mshale21
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 2,049
- 4,904
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema yoyote atakaye waonea waandishi wa habari wakati wakitimiza majukumu yao watakiona, kwani serikali inawatambua na kuwathamini na isingependa kuona hata siku moja mwandishi anapata tatizo anapotimiza wajibu wake.
===
SERIKALI: HATUTAKUBALI KUONA MWANDISHI WA HABARI ANAONEWA
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali haitakubali kuona Mwandishi anapata uonevu popote kutokana na thamani ya mchango wanaotoa katika kuufahamisha Umma, Ameeleza hayo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Mkoani Morogoro.
Amesema, "Sio Sera ya Serikali kuonea Waandishi wa Habari. Serikali haitomvumilia mtu yeyote atakayemkwaza Mwandishi wa Habari akiwa katika kazi, na hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Vilevile, amesema hatua kadhaa zinaendelea ili kuyafungulia Magazeti ya Mawio, Mseto, Tanzania Daima na Mwanahalisi akifafanua yalifungiwa Kisheria na Sheria hizo hizo zitafuata taratibu.