Waziri Mkuu amemsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji Makao Makuu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Waziri Mkuu amemsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji Makao Makuu, Grace Hokororo kwa kuwapa vibali vya uraia Wasomali bila kufuata sheria.

=======



======
Habari kamili:

RAIS Magufuli amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsimamisha kazi Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Bi. Grace Hokororo. Waziri Mkuu alewaambia waandishi wa habari kuwa Bi. Hokororo amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuingiza nchini raia 50 wa Somalia na kuwapa vibali vya kuishi kinyume cha taratibu.

Kauli hiyo imetolewa leo (Ijumaa, Julai 28, 2017), na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kikao na Makamishna wa uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba kuunda tume ya uchunguzi kuhusu utoaji wa vibali uraia nchini.

Amesema haiwezekani raia wa kigeni wanaingizwa nchini na wanapewa vibali vya kuishi bila ya kufanyiwa uchunguzi wa kina. “Idara ya Uhamiaji tunaitegemea kusimamia mipaka yetu na kuziba mianya ya watu kuingia bila ya kufuata taratibu lakini kwa mapenzi yake Ofisa huyu ameruhusu Wasomali kuingia bila kufuata taratibu.”

Waziri Mkuu amesema ni lazima uchunguzi ufanyike ili kubaini “Tulidhani ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa Wasomali hao ambao hawakuwepo nchini wameingia na kupewa vibali moja kwa moja kwa mapenzi yake tu sasa hii ni dosari hatuwezi kuivumilia.”

Amesema Serikali inaitegemea Idara ya Uhamiaji kwa kuzuia mianya ya uingiaji raia mbalimbali kutoka nje ya nchi bila ya kufuata taratibu, hivyo Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ameagiza Ofisa huyo asimamishwe kazi na uchunguzi ufanyike ili kubaini malengo yake.

"Hawa Wasomali aliowapa vibali vya kuishi wala hawakuwa wanaishi nchini wameingia tu na kupewa vibali, hivyo Mheshimiwa Rais Magufuli ameagiza ofisa huyo akae pembeni na achunguzwe ni kujua ni kitu gani kilimsukuma kutoa vibali kwa raia hao."

Pia Waziri Mkuu ameiagiza idara ya Uhamiaji wadhibiti kitengo cha utoaji hati za kusafiria za Kibalozi na kwa wanaomaliza muda wasipewe tena. "Lazima hati hizo zikaguliwe katika mipaka yote na maeneo yote ya usafiri ili kujua kama huyo anayeitumia bado anahadhi hiyo na msiporidhika ichukuweni kwani kuna watu wanazitumia vibaya."

Hata hivyo Waziri Mkuu ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike kwa watu wote walioomba hati za kusafiria pamoja na vibali vya makazi kama wanakidhi matakwa ya kisheria kabla ya kuwakabidhi.
 
Duuh!

Siku hizi Ukitoka kazini Jioni beba kabisa kila kilicho chako maana kesho huenda usirudi kwny Ile ofisi

Unaacha Packet za Kondom zilizotumika ukihisi utazibeba kesho asbh ukifika tu, unashangaa Greyson Msigwa anatumia kwny Wasap usiku wa Manane umetenguliwa!
Kama ni msafi huna haja ya kuwa na wasiwasi
 
Back
Top Bottom