Waziri Mkuu Kassim: Michango Mashuleni Ruksa

Waziri Mkuu Kassim: Michango Mashuleni Ruksa

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
73,321
Reaction score
103,591
Dodoma. Serikali imesema michango yenye kupeleka maendeleo mashuleni haijazuiwa, isipokuwa inachangishwa chini ya wakuu wa wilaya au mtu atakayeteuliwa kwa niaba.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Juni Mosi, 2023 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kusini (CCM), Ally Kasinge.

Katika swali lake Mbunge huyo amehoji licha ya Sera ya elimu bure lakini kumekuwa na michango mingi akauliza kama serikali haioni haja ya kuwapunguzia wazazi mzigo wa michango hiyo.

Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kutekeleza sera ya elimu bila malipo ambapo kila mwaka inapeleka fedha kwa walimu kwa ajili ya kulipia gharama ambazo zingeweza kuwafanya wazazi kutolipa michango.

“Natambua kuwa siyo maeneo yote yanapata fedha hasa chakula na eneo la ulinzi, kwa sasa tunashughulika na maboresho ya sera na kuona namna gani tutafanya katika jambo hilo kwani bado tunaendelea kuchakata ili tutoe huduma nzuri ya chakula,” amesema Majaliwa.

Ameomba wananchi kuendelea kuchangia michango ambayo itakuwa na tija ya kimaendeleo badala ya ile ya kusema walimu kusema njoo kesho na Sh200 ambayo ni kero.

Ametolea mfano wa michango ya maendeleo ni mfano wa ujenzi wa choo cha shule kama kimebomoka ambayo amesema haitazuiliwa kwani haliondoi maboresho kwa wazazi kusimamia elimu ya watoto wao

NB: Wazazi wahusike katika kuchangia maendeleo ya watoto wao mashuleni
 
Dodoma. Serikali imesema michango yenye kupeleka maendeleo mashuleni haijazuiwa, isipokuwa inachangishwa chini ya wakuu wa wilaya au mtu atakayeteuliwa kwa niaba.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Juni Mosi, 2023 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kusini (CCM), Ally Kasinge.
Elimu bure ilikwenda na JPM,
Nani alikuambia kuna elimu bure

Ova
 
ee35881f-ef8e-4981-9449-6746d73f366e.jpg
 
Katika kosa ililofanya serikali ni kuhangaika kuleta hii "Elimu bure" feki.

Gharama kubwa ufanisi sifuri, serikali wangejikita kujenga miundombinu bora yakufundishia na kujifunzia na kuboresha maslahi ya watumishi wa elimu.

Hali ni hovyo na hakuna la maana zaidi ya kutumia pesa nyingi kufadhili jambo lisilo la lazima.

Mimi nilisoma mwanzoni mwa 2000s kipindi cha Benjamin Mkapa. Tulikuwa tunalipa ada toka shule ya msingi na michango yote. Mambo yalikuwa vivyo hivyo mpaka Sekondari.

Elimu bure ni kudumaza na kuendekeza umasikini nchini.

Ifutwe, ililetwa kisiasa japo imesaidia kwa mbali sana, ila gharama zake ni kubwa mno.

Serikali itumie hiyo pesa kuajiri walimu wa kutosha na kuanzisha karakana za ufundi kila kijiji na wanafunzi wakifika darasa la 5 hadi la 7 wajifunze ufundi.
 
Hata wakati wa MAGU tulikua tunatoa hela Kwa ajili ya chakula, tunalipa hela Kwa ajili ya walimu wa part-time.

Kama vipi mfuate JPM uko aliko akakupe vya bure maana naona mzimu wa JPM unakusumbua
Sisi watu wa Chato kwa magu utwambii kitu
 
Kwamba uzae afu usomeshewe bure?
Kuna wakati binadamu huwaza ujinga!
Hivi mtoto unayemzaa wewe ni mtoto wako?
Mungu alituumbia upendo vifuani mwetu ili tuvipende vizazi vyetu, lakini kiuhalisia mtoto siyo wako ni wa Mungu na Serikali.
Kwa kulitambua hilo, Serikali inasomesha watoto mashuleni na vyuoni na inawaajiri.
 
Wewe ni mpumbavu
 
Back
Top Bottom