shilingi milioni 531 ambazo hazikuingizwa katika mfumo huo.
 
Eti suluhu ni kufukuza watu kazi
Believe me hata mkibadilisha kila wiki wizi hautaisha nchi hii maana ipo kwenye damu
Mbona kuna Mikoa ma DED hawajatumbuliwa tangu wateuliwe mpaka leo. Acha ku exagerate! Think crtitically na jitahidi kuwa na objective na sio subjective critism.

Queen Esther
 
Kwa bahati mbaya vyombo vya dola vimefungwa mdomo na vinatakiwa kusifia tu, hayo ndio madhara ya kudhibiti vyombo vya habari ambavyo vingeweza kuripoti huo ubadhirifu. Na ifahamike hilo tatizo sio Morogoro tu bali mikoa yote, na wapigaji wameshajua vyombo vya habari siku hizi haviripoti wizi hivyo watu wanapiga tu. Halafu hao wezi wameshajua kula na kipofu, kazi yao ni kuimba sifa za awamu ya tano, kumbe ni kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa. Huo mwenendo wa kusubiri waziri mkuu afike ndio aibue wizi watu watapiga mpaka tuchanganyikiwe.

Taarifa hizi umezipata kupitia vyombo gani kama vimefungwa midomo?

Queen Esther
 
Watu walishazoea Moro ni kuja, kupiga hela na kutoweka! Miradi mingi sio endelevu. Ndio mana Bosi wa ardhi na nyumba aliwaharibia maafisa ardhi kwa kuwatawanya sehemu mbalimbali.

Morogoro : PM amtaka DED na wenzake kulipa Bil 1

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika Halmashauri mbili za Wilaya ya Kilombero, kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha zaidi ya Sh. Bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani.

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi ha leo (Jumapili, Septemba 15, 2019) wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Watumishi hao ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Fransis Ndulane anayedaiwa sh. milioni tano alizoingiziwa katika akaunti yake bila maelezo yeyote.

Amesema “Mkoa mzima wa Morogoro umekuwa na tatizo la upotevu wa mapato, fedha zinakusanywa zinapita mikononi mwa watu hazifiki benki, hii ni shida, hatutavumilia.”

Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi juni 2019, Katika mji wa Ifakara makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7 ambapo fedha iliopelekwa bank ni shilingi bilioni 1.9 na kwamba kiasi cha shilingi milioni 727 hazijulikani zilipoenda.
 
Report Ya Gari La Mafuta Nadhani Ikiunganishwa Na Makandokando Basi Tutaenda Sawa Sawa. Morogoro Municipal Maji Safi Ni Tatizo Sugu
 
Akitoka Ifakara aende Morogoro vijijini hasa kwenye kata ya Selembala, akawasikilize wanachi waliopitiwa na mradi mkubwa wa bwawa la Kidunda wamueleze madudu yaliyofanywa na viongozi wa mkoa huo
 
Ndio raha ya sehemu kuongozwa na wapinzani.. Ubadhirifu lazima uonekane.. Hizo hslmashsuri zote zinaongozwa na Chadema na wabunge wake ni wa Chadema
 
Rc wa moro ni hopeless kabisa yaani wizi wote huo bado yupo ofisini nashauri wamuweke ndani kwa muda kashindwa kumsaidia raisi wetu
 
UPUUZI MTUPU! Yeye mwenyewe FISADI huyo. Ni lini ataipeleka ripoti ya CAG iliyotolewa March, 2019 ili ikajadiliwe na Wabunge!?

Mhe. Kassim Majaliwa anaendelea na ziara Mkoani Morogoro. Mkoa ambao mpaka sasa ndani ya miaka mitatu Wakurugenzi sita tayari wametumbuliwa kutokana na matumizi mabaya ya fedha.

Jambo hili linaleta sintofahamu kwanini wakurugenzi wanatumbuliwa hivi? Je! Tatizo ni viongozi wa Mkoa? Hawa Wakurugenzi wanasimamiwa na RC & RAS. Inakuwaje mpaka viongozi wa Kitaifa ndio wanakuja kutoa maagizo na kufichua wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka?? Wataalamu wa mambo ya utawala karibuni mshauri Mkoa huu unaotumbukia na kuporomoka kila kukicha. Hata kwenye kilimo ulikuwa Mkoa wa kwanza sasa umetupiliwa mbali.

Mojawapo ya kauli za Mhe. Majaliwa hivi leo ni hii hapa;
"Taarifa zangu Zinaonyesha Mkoa wa Morogoro Kuna Walaji Pamoja na Jitihada za Kukusanya Mapato lakini Kuna Wajanja Wachache. Halmashauri ya Ifakara zaidi ya Milioni 700 Hazijapelekwa Benki zimeishia mikononi mwa Wajanja Wachache".

Hivi mil 700 hazijapelekwa Bank? Ulanga kumeibwa 2.9 bilioni kwa mujibu wa Mhe. Jafo na Mkurugenzi akatumbuliwa. Moro vijijini pesa za ujenzi hosp ya wilaya zimechapwa, dawa ya mchwa mil 60 nk. Wakurugenzi wawili tayari wametumbuliwa. Hivyo hivyo Kilosa, Malinyi nk
Hosp ya Wilaya na Kituo cha Afya Malinyi kuna shida kubwa.

Lazima tukae chini tujiulize shida iko wapi?? Hongera Mhe. Kassim Majaliwa kwa uchapa kazi uliotukuka usiomuogopa mtu. Tuna imani na wewe. Endelea kufukua.

Queen Esther

Updates....
Morogoro : PM amtaka DED na wenzake kulipa Bil 1

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika Halmashauri mbili za Wilaya ya Kilombero, kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha zaidi ya Sh. Bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani.

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi ha leo (Jumapili, Septemba 15, 2019) wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Watumishi hao ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Fransis Ndulane anayedaiwa sh. milioni tano alizoingiziwa katika akaunti yake bila maelezo yeyote.

Amesema “Mkoa mzima wa Morogoro umekuwa na tatizo la upotevu wa mapato, fedha zinakusanywa zinapita mikononi mwa watu hazifiki benki, hii ni shida, hatutavumilia.”

Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi juni 2019, Katika mji wa Ifakara makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7 ambapo fedha iliopelekwa bank ni shilingi bilioni 1.9 na kwamba kiasi cha shilingi milioni 727 hazijulikani zilipoenda.

Katibu wa CCM Moro Mhe. Shaka amwambia Mhe. Majaliwa hali hii haikubaliki ktk Mkoa wake. Lazima maamuzi magumu yafanyike.
 
Mbona kuna Mikoa ma DED hawajatumbuliwa tangu wateuliwe mpaka leo. Acha ku exagerate! Think crtitically na jitahidi kuwa na objective na sio subjective critism.
Queen Esther

Hapo kwenye bil. 2.9 hapo ya Ulanga, ni kweli DED wa hiyo wilaya ametumbuliwa kwa ubadhirifu? Huyo jamaa nina bifu naye sana huyo na sitaiweka hapa maana wasaidizi wake watanishtukia tu.
 
Back
Top Bottom