Lusungo
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 29,532
- 42,696
Subscription kwa Mange mnalipia ila shule mnataka za bure serious?Elimu bure ilikwenda na JPM,
Subscription kwa Mange mnalipia ila shule mnataka za bure serious?Elimu bure ilikwenda na JPM,
Walipaswa kuwatambua ambao wangestahili hiyo elimi bure. Sehem ya iyo fedha wawalipie chakula.Katika kosa ililofanya serikali ni kuhangaika kuleta hii "Elimu bure" feki.
Gharama kubwa ufanisi sifuri, serikali wangejikita kujenga miundombinu bora yakufundishia na kujifunzia na kuboresha maslahi ya watumishi wa elimu.
Hali ni hovyo na hakuna la maana zaidi ya kutumia pesa nyingi kufadhili jambo lisilo la lazima.
Mimi nilisoma mwanzoni mwa 2000s kipindi cha Benjamin Mkapa. Tulikuwa tunalipa ada toka shule ya msingi na michango yote. Mambo yalikuwa vivyo hivyo mpaka Sekondari.
Elimu bure ni kudumaza na kuendekeza umasikini nchini.
Ifutwe, ililetwa kisiasa japo imesaidia kwa mbali sana, ila gharama zake ni kubwa mno.
Serikali itumie hiyo pesa kuajiri walimu wa kutosha na kuanzisha karakana za ufundi kila kijiji na wanafunzi wakifika darasa la 5 hadi la 7 wajifunze ufundi.
Ilo najua, rigidity yenu haijaanza Leo, Wala Jana enzi za Magu. Ni rigid Toka zamanSisi watu wa Chato kwa magu utwambii kitu
[emoji38][emoji38][emoji38]Dodoma. Serikali imesema michango yenye kupeleka maendeleo mashuleni haijazuiwa, isipokuwa inachangishwa chini ya wakuu wa wilaya au mtu atakayeteuliwa kwa niaba.
Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Juni Mosi, 2023 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kusini (CCM), Ally Kasinge.
Katika swali lake Mbunge huyo amehoji licha ya Sera ya elimu bure lakini kumekuwa na michango mingi akauliza kama serikali haioni haja ya kuwapunguzia wazazi mzigo wa michango hiyo.
Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kutekeleza sera ya elimu bila malipo ambapo kila mwaka inapeleka fedha kwa walimu kwa ajili ya kulipia gharama ambazo zingeweza kuwafanya wazazi kutolipa michango.
“Natambua kuwa siyo maeneo yote yanapata fedha hasa chakula na eneo la ulinzi, kwa sasa tunashughulika na maboresho ya sera na kuona namna gani tutafanya katika jambo hilo kwani bado tunaendelea kuchakata ili tutoe huduma nzuri ya chakula,” amesema Majaliwa.
Ameomba wananchi kuendelea kuchangia michango ambayo itakuwa na tija ya kimaendeleo badala ya ile ya kusema walimu kusema njoo kesho na Sh200 ambayo ni kero.
Ametolea mfano wa michango ya maendeleo ni mfano wa ujenzi wa choo cha shule kama kimebomoka ambayo amesema haitazuiliwa kwani haliondoi maboresho kwa wazazi kusimamia elimu ya watoto wao
NB: Wazazi wahusike katika kuchangia maendeleo ya watoto wao mashuleni
Sio kweli, kwamba unashindwa kuhoji muenendo wa mwanao kisa elimu ni bure... Hapana uo ni uongo bwana kaka pembeSerikali irudishe ada shuleni. Hizi nyimbo za elimu Bure zinatufanya hata tushindwe kuhoji matokeo na mienendo ya watoto wetu huko mashuleni.
Ada irudishwe mashuleni
Mkuu,elimu yoyote duniani ni ghali, iweje ya kwetu ni cheap Sana?.Sio kweli, kwamba unashindwa kuhoji muenendo wa mwanao kisa elimu ni bure... Hapana uo ni uongo bwana kaka pembe
Sijakataa, ninachokataa hapo ni madai Yako kusema elimu bure inakufanya ushindwe kuhoji maendeleo ya mwanaoMkuu,elimu yoyote duniani ni ghali, iweje ya kwetu ni cheap Sana?.