Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aibua madudu mazito Mkoa wa Morogoro

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi wanane wa halmashauri ya wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na kuagiza wafikishwe mahakamani kujibu tuhuma za ubadhilifu wa zaidi ya sh. bilioni tatu za mapato ya ndani.

Amesema watumishi wa umma wanawajibu wa kufanya kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu. “Nawasihi nyote muache kufanya kazi kwa mazoea, mbadilike na kuenenda sawa na matakwa na maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Tano na anayejiona hatoshi ajiondoe.”

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi hao leo (Jumatatu, Septemba 16, 2019) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo uliopo mjini Mahenge.

Watumishi hao kuwa ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Yusuph Semguruka ambaye kwa sasa amehamishiwa TAMISEMI, Rajabu Siriwa (mwekahazina), Stanley Nyange, Jonson Mwenyembole, Isack Mwansokope, Said Majaliwa, Charles Steven na Hezron Lopa.

Pia, Waziri Mkuu ametumia kikao hicho kumrejesha kazini na kumpandisha kuwa mkuu wa Idara ya Ukaguzi wa Ndani, Agustine Mwaria ambaye awali alikuwa akikaimu nafasi na kuibua ubadhilifu huo. Baada ya kuibua ubadhilifu huyo mtumishi huyo alisimamishwa kazi.

Waziri Mkuu amewataka watumishi hao wazingatie sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi pamoja na kujiepusha na vitendo vya wizi kwa sababu wanaoathirika baada ya wao kuchukuliwa hatua za kisheria ni wenza wao na watoto.

Awali,Mkuu wa wilaya ya Ulanga, Ngollo Malenya alisema wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto wa ubadhilifu wa fedha za umma hali inayosababisha kuwepo kwa mpasuko kati ya watumishi na Baraza na Madiwani. Alisema watumishi wanaotekeleza majukumu yao ipasavyo wanaandamwa.
 
Haya mambo yanaleta swali moja tu, ni nini kazi ya hawa ma DC na ma RC kama mpaka PM aje kufanya usafi huu?
 
Mhe. Kassim Majaliwa anaendelea na ziara Mkoani Morogoro. Mkoa ambao mpaka sasa ndani ya miaka mitatu Wakurugenzi sita tayari wametumbuliwa kutokana na matumizi mabaya ya fedha.

Jambo hili linaleta sintofahamu kwanini wakurugenzi wanatumbuliwa hivi? Je! Tatizo ni viongozi wa Mkoa? Hawa Wakurugenzi wanasimamiwa na RC & RAS. Inakuwaje mpaka viongozi wa Kitaifa ndio wanakuja kutoa maagizo na kufichua wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka?? Wataalamu wa mambo ya utawala karibuni mshauri Mkoa huu unaotumbukia na kuporomoka kila kukicha. Hata kwenye kilimo ulikuwa Mkoa wa kwanza sasa umetupiliwa mbali.

Mojawapo ya kauli za Mhe. Majaliwa hivi leo ni hii hapa;
"Taarifa zangu Zinaonyesha Mkoa wa Morogoro Kuna Walaji Pamoja na Jitihada za Kukusanya Mapato lakini Kuna Wajanja Wachache. Halmashauri ya Ifakara zaidi ya Milioni 700 Hazijapelekwa Benki zimeishia mikononi mwa Wajanja Wachache".

Hivi mil 700 hazijapelekwa Bank? Ulanga kumeibwa 2.9 bilioni kwa mujibu wa Mhe. Jafo na Mkurugenzi akatumbuliwa. Moro vijijini pesa za ujenzi hosp ya wilaya zimechapwa, dawa ya mchwa mil 60 nk. Wakurugenzi wawili tayari wametumbuliwa. Hivyo hivyo Kilosa, Malinyi nk
Hosp ya Wilaya na Kituo cha Afya Malinyi kuna shida kubwa.

Lazima tukae chini tujiulize shida iko wapi?? Hongera Mhe. Kassim Majaliwa kwa uchapa kazi uliotukuka usiomuogopa mtu. Tuna imani na wewe. Endelea kufukua.

Queen Esther

Updates....
Morogoro : PM amtaka DED na wenzake kulipa Bil 1

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika Halmashauri mbili za Wilaya ya Kilombero, kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha zaidi ya Sh. Bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani.

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi ha leo (Jumapili, Septemba 15, 2019) wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Watumishi hao ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Fransis Ndulane anayedaiwa sh. milioni tano alizoingiziwa katika akaunti yake bila maelezo yeyote.

Amesema “Mkoa mzima wa Morogoro umekuwa na tatizo la upotevu wa mapato, fedha zinakusanywa zinapita mikononi mwa watu hazifiki benki, hii ni shida, hatutavumilia.”

Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi juni 2019, Katika mji wa Ifakara makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7 ambapo fedha iliopelekwa bank ni shilingi bilioni 1.9 na kwamba kiasi cha shilingi milioni 727 hazijulikani zilipoenda.

Katibu wa CCM Moro Mhe. Shaka amwambia Mhe. Majaliwa hali hii haikubaliki ktk Mkoa wake. Lazima maamuzi magumu yafanyike.
Rais Mwizi, MaRC wezi, MaDC wezi, MaDED wezi, yaani kila mahali wizi tu.
 
Waziri mkuu yupo ziarani mkoani morogoro. Katika ziara yake, Mhe waziri mkuu ameibua madudu mengi yaliyokuwa yakifanyika katika wilaya mbalimbali za mkoa wa morogoro. Tumeona baadhi ya viongozi wa serikali wakichukuliwa hatua na wengine kutenguliwa katika nafasi zao. Mambo yote haya yamefanyika huku mkoa huo ukiwa na mkuu wa mkoa ambae ameonyesha udhaifu mkubwa sana wa kusimamia shughuli za serikali. Dk Kebwe kama mkuu wa mkoa wa morogoro anarudisha nyuma jitihada za Mhe Rais za kuwatumikia watanzania. Nae pia anapaswa kutenguliwa kama ilivyofanyika kwa wakurugenzi na mkuu wa wilaya ya Malinyi. Ameonyesha udhaifu mkubwa
 
RC anaweza kuwa ni tatizo kwa maana ya kushindwa kuwasimamia watumishi wengine lakini pia RC anaweza asiye chanzo cha tatizo kwa sababu watumishi wengine wanaoshindwa kujisimamia sio mamlaka yake ya nidhamu na uwajibikaji.

kuna uwezekano wa tatizo la Morogoro likawa limeanzia mbali, naamini serikali sikivu ya Rais Magufuli inalifuatilia kwa makini.
 
Watu wake wa karibu wamwambie huyu daktari kuwa siku zake za kuwa mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa Mkoa zinahesabiwa. Kwa madudu yale huku ripoti ya ajali ya moto hijatoka, sioni akipona.
 
Morogoro mkoa mzima kweli ni shida,mbona mambo yako wazii.Vijijini ndio usiseme,Waziri Mkuu karibu Mvomero,huku nako mambo si swari,it is business as usual,ni kama Magufuli hayupo hivii.
Duuuu!! Balaaaa. Morogoro Vijijini kwa Mhe. Mgumba NW Kilimo tayari kumeondoa ma DED wawili na hali bado ni tete. Dawa ni kuwapeleka mahakamani kama PM alivyofanya kule Ulanga.

Queen Esther
 
Kumekucha! Ni kuchongeana tu

Updates...
DC na DED Wilaya ya Malinyi wametumbuliwa. Ulanga watumishi waliohusika na ubadhirifu kusimamishwa kazi na kupelekwa mahakamani. Mhe. Majaliwa anaendelea kutema chechheeee... stay tuned Moro Vijijini Mbunge amechomoa betri
 
Ziara ya Waziri mkuu mkoa wa Morogoro umebaini madudu mengi na ya ovyoo mno utazani hakuna mkuu wa mkoa. Km madudu haya yanafanyika wakati mkuu wa mkoa upo na unaendelea kupokea mshahara bure, kuna haja gani ya uwepo wa mkuu wa mkoa. Nazani katibu mkuu wa CCM alikua sahihi aliposema hutoshi na alishangaa kwanini hadi sasa hujatumbuliwa. Mtaani kuna njaa kali lakini kwa uzembee huu njoo tugange ote kitaa naona umeshindwa kabsa kumsaidia mzee baba. Nazani kakuvumilia sn.
 
Mkoani kuna Takukuru, polisi, usalama wa taifa, jeshi nk, hao pia walikua wapi wakati ufisadi huo unafanyika? Zigo la lawama apewe rc au kudhibiti ufisadi na rushwa ni kazi ya rc tu?
 
Mhe. Kassim Majaliwa anaendelea na ziara Mkoani Morogoro. Mkoa ambao mpaka sasa ndani ya miaka mitatu Wakurugenzi sita tayari wametumbuliwa kutokana na matumizi mabaya ya fedha.

Jambo hili linaleta sintofahamu kwanini wakurugenzi wanatumbuliwa hivi? Je! Tatizo ni viongozi wa Mkoa? Hawa Wakurugenzi wanasimamiwa na RC & RAS. Inakuwaje mpaka viongozi wa Kitaifa ndio wanakuja kutoa maagizo na kufichua wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka?? Wataalamu wa mambo ya utawala karibuni mshauri Mkoa huu unaotumbukia na kuporomoka kila kukicha. Hata kwenye kilimo ulikuwa Mkoa wa kwanza sasa umetupiliwa mbali.

Mojawapo ya kauli za Mhe. Majaliwa hivi leo ni hii hapa;
"Taarifa zangu Zinaonyesha Mkoa wa Morogoro Kuna Walaji Pamoja na Jitihada za Kukusanya Mapato lakini Kuna Wajanja Wachache. Halmashauri ya Ifakara zaidi ya Milioni 700 Hazijapelekwa Benki zimeishia mikononi mwa Wajanja Wachache".

Hivi mil 700 hazijapelekwa Bank? Ulanga kumeibwa 2.9 bilioni kwa mujibu wa Mhe. Jafo na Mkurugenzi akatumbuliwa. Moro vijijini pesa za ujenzi hosp ya wilaya zimechapwa, dawa ya mchwa mil 60 nk. Wakurugenzi wawili tayari wametumbuliwa. Hivyo hivyo Kilosa, Malinyi nk
Hosp ya Wilaya na Kituo cha Afya Malinyi kuna shida kubwa.

Lazima tukae chini tujiulize shida iko wapi?? Hongera Mhe. Kassim Majaliwa kwa uchapa kazi uliotukuka usiomuogopa mtu. Tuna imani na wewe. Endelea kufukua.

Queen Esther

Updates....
Morogoro : PM amtaka DED na wenzake kulipa Bil 1

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi watumishi saba katika Halmashauri mbili za Wilaya ya Kilombero, kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha zaidi ya Sh. Bilioni 1.3 za makusanyo ya mapato ya ndani.

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi ha leo (Jumapili, Septemba 15, 2019) wakati akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, akiwa katika siku ya pili za ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro.

Mbali na kuwasimamisha kazi watumishi hao, pia Waziri Mkuu ameagiza watumishi hao warejeshe fedha hizo ndani ya siku tatu kabla hajamaliza ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. Watumishi hao ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Fransis Ndulane anayedaiwa sh. milioni tano alizoingiziwa katika akaunti yake bila maelezo yeyote.

Amesema “Mkoa mzima wa Morogoro umekuwa na tatizo la upotevu wa mapato, fedha zinakusanywa zinapita mikononi mwa watu hazifiki benki, hii ni shida, hatutavumilia.”

Waziri Mkuu amesema kwa mujibu wa taarifa ya mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG) kipindi cha mwaka 2016 hadi juni 2019, Katika mji wa Ifakara makusanyo yalikuwa ni bilioni 2.7 ambapo fedha iliopelekwa bank ni shilingi bilioni 1.9 na kwamba kiasi cha shilingi milioni 727 hazijulikani zilipoenda.

Katibu wa CCM Moro Mhe. Shaka amwambia Mhe. Majaliwa hali hii haikubaliki ktk Mkoa wake. Lazima maamuzi magumu yafanyike.

Updates...
DC na DED Wilaya ya Malinyi wametumbuliwa. Ulanga watumishi waliohusika na ubadhirifu kusimamishwa kazi na kupelekwa mahakamani. Mhe. Majaliwa anaendelea kutema chechheeee... stay tuned Moro Vijijini Mbunge amechomoa betri.
Zamani DED anateuliwa kutoka afisa mipango au mkuu wa idara ina maana anakuwa na uzoefu wa kutosha.SIKU HIZI DED NI KADA WA CCM A MBAYE HAJAWAHI KUTUMIKIA SERIKALI KUTOKA MPIGA DEBE MPAKA DED
 
Zamani DED anateuliwa kutoka afisa mipango au mkuu wa idara ina maana anakuwa na uzoefu wa kutosha.SIKU HIZI DED NI KADA WA CCM A MBAYE HAJAWAHI KUTUMIKIA SERIKALI KUTOKA MPIGA DEBE MPAKA DED
Su 100% nakubaliana na ww
 
Shida RC, tumbua RC Steven Kabwe na RAS wake, mambo yatakuwa mazuri kabisa, alafu wamtafute mtendaji kama mm, Jay One uone mambo ya moto, mkoa wa Moro utaongoza kwa chakula Tanzania
SI mnasema upigaji umekwisha kwa makelele ya hilo lipenda sifa lenu? j...hu
 
Back
Top Bottom