Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,340
- 10,866
Katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu wa JMT, kuna mbunge mmoja (mwanamke) aliuliza swali juu ya mpango wa serikali kupanua matumizi ya lugha ya kiswahili duniani. Katika majibu ya WM, alielezea 'mikakati' mbalimbali iliyochukuliwa na serikali. Jambo moja lililonivutia ni WM kusema lugha ya kiswahili ni moja ya lugha zinazozungumzwa zaidi duniani. Alienda mbele kwa kutaja kabisa kwamba ni kati ya lugha ya 6 au 8 duniani. Alirudia kusema hivyo mara mbili, licha ya kukiri hana taarifa za uhakika! Sitaki kuzungumzia WM kutoa conclusive responses bila ya kuwa na uhakika. Ninachokisema hapa ni uongo (intentionally or not) wa WM mbele ya Bunge.
Hapa nimejaribu ku-google na kufahamu lugha kumi zinazozungumzwa zaidi duniani. Kuna vyanzo mbalimbali, lakini hakuna hata kimoja kinachoonyesha lugha ya kiswahili kuwa kati ya lugha kumi zinazozungumzwa zaidi duniani.
1. Top 10 Most Spoken Languages In The World - Listverse
2. Most Popular Languages in the World by Number of Speakers
3. Most spoken Languages of the World - Nations Online Project
4. Top Ten Most Spoken Languages In The World In 2014
5. The 10 Most Common Languages
6. TOP 10 Most Spoken Languages in the World 2016 Update
Tujadili kwa mtazamo wa kutaka viongozi wetu waache mazoea ya kuzungumza masuala wasiyo na uhakika nayo.