PreGE2025 Waziri mkuu Majaliwa: Hakuna Mwanasiasa maarufu kama Rais Samia ndani na nje ya CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
137,288
Reaction score
271,523
sijawahi kuona Waziri Mkuu Chawa

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema kwa msisitizo kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ndiye mwanasiasa maarufu zaidi nchini kwa sasa, ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akitoa hotuba ya kuhitimisha Mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano leo Alhamisi, Juni 26, 2025, Majaliwa amesema kauli hiyo inaakisi uhalisia wa uongozi wa Rais Samia uliojaa busara, subira, uthabiti na maono ya mbali, ambao umeiletea Tanzania heshima, mshikamano na maendeleo ya kweli.

“Mheshimiwa Spika, niruhusu nimnukuu Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, aliyewahi kusema: ‘Hapa Tanzania leo hakuna mwanasiasa maarufu kama Rais Samia iwe ndani ya Chama ama nje ya Chama Cha Mapinduzi.’ Maneno haya yana uzito mkubwa na yanabeba ukweli wa hali halisi,” alisema Majaliwa.

Akimzungumzia zaidi Rais Samia, Majaliwa ameeleza kuwa tangu kuchukua hatamu za uongozi baada ya kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mwaka 2021, Rais Samia ameonesha uwezo mkubwa wa kiuongozi uliogusa mioyo ya Watanzania wa makundi yote.

“Alisimama imara katika kipindi kigumu sana cha historia ya nchi yetu, akachukua uongozi kwa utulivu, kwa busara na kwa ujasiri usioyumba. Alithibitisha kuwa utulivu si udhaifu, bali ni nguvu ya ndani inayotoka kwa Mungu,” alisema Waziri Mkuu.

Majaliwa amesema uongozi wa Dkt. Samia umeiwezesha Tanzania kuendeleza miradi mikubwa ya maendeleo, kuimarisha demokrasia, diplomasia na mshikamano wa kitaifa sambamba na kujenga uchumi imara unaowajumuisha Watanzania wote.

Aidha, Majaliwa ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia kwa imani kubwa aliyoendelea kumuonyesha kwa kumteua kuwa Waziri Mkuu, akisema ni heshima isiyopimika kwake binafsi, familia yake, wana-Ruangwa na Taifa kwa ujumla.

Waziri Mkuu amehitimisha kwa kumtakia Rais Samia ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao, pamoja na mgombea mwenza wake Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi na Mgombea wa Urais Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Screenshot_2025-06-26-17-21-57-1.png

Au ndio analinda yale mabilioni anayopata kama 10% kwenye Stakabadhi Ghalani?
 
View attachment 3384711

Au ndio analinda yale mabilioni anayopata kama 10% kwenye Stakabadhi Ghalani?
Ufisadi,Ufisadi,Ufisadi tu na hakuna kingine.
 
Hapo lazima asifie kwenye speech yake
Shida mazingira yamewekwa kwamba mtu amsifie

Mfano Je ingekuwa
“pamoja na kukusifia kuna haya fuatayo ya kukuponda
…Mhe … Hatutaki…
Haufai…..”

Ingekuwaje?
 
Yupo wewe sitaki kutukana, ni TUNDU ANTIPAS MUGWAI LISSU, Hata hivyo gwajima ni maarufu kuliko huyo raia wa zanzibar
 
Anapalilia kuteuliwa tena ktk nafasi ya uwaziri mkuu
Kuna swali huwa najiuliza. Hivi hata Trump akienda chooni anachuchumaa/kaa kama sisi? Au kuna mtambo maalum ambaoo kazi yake ni kuhakikisha rais wa dunia hanyi? Kukojoa je, anashikilia kabisa nyeti halafu anakojoa?
Nimewaza hivi kwasababu jamaa ni tajiri halafu ni Rais wa dunia.
 
Back
Top Bottom