Waziri Mkullo afanya kufuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkullo afanya kufuru

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 29, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,977
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Wakati makele yamepigiwa juu ya matumizi yenye harufu ya ubadhirifu serikalini kama vile ununuzi wa mashangingi ghali sana huko magari yaliyopo bado ni mapya....................gazeti la Tanzania Daima linaripoti ya kuwa Waziri wa fedha Mkullo amefanya kufuru kwa kuruhusu matumizi makubwa na yasiyo ya lazima ya fedha za serikali.............................

  Huu sasa ni ubadhirifu wa mali ya umma..................

  Waziri Mkulo afanya kufuru
  • Akodi ndege kwenda Dodoma, aagiza shangingi toka Dar

  na Bakari Kimwanga

  [​IMG] WAKATI serikali ikisisitiza kutaka kupunguza gharama za matumizi kwa kuacha kuendelea kununua magari ya kifahari 'mashangingi', baadhi ya matumizi ya mawaziri yanatisha na kuwa mzigo kwa serikali. Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano kwa muda mrefu sasa, umebaini kuwa wapo mawaziri na watendaji wengine wa serikali, wanaofanya ziara mikoani na kusafiri kwa ndege za kukodi, lakini hulazimika kuyaagiza mashangingi yao aina ya G8 kutoka Dar es Salaam hadi katika mikoa wanayokwenda kufanya ziara hata kama yatatumika kwa siku moja.
  Mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Uchumi na Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye wiki iliyopita alikodi ndege kwa fedha za serikali kwenda kuhudhuria mahafari ya Chuo cha Mipango mjini Dodoma, lakini bado aliliagiza gari lake la uwaziri limfuate kutoka jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kulitumia katika mji huo wakati Wizara ya Fedha na Uchumi, ina ofisi na magari mjini Dodoma.
  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano, ulibaini kuwa Desemba 17, mwaka huu, Waziri Mkulo mwenye dhamana ya fedha nchini, alikodi ndege ya Shirika la Tanzania Air, yenye namba za usajili 5HTZC na kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma, majira ya saa nane mchana.
  Wakati Waziri Mkulo akipasua anga la Dodoma kwa ndege ya kukodi, siku hiyo hiyo, dereva wake alilazimika kujaza mafuta shangingi la waziri huyo na kuweka kibindoni posho yake kumfuata bosi wake mjini Dodoma.
  Kwa mujibu wa habari hizo, ndege hiyo ilikodishwa kwa dola za Kimarekani 5,000, sawa na sh milioni 7.5.
  'Mimi niko hazina, hivi sasa serikali haina fedha, kuna madeni mengi, kuna walimu zaidi ya 500,000 waliomaliza vyuo vya elimu ya juu tangu Mei mwaka huu wanasubiri ajira kutokana na ukosefu wa fedha, lakini hazina inafanya matumizi mabaya kila siku. Huku ni kulifilisi taifa bila sababu,'� alisema mtoa habari wetu ambaye jina lake limehifadhiwa.
  Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kuhusina na kashfa hiyo, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, John Haule, alikiri kuwa Desemba 17, mwaka huu, wizara yake ilikodi ndege kwa ajili ya kumuwahisha Waziri Mkulo kuwahi mahafali ya Chuo cha Mipango ambapo alikuwa mgeni rasmi.
  Haule ambaye alikuwa na wakati mgumu kutoa ufafanuzi huo, alisema walilazimika kufanya hivyo kutokana na umuhimu wa kazi alizokuwa nazo Waziri Mkulo siku hiyo kabla ya kuondoka kwenda Dodoma na kusisitiza kuwa ukodishwaji wa ndege ni jambo la kawaida kwa watendaji wa wizara hiyo.
  'Hili ni suala la kawaida kabisa katika utendaji wa wizara yetu; siku hiyo ilikuwa lazima waziri aende Dodoma katika mahafali na kuzindua bodi ya chuo cha mipango, sasa kwa hili tulishirikiana na chuo chenyewe kulipia gharama za ndege kwa waziri,'� alisema Haule bila kufafanua chuo kililipia kiasi gani na wizara kiasi gani.
  Alisema gharama za kukodisha ndege hiyo ilikuwa dola za Kimarekani 350,000, sawa na sh milioni 5.2 na kusisitiza kuwa kiasi hicho kimelipwa na wizara kwa kushirikiana na Chuo cha Mipango.
  Alipoulizwa sababu ya wizara kulituma shangingi la waziri huyo kutoka Dar es Salaam wakati Dodoma kuna magari ya wizara hiyo yenye hadhi ya waziri, Haule alisema walilazimika kufanya hivyo ili Waziri Mkulo aende na kurudi kuwahi majukumu mengine jijini Dar es Salaam.
  Mwanzoni mwa mwaka huu, Naibu Waziri wa wizara nyeti inayochangia sehemu kubwa ya pato la taifa (jina lake limehifadhiwa), ambayo iliwahi kuwa katika wakati mgumu kutokana na kugubikwa na hoja ya ufisadi, alikumbwa na kashfa ya aina hiyo ya matumizi mabaya ya fedha za serikali.
  Waziri huyo akiambatana na msaidizi wake, alifanya ziara mkoani Kilimanjaro kwa kutumia usafiri wa ndege ya kampuni ya Precision, lakini alilitanguliza gari lake la uwaziri kutoka jijini Dar es Salaam hadi mkoani humo siku mbili kabla ambapo alilitumia kwa takriban saa sita tu na jioni alirejea Dar es Salaam kwa ndege hiyo na kuliacha gari lake likirudi na dereva pekee.
  Gari hilo lilifika mkoani humo siku moja kabla ya waziri huyo na msaidizi wake kufika na mara alipotua katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), majira ya saa 2.30 asubuhi, tayari dereva wa gari lake alikuwa akimsubiri na kumpeleka katika ofisi ya wizara hiyo mkoani humo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi.
  Ilipofika majira ya saa 12 jioni siku hiyo hiyo, Naibu Waziri huyo ambaye ni mmoja wa mawaziri vijana na mara yake ya kwanza kuwa waziri baada ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko madogo ya baraza lake, aliwasili tena KIA na msaidizi wake kwa ajili ya safari ya kurudi jijini Dar es Salaam kwa ndege na kuliacha shangingi lake lililorudi siku iliyofuata.
  Kwa hali hiyo, serikali ililazimika kulipa posho ya siku tatu kwa dereva huyo na gharama za mafuta yaliyotumika kuliwezesha gari hilo kusafiri kwenda na kurudi mkoani Kilimanjaro.
  Malalamiko ya matukio kama hayo, yaliwahi kutolewa bungeni na Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee (CHADEMA) wakati akichangia hoja ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba kigogo mmoja mkoani Kigoma, alialikwa kwenye semina iliyofanyika mjini Bagamoyo na kusafiri kwa ndege, lakini alilitanguliza shangingi lake wiki moja kabla ya yeye kuwasili.
  Halima ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kawe (CHADEMA), alisema gari hilo lilitumika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na mwisho wa semina, alilitumia kumfikisha katika uwanja huo wa ndege na gari hilo lilisafari kurudi Kigoma baada ya kigogo huyo kuondoka.
  Mbunge huyo alilalamikia kuwa hali hiyo imekuwa ikitumiwa na viongozi wengi wa serikali na kumtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa makini kudhibiti matumizi ya aina hiyo kwa watendaji wake.
  Mawaziri hao pia wamekuwa wakilalamikiwa kwa matumizi binafsi ya magari ya serikali kama vile kuyatumia kuwapeleka watoto wao shule katika safari nyingine binafsi ambazo hutumia mafuta ya serikali.
  Wakati yakitumika kwa shughuli hizo binafsi, magari hayo hung'olewa namba za uwaziri na kubandikwa zingine, jambo ambalo linaelezwa na duru za kisiasa kama ni aina nyingine ya ufisadi
   
 2. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  ? We nawe unataka kuongeza posts zako tu kwa kutuletea story za udaku. Ni kufuru gani aliyoifanya?
   
 3. W

  We can JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Afterall,

  PM ni mpole mno? Nadhani. Ni mwoga mno? Sina uhakika. Ni mtu wa busara sana? Yawezekana. Anaganga njaa? Hilo nalo sijui. Je, atamchukulia hatua? Yawezekana baada ya mwaka 2015!
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,595
  Likes Received: 5,776
  Trophy Points: 280
  clouuuuuuuuuuuuuuuuuuuds fmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmmm
   
 5. kagumyamuheto

  kagumyamuheto JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kelele za Chura hizo.
   
 6. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  We mtanzania kweli? udaku uko wapi sasa hapo?
   
 7. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mwaga data tuzungumze kwa vielelezo,yumkini ni mtizamo wako tu...
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Mleta hoja hajasema lolote kuhusiana na story yake. Labda angatuletea source ili tuone kinachoendelea badala ya kutuacha kwenye mataa. Sasa sioni tutachangia nini hapa kwa design ya postings kama ya mleta hoja.
   
 9. kmwemtsi

  kmwemtsi Senior Member

  #9
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  source
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,977
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkulo afanya kufuru
  • Akodi ndege kwenda Dodoma, aagiza shangingi toka Dar

  na Bakari Kimwanga

  [​IMG] WAKATI serikali ikisisitiza kutaka kupunguza gharama za matumizi kwa kuacha kuendelea kununua magari ya kifahari 'mashangingi', baadhi ya matumizi ya mawaziri yanatisha na kuwa mzigo kwa serikali. Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano kwa muda mrefu sasa, umebaini kuwa wapo mawaziri na watendaji wengine wa serikali, wanaofanya ziara mikoani na kusafiri kwa ndege za kukodi, lakini hulazimika kuyaagiza mashangingi yao aina ya G8 kutoka Dar es Salaam hadi katika mikoa wanayokwenda kufanya ziara hata kama yatatumika kwa siku moja.
  Mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Uchumi na Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye wiki iliyopita alikodi ndege kwa fedha za serikali kwenda kuhudhuria mahafari ya Chuo cha Mipango mjini Dodoma, lakini bado aliliagiza gari lake la uwaziri limfuate kutoka jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kulitumia katika mji huo wakati Wizara ya Fedha na Uchumi, ina ofisi na magari mjini Dodoma.
  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano, ulibaini kuwa Desemba 17, mwaka huu, Waziri Mkulo mwenye dhamana ya fedha nchini, alikodi ndege ya Shirika la Tanzania Air, yenye namba za usajili 5HTZC na kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma, majira ya saa nane mchana.
  Wakati Waziri Mkulo akipasua anga la Dodoma kwa ndege ya kukodi, siku hiyo hiyo, dereva wake alilazimika kujaza mafuta shangingi la waziri huyo na kuweka kibindoni posho yake kumfuata bosi wake mjini Dodoma.
  Kwa mujibu wa habari hizo, ndege hiyo ilikodishwa kwa dola za Kimarekani 5,000, sawa na sh milioni 7.5.
  'Mimi niko hazina, hivi sasa serikali haina fedha, kuna madeni mengi, kuna walimu zaidi ya 500,000 waliomaliza vyuo vya elimu ya juu tangu Mei mwaka huu wanasubiri ajira kutokana na ukosefu wa fedha, lakini hazina inafanya matumizi mabaya kila siku. Huku ni kulifilisi taifa bila sababu,'� alisema mtoa habari wetu ambaye jina lake limehifadhiwa.
  Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kuhusina na kashfa hiyo, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, John Haule, alikiri kuwa Desemba 17, mwaka huu, wizara yake ilikodi ndege kwa ajili ya kumuwahisha Waziri Mkulo kuwahi mahafali ya Chuo cha Mipango ambapo alikuwa mgeni rasmi.
  Haule ambaye alikuwa na wakati mgumu kutoa ufafanuzi huo, alisema walilazimika kufanya hivyo kutokana na umuhimu wa kazi alizokuwa nazo Waziri Mkulo siku hiyo kabla ya kuondoka kwenda Dodoma na kusisitiza kuwa ukodishwaji wa ndege ni jambo la kawaida kwa watendaji wa wizara hiyo.
  'Hili ni suala la kawaida kabisa katika utendaji wa wizara yetu; siku hiyo ilikuwa lazima waziri aende Dodoma katika mahafali na kuzindua bodi ya chuo cha mipango, sasa kwa hili tulishirikiana na chuo chenyewe kulipia gharama za ndege kwa waziri,'� alisema Haule bila kufafanua chuo kililipia kiasi gani na wizara kiasi gani.
  Alisema gharama za kukodisha ndege hiyo ilikuwa dola za Kimarekani 350,000, sawa na sh milioni 5.2 na kusisitiza kuwa kiasi hicho kimelipwa na wizara kwa kushirikiana na Chuo cha Mipango.
  Alipoulizwa sababu ya wizara kulituma shangingi la waziri huyo kutoka Dar es Salaam wakati Dodoma kuna magari ya wizara hiyo yenye hadhi ya waziri, Haule alisema walilazimika kufanya hivyo ili Waziri Mkulo aende na kurudi kuwahi majukumu mengine jijini Dar es Salaam.
  Mwanzoni mwa mwaka huu, Naibu Waziri wa wizara nyeti inayochangia sehemu kubwa ya pato la taifa (jina lake limehifadhiwa), ambayo iliwahi kuwa katika wakati mgumu kutokana na kugubikwa na hoja ya ufisadi, alikumbwa na kashfa ya aina hiyo ya matumizi mabaya ya fedha za serikali.
  Waziri huyo akiambatana na msaidizi wake, alifanya ziara mkoani Kilimanjaro kwa kutumia usafiri wa ndege ya kampuni ya Precision, lakini alilitanguliza gari lake la uwaziri kutoka jijini Dar es Salaam hadi mkoani humo siku mbili kabla ambapo alilitumia kwa takriban saa sita tu na jioni alirejea Dar es Salaam kwa ndege hiyo na kuliacha gari lake likirudi na dereva pekee.
  Gari hilo lilifika mkoani humo siku moja kabla ya waziri huyo na msaidizi wake kufika na mara alipotua katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), majira ya saa 2.30 asubuhi, tayari dereva wa gari lake alikuwa akimsubiri na kumpeleka katika ofisi ya wizara hiyo mkoani humo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi.
  Ilipofika majira ya saa 12 jioni siku hiyo hiyo, Naibu Waziri huyo ambaye ni mmoja wa mawaziri vijana na mara yake ya kwanza kuwa waziri baada ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko madogo ya baraza lake, aliwasili tena KIA na msaidizi wake kwa ajili ya safari ya kurudi jijini Dar es Salaam kwa ndege na kuliacha shangingi lake lililorudi siku iliyofuata.
  Kwa hali hiyo, serikali ililazimika kulipa posho ya siku tatu kwa dereva huyo na gharama za mafuta yaliyotumika kuliwezesha gari hilo kusafiri kwenda na kurudi mkoani Kilimanjaro.
  Malalamiko ya matukio kama hayo, yaliwahi kutolewa bungeni na Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee (CHADEMA) wakati akichangia hoja ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba kigogo mmoja mkoani Kigoma, alialikwa kwenye semina iliyofanyika mjini Bagamoyo na kusafiri kwa ndege, lakini alilitanguliza shangingi lake wiki moja kabla ya yeye kuwasili.
  Halima ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kawe (CHADEMA), alisema gari hilo lilitumika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na mwisho wa semina, alilitumia kumfikisha katika uwanja huo wa ndege na gari hilo lilisafari kurudi Kigoma baada ya kigogo huyo kuondoka.
  Mbunge huyo alilalamikia kuwa hali hiyo imekuwa ikitumiwa na viongozi wengi wa serikali na kumtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa makini kudhibiti matumizi ya aina hiyo kwa watendaji wake.
  Mawaziri hao pia wamekuwa wakilalamikiwa kwa matumizi binafsi ya magari ya serikali kama vile kuyatumia kuwapeleka watoto wao shule katika safari nyingine binafsi ambazo hutumia mafuta ya serikali.
  Wakati yakitumika kwa shughuli hizo binafsi, magari hayo hung'olewa namba za uwaziri na kubandikwa zingine, jambo ambalo linaelezwa na duru za kisiasa kama ni aina nyingine ya ufisadi
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,977
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Are you serious?
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,977
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Zipi hizo?
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,977
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Takwimu sasa wazihitaji.........Source ni Tanzania Daima na somo lote lipo hapo juu.........................
   
 14. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkulo afanya kufuru
  • Akodi ndege kwenda Dodoma, aagiza shangingi toka Dar

  na Bakari Kimwanga

  [​IMG]
  WAKATI serikali ikisisitiza kutaka kupunguza gharama za matumizi kwa kuacha kuendelea kununua magari ya kifahari 'mashangingi', baadhi ya matumizi ya mawaziri yanatisha na kuwa mzigo kwa serikali. ​

  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano kwa muda mrefu sasa, umebaini kuwa wapo mawaziri na watendaji wengine wa serikali, wanaofanya ziara mikoani na kusafiri kwa ndege za kukodi, lakini hulazimika kuyaagiza mashangingi yao aina ya G8 kutoka Dar es Salaam hadi katika mikoa wanayokwenda kufanya ziara hata kama yatatumika kwa siku moja.
  Mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Uchumi na Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye wiki iliyopita alikodi ndege kwa fedha za serikali kwenda kuhudhuria mahafari ya Chuo cha Mipango mjini Dodoma, lakini bado aliliagiza gari lake la uwaziri limfuate kutoka jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kulitumia katika mji huo wakati Wizara ya Fedha na Uchumi, ina ofisi na magari mjini Dodoma.
  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano, ulibaini kuwa Desemba 17, mwaka huu, Waziri Mkulo mwenye dhamana ya fedha nchini, alikodi ndege ya Shirika la Tanzania Air, yenye namba za usajili 5HTZC na kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma, majira ya saa nane mchana.
  Wakati Waziri Mkulo akipasua anga la Dodoma kwa ndege ya kukodi, siku hiyo hiyo, dereva wake alilazimika kujaza mafuta shangingi la waziri huyo na kuweka kibindoni posho yake kumfuata bosi wake mjini Dodoma.
  Kwa mujibu wa habari hizo, ndege hiyo ilikodishwa kwa dola za Kimarekani 5,000, sawa na sh milioni 7.5.
  'Mimi niko hazina, hivi sasa serikali haina fedha, kuna madeni mengi, kuna walimu zaidi ya 500,000 waliomaliza vyuo vya elimu ya juu tangu Mei mwaka huu wanasubiri ajira kutokana na ukosefu wa fedha, lakini hazina inafanya matumizi mabaya kila siku. Huku ni kulifilisi taifa bila sababu,' alisema mtoa habari wetu ambaye jina lake limehifadhiwa.
  Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kuhusina na kashfa hiyo, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, John Haule, alikiri kuwa Desemba 17, mwaka huu, wizara yake ilikodi ndege kwa ajili ya kumuwahisha Waziri Mkulo kuwahi mahafali ya Chuo cha Mipango ambapo alikuwa mgeni rasmi.
  Haule ambaye alikuwa na wakati mgumu kutoa ufafanuzi huo, alisema walilazimika kufanya hivyo kutokana na umuhimu wa kazi alizokuwa nazo Waziri Mkulo siku hiyo kabla ya kuondoka kwenda Dodoma na kusisitiza kuwa ukodishwaji wa ndege ni jambo la kawaida kwa watendaji wa wizara hiyo.
  'Hili ni suala la kawaida kabisa katika utendaji wa wizara yetu; siku hiyo ilikuwa lazima waziri aende Dodoma katika mahafali na kuzindua bodi ya chuo cha mipango, sasa kwa hili tulishirikiana na chuo chenyewe kulipia gharama za ndege kwa waziri,' alisema Haule bila kufafanua chuo kililipia kiasi gani na wizara kiasi gani.
  Alisema gharama za kukodisha ndege hiyo ilikuwa dola za Kimarekani 350,000, sawa na sh milioni 5.2 na kusisitiza kuwa kiasi hicho kimelipwa na wizara kwa kushirikiana na Chuo cha Mipango.
  Alipoulizwa sababu ya wizara kulituma shangingi la waziri huyo kutoka Dar es Salaam wakati Dodoma kuna magari ya wizara hiyo yenye hadhi ya waziri, Haule alisema walilazimika kufanya hivyo ili Waziri Mkulo aende na kurudi kuwahi majukumu mengine jijini Dar es Salaam.
  Mwanzoni mwa mwaka huu, Naibu Waziri wa wizara nyeti inayochangia sehemu kubwa ya pato la taifa (jina lake limehifadhiwa), ambayo iliwahi kuwa katika wakati mgumu kutokana na kugubikwa na hoja ya ufisadi, alikumbwa na kashfa ya aina hiyo ya matumizi mabaya ya fedha za serikali.
  Waziri huyo akiambatana na msaidizi wake, alifanya ziara mkoani Kilimanjaro kwa kutumia usafiri wa ndege ya kampuni ya Precision, lakini alilitanguliza gari lake la uwaziri kutoka jijini Dar es Salaam hadi mkoani humo siku mbili kabla ambapo alilitumia kwa takriban saa sita tu na jioni alirejea Dar es Salaam kwa ndege hiyo na kuliacha gari lake likirudi na dereva pekee.
  Gari hilo lilifika mkoani humo siku moja kabla ya waziri huyo na msaidizi wake kufika na mara alipotua katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), majira ya saa 2.30 asubuhi, tayari dereva wa gari lake alikuwa akimsubiri na kumpeleka katika ofisi ya wizara hiyo mkoani humo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi.
  Ilipofika majira ya saa 12 jioni siku hiyo hiyo, Naibu Waziri huyo ambaye ni mmoja wa mawaziri vijana na mara yake ya kwanza kuwa waziri baada ya Rais Kikwete kufanya mabadiliko madogo ya baraza lake, aliwasili tena KIA na msaidizi wake kwa ajili ya safari ya kurudi jijini Dar es Salaam kwa ndege na kuliacha shangingi lake lililorudi siku iliyofuata.
  Kwa hali hiyo, serikali ililazimika kulipa posho ya siku tatu kwa dereva huyo na gharama za mafuta yaliyotumika kuliwezesha gari hilo kusafiri kwenda na kurudi mkoani Kilimanjaro.
  Malalamiko ya matukio kama hayo, yaliwahi kutolewa bungeni na Mbunge wa Viti Maalum, Halima Mdee (CHADEMA) wakati akichangia hoja ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba kigogo mmoja mkoani Kigoma, alialikwa kwenye semina iliyofanyika mjini Bagamoyo na kusafiri kwa ndege, lakini alilitanguliza shangingi lake wiki moja kabla ya yeye kuwasili.
  Halima ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kawe (CHADEMA), alisema gari hilo lilitumika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na mwisho wa semina, alilitumia kumfikisha katika uwanja huo wa ndege na gari hilo lilisafari kurudi Kigoma baada ya kigogo huyo kuondoka.
  Mbunge huyo alilalamikia kuwa hali hiyo imekuwa ikitumiwa na viongozi wengi wa serikali na kumtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa makini kudhibiti matumizi ya aina hiyo kwa watendaji wake.
  Mawaziri hao pia wamekuwa wakilalamikiwa kwa matumizi binafsi ya magari ya serikali kama vile kuyatumia kuwapeleka watoto wao shule katika safari nyingine binafsi ambazo hutumia mafuta ya serikali.
  Wakati yakitumika kwa shughuli hizo binafsi, magari hayo hung'olewa namba za uwaziri na kubandikwa zingine, jambo ambalo linaelezwa na duru za kisiasa kama ni aina nyingine ya ufisadi.  [​IMG]

  juu[​IMG] [​IMG]
   
 15. L

  Leonard Mwanja Member

  #15
  Dec 29, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ndio tujue viongozi wetu hawana uchungu na nchi hii yetu macho lkn kuna ck watajua machungu yetu ni watu wa kutandikwa viboko tu bila huruma
   
 16. m

  mapambano JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah sasa hii nchi sijui inakwenda wapi...Huyu na JK lao moja. FISADI MKULO anayekuwekea kifua ni JK kwa sababu wewe haulizi gharama ya safari za vasco...
   
 17. Lisa Rina

  Lisa Rina JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 1,771
  Likes Received: 2,043
  Trophy Points: 280
  duh
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ahca mibange imekuharibu sana tu... hukua hivyo mazee
   
 19. k

  kayumba JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Si Mawaziri peke yao hata matumizi ya watumishi wa umma wengine nayo yanatisha!  Ndege ilikodiwa kwenda tu, waliogopa asipande SHABIB wakati wa kurudi nini?

  Hawa watendaji wetu huwa hawajui kipi wakipe kipaumbele katika taifa letu! Pole sana Mzalendo lakini Tanzania ndivyo nchi inavyoendeshwa. Kwani mbona watembelea magari ya Mil. 200 wakati shule hata za mkoani Dar es salaam zina watoto wanakaa chini kisa Hakuna madawati?

  Ningekubali hakuna pesa ya madawati endapo Viongozi wangekuwa wanatumia BAJAJ Period!

  Ebu angalia maneno ya hawa watendaji wa Serikali, Eti kukodi ndege ni jambo la kawaida kwa watendaji wa wizara yao?

  Je ni kwasababu wao ndiyo wenye kutunza hazina au na watendaji wa wizara nyingine huwa wanaruhusiwa kukodi ndege?

  Kauli hizi ndizo zile za Prof. Kapuya alipoulizwa kuhusu kutumia ndege ya Jeshi kwa matumizi binafsi, "Eti hata watangulizi wangu walikuwa wanatumia ndege za jeshi"!

  Pinda hapo upo? Kumbe wakati unazuia Mashangingi wengine kukodi ndege ni jambo la kawaida!!!!!

  Tuondoleeni hawa watu wenye fikra mgando Serikalini.  Kumbe kila wizara ufujaji ni ule ule!

  Haya matumizi ya ovyo ya pesa za walipa kodi yakikomeshwa mbona tutanunua Ambulance kwa vituo vya afya badala ya Bajaj 400 alizoahidi mkuu wa kaya!

  Watumishi wengi hawajui mipaka ya matumizi ya magari ya umma, si mnakumbuka Pombe Magufuli alikuta wengine washajimilikisha magari ya umma!

  Ni makosa kutumia magari ya umma kwa matumizi binafsi, lakini wote tunajua haya magari yanavyopisha kila kukicha mitaani yakiwa kwenye misele isiyo na manufaa kwa umma. Ukiuliza wanasema mbona hiyo ni kawaida!  UHURU wa kweli bado kupatikani.....!
   
 20. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #20
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hii nayo kali
   
Loading...