Observer
JF HQ
- Oct 18, 2006
- 189
- 299
Chama cha Conservative kinachotawala nchini Uingereza leo kimewapitisha Waziri wa mambo ya ndani Bi Theresa May na Bi Andrea Leadsom kwenda kupigiwa kura na wanachama wao katika uchaguzi wa kumpata kiongozi wa chama hicho ambaye atakuja kuwa Waziri Mkuu.
Hatua hio inafuatia baada ya kiongozi wa chama hicho na Waziri Mkuu wa Uingereza kutangaza kung'atuka nafasi hiyo baada ya wananchi wa nchi hiyo kuamua Uingereza ijitoe katika muungano wa Ulaya.
Katika kura zilizopigwa leo na wabunge wa chama hicho kuwachagua watu wawili watakaokwenda kupigiwa kura na wanachama wao, Theresa May alipata kura 199 Andrea Leadsom alipata kura 84 na Michael Gove alipata kura 46 na kutupwa nje