Waziri Mkuu atoa masaa 48 Wafanyakazi 89 wafukuzwe kazi halmashauri ya manispaa Temeke

Ujinga huu, elimu huna basi hata certificate ya driving nayo ni shida?

Hawa wengi wao ndio wale wenye matumbo makubwa wakiwaleta mabosi zao kwenye tafrija yanapenda kufakamia msosi utadhani ndio mwisho wa maisha, majitu ya namna hii hayawezi kuwa na akili.
Acha tharau ndugu yangu
 
Huu mtindo wa kuuliza sifa wakati malengo yanatimizwa na matokeo yanaonekana ni mazuri hauna tija.Kama Paka anakamata Panya ya nini kutilia shaka rangi yake?.Kama hawana hizo sifa wapatiwe kuliko kuwaacha kwani wana uzoefu.
 
Huu mtindo wa kuuliza sifa wakati malengo yanatimizwa na matokeo yanaonekana ni mazuri hauna tija.Kama Paka anakamata Panya ya nini kutilia shaka rangi yake?.Kama hawana hizo sifa wapatiwe kuliko kuwaacha kwani wana uzoefu.
Ni utaratibu wa serikali, Private hatuangalii vyeti bali utendaji kazi. Serikali iliwapa muda watumishi wake walioishia darasa la saba wakasome QT maana hakuna ajira ya dara la serikalini kwa sasa.
 
Acha tharau ndugu yangu
Dharau iko wapi? Wewe huoni wafuga matumbo na kupenda kula?

Ukiyaona mtaani yanavyjojsikia kwenye hayo magari sasa ya STK....

Kuna Brother wangu ni boss fulani huko serikalini ili kuwafundisha adabu hawa ndio aliyetowa wazo washonewe kaunda suti hawa madereva ili kwenye gari Boss ajurikane.

Maana kwa matumbo yao makubwa ukiwaacha wavae tai Boss unaweza onekana umepewa lift tu.
 
Nahisi kulikuwa na teni paseti 89 hawajaajiriwa, kwa maana hiyo unawalipa kwa kutumia bahasha sio.
 
Hao madereva no wazembe sana,Nina mashaka si hajabu wanajua kuendesha magari ya aina zote lakini hawajui kusoma na kuandika.
 
Hii fukuza fukuza itawapa Watu Gonjwa la moyo, kwa utawala huu Watumishi wa Serikali wanaona Moto, mpaka huruma, maana hakuna ajuaye atatumbuliwa lini?
 
Sasa watatangazaje Ajira wakati ajira zimesimamishwa?

Pili kama hawa watu hawana sifa lakini wameonyesha Utendaji mzuri kwa nini serikali isiwape Ultimatum ya kuzisaka hizo sifa ndani ya muda fulani?

Mheshimiwa Waziri Mkuu, haya ni maisha ya watu, hawa watu wana familia wana watoto. Tuwape muda wazisake hizo sifa!
Wewe bwana usiwe kama hauko Tanzania au wewe siyo Mtanzania bwana. Nini kigeni ambacho hukijui kwa nchi yetu? Ukiona hivyo hao ni ndugu na jamaa wa wakubwa wa halmashuri hiyo. Kwa hiyo usitegemee kama watapimwa utendaji wao kwani waliowaweka hapo wamewakeka kwa maksudi maalum (mojawapo likiwa saidia ndugu). Kuna taasisi nyingi tu za serikali zinazofanya madudu kama hayo. Nenda kwenye vyuo ndo utashangaa. Kuna chuo kimoja cha serikali cashier hana hata mkataba wa kazi, na kwa sababu ni mtoto wa wakubwa basi yupo anadunda.
 
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa saa 48 kwa Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke kuwa amewaondoa kazini watumishi 89 wanaofanya kazi katika halmashauri hiyo kwa Mikataba.

Amewatahadharisha pia watendaji wa halmashauri zote nchini kutotumia fedha za miradi zinazopelekwa na serikali kinyume na malengo kutokana na kuimarishwa kwa mfumo wa ufuatiliaji wa matumizi yake na thamani ya miradi itakayojengwa.

Aliyasema hayo alipozungumza na watumishi na watendaji wa manispaa hiyo, huku akiweka bayana kwamba halmashauri hiyo inaongoza kwa kuwa na watumishi wa Mikataba, jambo ambalo ni kinyume cha taratibu za utumishi.

Akiendelea na mkutano huo, ghafla Waziri Mkuu alimsimamisha Kaimu Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Zaituni Hassan na kumuuliza idadi ya watumishi wa Mikataba katika halmashauri hiyo ambapo ofisa huyo alijibu kuwepo kwa watumishi 89.

Jibu hilo lilimfanya Waziri Mkuu kuhoji sababu ya kuwepo kwa idadi kubwa hiyo na kujibiwa kuwa hatua hiyo ilitokana na wengi wao kukosa sifa za kuajiriwa huku akisema wengi wao ni madereva.

Zaituni aliendelea kumwambia Waziri Mkuu kwamba mwaka jana Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ilitangaza nafasi za kazi na kuwataka watumishi hao kuomba lakini walishindwa kufikia vigezo vilivyowekwa na kusababisha halmashauri kuendelea kuwatumia bila kuwaajiri.

Pamoja na maelezo hayo, Waziri Mkuu alieleza kushangazwa na hatua ya kutokuwepo kwa madereva waliohitimu Kidato cha Nne ambao wangeweza kuajiriwa, hata hivyo Ofisa Utumishi huyo alimwambia waliopo wana elimu ya Kidato cha Nne lakini hawana vyeti vya mafunzo ya udereva kutoka Chuo cha Elimu na Mafunzo Stadi (VETA).

Majaliwa alieleza kuwa wanaotakiwa kuajiriwa kwa Mikataba ni walimu wa Masomo ya Sayansi na watendaji wa mitaa hivyo kama madereva hao hawana sifa ni vyema wakaondolewa kwa vile wanaziba nafasi za watu wenye sifa za kuajiriwa.

Alisema kutokuajiriwa ni moja ya sababu za kuwepo watumishi hewa hivyo alisema hadi kufikia Julai 30, mwaka huu, Ofisa Utumishi huyo awe amejiridhisha kuhusiana na sifa za watumishi hao ili wasio na sifa waondolewe na wenye sifa waajiriwe huku akisema zoezi hilo lifanyike katika idara zote.

Alimtaka kuanza taratibu za kumuomba Katibu Mkuu wa Utumishi kibali cha kuwaajiri watumishi hao na kusema ametoa nafasi hiyo kwa kuwa watumishi wengi katika halmashauri hawana mwelekeo mzuri kutokana na kutoajiriwa, hivyo wasio na sifa waondoke ili watafutwe wenye nazo.

Akizungumzia fedha zinazopelekwa katika halmashauri, Waziri Mkuu alisema kila fedha inayoingia katika halmashauri itakuwa na maelekezo ya matumizi na Mkurugenzi atalazimika kutoa nakala ya maelezo hayo na kumpatia Mkuu wa Wilaya ili ajue matumizi ya kila shilingi na thamani ya miradi.

Alisema baada ya kumaliza uteuzi wa viongozi mbalimbali, sasa Serikali inaanza kupeleka fedha za maendeleo katika halmashauri zote ili utekelezaji wa shughuli za maendeleo uendelee.
swali kwa Waziri kwanini walimu wa science waajiriwe kwa mikataba na halmashauri wakati mtaani huku wapo wengi waliomaliza vyuo mwaka Jana na mwaka huu na serikali mpaka muda huu imeshindwa kuwaajiri..hizo ela wanazolipwa na halmashauri ikiwaajiri kwa mikataba inatoka wapi??
 
Ata wakifukuzwa ni halali coz kusomea udereva au malizi ata mweziii, wao walikua wanajali ela sana wakasahau vyeti pia ni muhimu kwa hiki kipindi cha kutumbuliwa na mzee...
 
Hivi hao madereva wanashindwaje kusoma kozi za mwezi mmoja mmoja za umahiri pale VETA na NIT wanapokuwa likizo? Bora wafukuzwe kazi tu.
Kwa kwweli hilo ndio la kushangaza kwa kweli. Katika maisha ni vema kufuata taratibu hizi short cut sio nzuri hata kidogo matokeo yake ndio haya halafu wataanza kulalamika wakati kosa ni la kwao!
 
Sasa watatangazaje Ajira wakati ajira zimesimamishwa?

Pili kama hawa watu hawana sifa lakini wameonyesha Utendaji mzuri kwa nini serikali isiwape Ultimatum ya kuzisaka hizo sifa ndani ya muda fulani?

Mheshimiwa Waziri Mkuu, haya ni maisha ya watu, hawa watu wana familia wana watoto. Tuwape muda wazisake hizo sifa!
sheria za utumishi wa umma hazitambui familia wala vimada. Kumbuka likitokea tatizo la kiufundi lazima tuhoji taaluma yake kwanza.
 
Back
Top Bottom