Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema hali ya siasa na utekelezaji wa demokrasia nchini umeendelea kuimarika kutokana na maboresho ya mifumo na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali.
Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatano, Aprili 9, 2025, jijini Dodoma wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Amesema moja ya jitihada hizo ni pamoja na marekebisho ya sheria mbalimbali kwa lengo la kuimarisha utawala wa kidemokrasia nchini.
“Miongoni mwa sheria hizo ni Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na. 1 ya Mwaka 2024, Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 2 ya Mwaka 2024, pamoja na marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258,” amesema Majaliwa.
Ameongeza kuwa Serikali imeshakamilisha utungaji wa Kanuni za Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi. Aidha, Tume hiyo inaendelea na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwa kusimamia na kuratibu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura.