Waziri Mkuu amuagiza Simbachawene ahakikishe Halmashauri zinajenga Maabara

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
2-26.jpg

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa (mwenye tai nyekundu) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa zoezi la usambazaji wa vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalum mapema hii leo katika viwanja vya hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Majaliwa amemwagiza Waziri wa Nchi, Ofisi Rais (TAMISEMI), Simbachawene ahakikishe Halmashauri zinakamilisha ujenzi wa maabara.

Usambazaji wa vifaa masomo ya Sayansi utafanyika kwenye kanda 11 za kielimu na utahusisha shule za wananchi 1,625 na shule kongwe 71

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mtu yeyote atakayebainika amemkatisha mwanafunzi wa kike masomo kwa kumpa mimba au kumfanyia vitendo vya ukatili vitakavyopelekea kukatisha masomo yake ni lazima afungwe miaka 30 jela.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Lugalo jeshini Jijini Dar es Salaam wakati akizindua na kukabidhi vifaa vya maabara na vifaa vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu vyenye jumla ya thamani ya Shilingi Bilioni 16.9 kwa ajili ya shule 1696 kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha uboreshaji wa masomo ya sayansi.

Vilevile Majaliwa ameiagiza TAMISEMI kuhakikisha wanakamilisha maabara za shule zote nchini 4587 ambazo bado hazijakamilika ili vifaa hivyo vianze kusaidia wanafunzi kwa haraka na kufikia malengo ya nchi ya kuwa ya uchumi wa kati.

Pamoja na hayo, Majaliwa amesema watendaji watakaoenda kinyume na maadili ya kazi zao ni lazima mkono wa sheria uchukue nafasi yake.
 
Halmashauri zitajengaje barabara bila ya kuwepo pesa!? Huyu naye aache kuropoka ropoka. Apambane kwanza na bajeti hewa ya Serikali.

View attachment 520329

du!!!! kweli mnaendelea kupagawa....naanza kuamini kuwa jamaa pengine anawanyosha kweli, maana si kwa hali hii ya kurukia habari bila hata kuielewa!!
 
Sasa badala ya kuangalia chanzo cha mimba hizi na kukishughulikia, tunataka kufunga watu baada ya mimba kutokea.

Hatufuati hekima za "kinga ni bora kuliko tiba".

Matokeo yake watu watatia mimba wanafunzi,halafu hata kama mtu angetakakukubali kumuoa mwanafunzi na kumtunza mtoto, atafungwa jela miaka 30 na huyo mtoto atakosa baba na mwanafunzi atakosa mume.

Na huko jela kutajaa watu wasiotumikia uchumi wa nchi ambao wanalishwa kwa hela ya walipa kodi.

Kwa sababu tu viongozi wanatafuta majibu mepesi kwa maswali magumu.
 
Halmashauri zitajengaje maabara bila ya kuwepo pesa!? Huyu naye aache kuropoka ropoka. Apambane kwanza na bajeti hewa ya Serikali.
Zitajengwa tu taratibu,kila Kitu ni dhamira kwanza mambo mengine baadaye.

Kama alivyokuwa shule za kata.Madawati n.k
 
Miaka mingine 56 huku chama chenu cha wahuni na mafisadi kikiendeleza ufisadi wa kutisha nchini dhidi ya Watanzania eh!

Back
Top Bottom