Waziri Mkuu Ampa Zawadi Ya Laptop Ya Milionin 1.9 Mwanafunzi Wa Shule Ya Kata

TataMadiba

JF-Expert Member
Feb 7, 2014
9,866
5,742
8.jpg

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema shule za sekondari za kata zina fursa ya kufanya vizuri kama zilivyo shule nyingine licha ya kuwa watu wengi wamekuwa wakizidharau.
Ametoa kauli hiyo jana mchana (Jumatatu, Machi 7, 2016) wakati akikabidhi zawadi ya kompyuta mpakato (laptop) kwa mwanafunzi aliyeshinda shindano la kuandika insha katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC ). Kompyuta hiyo ina thamani ya sh. 1,992,000/-.
Mwanafunzi huyo, Jabir Mandando (20), amehitimu kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Mbekenyera iliyoko wilayani Ruangwa mkoani Lindi. Amepata ufaulu wa daraja la pili na sasa anasubiri matokeo ya kujiunga na kidato cha tano. Lakini aliandika insha hiyo mwaka jana wakati akiwa kidato cha nne.

“Huyu ni mtoto wa kijijini tu. Anatoka kijiji cha Namilema wilaya ya Ruangwa mkoa wa Lindi. Shule ya Mbekenyera aliyosoma ni shule ya kata. Ameweza kushinda tuzo na kushika nafasi ya tatu katika shindano lililoshirikisha shule nyingi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.”

“Jabir ameweza kuchomoza kitaifa kwa kushiriki shindano la kimataifa. Nimeamua kumpa zawadi ya laptop pamoja na begi lake ili aweze kujisomea zaidi na kupata elimu ya masuala mbalimbali kwa kutumia kompyuta hii. Pia nataka iwe ni chachu kwa vijana wengine kushiriki mashindano kama haya,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu pia alikabidhi Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Shanael Nchimbi fedha taslimu sh. 500,000/- zikiwa ni zawadi kwa ajili ya shule hiyo. mwalimu Nchimbi alimsindikiza mwanafunzi huyo Arusha kupokea zawadi hizo kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliomalizika Arusha wiki iliyopita.

Kwa upande wake, kijana Jabir alisema anashukuru sana kwa zawadi aliyopewa na kuahidi kuwa atajitahidi kusoma kwa bidii masomo ya kidato cha tano na sita ili aweze kutimiza ndoto yake ya kuwa daktari.
Alipoulizwa alipataje taarifa ya uwepo wa shindano hilo, Jabir alisema:“Walimu walipata taarifa wakazileta darasani na kutuambia tushiriki kuandika. Walizikusanya na kuchagua tatu bora, ndipo yangu ikashinda.”

Amesema insha aliyoiandika ilihusu: “The importance of political stability in the East African Integration.”
Alimwonyesha Waziri Mkuu cheti na dola za Marekani 200 ambavyo alipewa zawadi kutokana na ushindi huo. Shule ya Mbekenyera ambayo alikuwa akisoma, pia ilizawadiwa laptop na printer kutokana na ushindi wa kijana Jabir.

Mshindi wa kwanza katika shindano hilo ametoka shule ya Sekondari Mzumbe, mshindi wa pili alitoka Kenya na wa tatu alitoka shule ya Mbekenyera.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,2 MTAA WA MAGOGONI,

S. L. P. 3021, 11410 DAR ES SALAAM.

JUMATATU, MACHI 7, 2016.
 
Ngoja tusubiri labda huyo atakuja kubahatisha hata kubahatisha ukurugenzi wa PPF
 
Ni sawa kumtunuku mwanafunzi aliye na ufaulu mzuri. Ila Unafiki wa viongozi wetu upo hapa:-

-Ni kweli Mh. hajui kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya shule za kata na za private(especcially seminaries) mpaka aseme wote wana fursa sawa ya kufaulu?

-Watoto zao wanasoma kwenye hizi shule za kata?

-Amejiuliza huyo mtoto angesoma St. Francis au Feza boys angekuwa na Div 1 ya point ngapi?

We need to think out of box
 
Akili ndogo kweli,hamjamwelewa mtoa comment ya udini,anamaana kwamba kuna wapuuzi fulani hua wanasema eti kuna upendeleo kwa wakristo na kubinya fursa kwa waislam huko wizarani kama ile kesi ya prof.Ndalichako pale NECTA,so ku excel kwa huyu kijana wa kiislam kumewaumbua
wewe pekee ndo umuelewe njiwa , wengine tusimuelewe? wale wale. nawe una utindio wa ubongo. mimi ni mkristo na siwezi kuungana na wajinga kama ww na njiwa.
 
Iyo nzuri kwa kuongeza juhudi kwa wanafunzi...ila laptop bongo bei zipo juu sana..maana wenye bei ni Apple hii sawa hawa wengine sijui Toshiba,dell,Hp nao wapo juu sana na kodi hakuna inakuaje hapo..
 
Akili ndogo kweli,hamjamwelewa mtoa comment ya udini,anamaana kwamba kuna wapuuzi fulani hua wanasema eti kuna upendeleo kwa wakristo na kubinya fursa kwa waislam huko wizarani kama ile kesi ya prof.Ndalichako pale NECTA,so ku excel kwa huyu kijana wa kiislam kumewaumbua
Jamaa anaakili sana!
 
Ni sawa kumtunuku mwanafunzi aliye na ufaulu mzuri. Ila Unafiki wa viongozi wetu upo hapa:-

-Ni kweli Mh. hajui kuwa kuna utofauti mkubwa kati ya shule za kata na za private(especcially seminaries) mpaka aseme wote waba fursa sawaya kufaulu?

-Watoto zao wanasoma kwenye hizi shule za kata?

-Amejiuliza huyo mtoto angesoma St. Francis au Feza boys angekuwa na Div 1 ya point ngapi?

We need to think out of box
ndiyo maana amesema , shule za kata nazo zinaweza kufanya vizuri. tuliza kichwa, soma vizuri alichokisema PM.
 
mnadhani hii ni NECTA ya upendeleo wa kina JOHN
kiuhalisia WAISLAM wengi UBONGO umechangamka na wanavipaji vilivuoyutukuka sema kutokana na FIGISUFIGISU za kina MICHAEL waliojazana kule ndo shidaaa
Huyo ni muislam mwenzako, anachofanya ni uchokozi tu na ni njia ya kumtambua na kumtambulisha Jabir kwa dini yake. Hongera sana Jabir Mungu akufikishe mbali zaidi. Amina
 
ndiyo maana amesema , shule za kata nazo zinaweza kufanya vizuri. tuliza kichwa, soma vizuri alichokisema PM.
Nani amebisha hilo? Au unakurupuka bila kuelewa nilichoandika, NI KWELI KUWA WANAFUNZI WA KATA WANA FURSA SAWA ZA UFAULU NA AKINA ST.FRANCIS NA FEZA'S unajua tofauti ya mazingira yao ya kusoma?

Huyo mtoto na juhudi yake hiyo ya kupata II je angekuwa seminary nzuri angepata daraja gani? Tumia akili yako vizuri kufikiri.
 
Seminary hakuna wanaopata division III, IV na 0?
 
Nani amebisha hilo? Au unakurupuka bila kuelewa nilichoandika, NI KWELI KUWA WANAFUNZI WA KATA WANA FURSA SAWA ZA UFAULU NA AKINA ST.FRANCIS NA FEZA'S unajua tofauti ya mazingira yao ya kusoma?

Huyo mtoto na juhudi yake hiyo ya kupata II je angekuwa seminary nzuri angepata daraja gani? Tumia akili yako vizuri kufikiri.
hizo juhudi alifanyia akiwa grocery au shule ya kata? Nyumbu type.
 
Huyo ni muislam mwenzako, anachofanya ni uchokozi tu na ni njia ya kumtambua na kumtambulisha Jabir kwa dini yake. Hongera sana Jabir Mungu akufikishe mbali zaidi. Amina

mbona wengine mnawatambuwa na kuwatambulisha kwa majina yao na kuanza kuwaita wadini ..? iwe jabiri awe mgalatia..? au haiwezekani muislam kupata achievement ya aina hii...

comment yangu iligonga penyewe mme report mods kaiondoa.. i wish angefanya same kwenye zile thread nyingine lakini zipo hewani mpaka sasa ...
 
Nani amebisha hilo? Au unakurupuka bila kuelewa nilichoandika, NI KWELI KUWA WANAFUNZI WA KATA WANA FURSA SAWA ZA UFAULU NA AKINA ST.FRANCIS NA FEZA'S unajua tofauti ya mazingira yao ya kusoma?

Huyo mtoto na juhudi yake hiyo ya kupata II je angekuwa seminary nzuri angepata daraja gani? Tumia akili yako vizuri kufikiri.
wewe mwehu, nasubiri unijibu, umesema ni juhudi binafsi za jabir angekuwa seminary angefaulu zaidi. seminary hakuna wanaopata daraja la III, IV au 0?
 
Back
Top Bottom