Huyo mdee aliliona la waziri wa ccm kuwa ni ubadhirifu, lakini sijamsikia akiongelea ya zitto kabwe aliye kodiwa ndege na mfuko wa pension wa ppf kama shukrani kwa kuzima soo la ufisadi. Bunge hutoa fedha za usafiri kwa kamati zake, ppf wanakodi ndege kumpeleka zitto kabwe bukoba kama nani? Wanachezea fedha zetu wachangiaji huku tukiishia kupewa pension ya shs. 21,000 kwa kwa mwezi. Wizi mtupu.
waziri mkulo afanya kufuru
• akodi ndege kwenda dodoma, aagiza shangingi toka dar
na bakari kimwanga
wakati serikali ikisisitiza kutaka kupunguza gharama za matumizi kwa kuacha kuendelea kununua magari ya kifahari 'mashangingi', baadhi ya matumizi ya mawaziri yanatisha na kuwa mzigo kwa serikali.
uchunguzi uliofanywa na tanzania daima jumatano kwa muda mrefu sasa, umebaini kuwa wapo mawaziri na watendaji wengine wa serikali, wanaofanya ziara mikoani na kusafiri kwa ndege za kukodi, lakini hulazimika kuyaagiza mashangingi yao aina ya g8 kutoka dar es salaam hadi katika mikoa wanayokwenda kufanya ziara hata kama yatatumika kwa siku moja.
Mmoja wa mawaziri hao ni waziri wa uchumi na fedha, mustafa mkulo, ambaye wiki iliyopita alikodi ndege kwa fedha za serikali kwenda kuhudhuria mahafari ya chuo cha mipango mjini dodoma, lakini bado aliliagiza gari lake la uwaziri limfuate kutoka jijini dar es salaam kwa ajili ya kulitumia katika mji huo wakati wizara ya fedha na uchumi, ina ofisi na magari mjini dodoma.
Uchunguzi uliofanywa na tanzania daima jumatano, ulibaini kuwa desemba 17, mwaka huu, waziri mkulo mwenye dhamana ya fedha nchini, alikodi ndege ya shirika la tanzania air, yenye namba za usajili 5htzc na kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini dodoma, majira ya saa nane mchana.
Wakati waziri mkulo akipasua anga la dodoma kwa ndege ya kukodi, siku hiyo hiyo, dereva wake alilazimika kujaza mafuta shangingi la waziri huyo na kuweka kibindoni posho yake kumfuata bosi wake mjini dodoma.
Kwa mujibu wa habari hizo, ndege hiyo ilikodishwa kwa dola za kimarekani 5,000, sawa na sh milioni 7.5.
'mimi niko hazina, hivi sasa serikali haina fedha, kuna madeni mengi, kuna walimu zaidi ya 500,000 waliomaliza vyuo vya elimu ya juu tangu mei mwaka huu wanasubiri ajira kutokana na ukosefu wa fedha, lakini hazina inafanya matumizi mabaya kila siku. Huku ni kulifilisi taifa bila sababu,' alisema mtoa habari wetu ambaye jina lake limehifadhiwa.
Akizungumza na tanzania daima jumatano kuhusina na kashfa hiyo, kaimu katibu mkuu wizara ya fedha, john haule, alikiri kuwa desemba 17, mwaka huu, wizara yake ilikodi ndege kwa ajili ya kumuwahisha waziri mkulo kuwahi mahafali ya chuo cha mipango ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Haule ambaye alikuwa na wakati mgumu kutoa ufafanuzi huo, alisema walilazimika kufanya hivyo kutokana na umuhimu wa kazi alizokuwa nazo waziri mkulo siku hiyo kabla ya kuondoka kwenda dodoma na kusisitiza kuwa ukodishwaji wa ndege ni jambo la kawaida kwa watendaji wa wizara hiyo.
'hili ni suala la kawaida kabisa katika utendaji wa wizara yetu; siku hiyo ilikuwa lazima waziri aende dodoma katika mahafali na kuzindua bodi ya chuo cha mipango, sasa kwa hili tulishirikiana na chuo chenyewe kulipia gharama za ndege kwa waziri,' alisema haule bila kufafanua chuo kililipia kiasi gani na wizara kiasi gani.
Alisema gharama za kukodisha ndege hiyo ilikuwa dola za kimarekani 350,000, sawa na sh milioni 5.2 na kusisitiza kuwa kiasi hicho kimelipwa na wizara kwa kushirikiana na chuo cha mipango.
Alipoulizwa sababu ya wizara kulituma shangingi la waziri huyo kutoka dar es salaam wakati dodoma kuna magari ya wizara hiyo yenye hadhi ya waziri, haule alisema walilazimika kufanya hivyo ili waziri mkulo aende na kurudi kuwahi majukumu mengine jijini dar es salaam.
Mwanzoni mwa mwaka huu, naibu waziri wa wizara nyeti inayochangia sehemu kubwa ya pato la taifa (jina lake limehifadhiwa), ambayo iliwahi kuwa katika wakati mgumu kutokana na kugubikwa na hoja ya ufisadi, alikumbwa na kashfa ya aina hiyo ya matumizi mabaya ya fedha za serikali.
Waziri huyo akiambatana na msaidizi wake, alifanya ziara mkoani kilimanjaro kwa kutumia usafiri wa ndege ya kampuni ya precision, lakini alilitanguliza gari lake la uwaziri kutoka jijini dar es salaam hadi mkoani humo siku mbili kabla ambapo alilitumia kwa takriban saa sita tu na jioni alirejea dar es salaam kwa ndege hiyo na kuliacha gari lake likirudi na dereva pekee.
Gari hilo lilifika mkoani humo siku moja kabla ya waziri huyo na msaidizi wake kufika na mara alipotua katika uwanja wa kimataifa wa kilimanjaro (kia), majira ya saa 2.30 asubuhi, tayari dereva wa gari lake alikuwa akimsubiri na kumpeleka katika ofisi ya wizara hiyo mkoani humo kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi.
Ilipofika majira ya saa 12 jioni siku hiyo hiyo, naibu waziri huyo ambaye ni mmoja wa mawaziri vijana na mara yake ya kwanza kuwa waziri baada ya rais kikwete kufanya mabadiliko madogo ya baraza lake, aliwasili tena kia na msaidizi wake kwa ajili ya safari ya kurudi jijini dar es salaam kwa ndege na kuliacha shangingi lake lililorudi siku iliyofuata.
Kwa hali hiyo, serikali ililazimika kulipa posho ya siku tatu kwa dereva huyo na gharama za mafuta yaliyotumika kuliwezesha gari hilo kusafiri kwenda na kurudi mkoani kilimanjaro.
Malalamiko ya matukio kama hayo, yaliwahi kutolewa bungeni na mbunge wa viti maalum, halima mdee (chadema) wakati akichangia hoja ya ofisi ya waziri mkuu kwamba kigogo mmoja mkoani kigoma, alialikwa kwenye semina iliyofanyika mjini bagamoyo na kusafiri kwa ndege, lakini alilitanguliza shangingi lake wiki moja kabla ya yeye kuwasili.
Halima ambaye kwa sasa ni mbunge wa kawe (chadema), alisema gari hilo lilitumika kumpokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu nyerere jijini dar es salaam na mwisho wa semina, alilitumia kumfikisha katika uwanja huo wa ndege na gari hilo lilisafari kurudi kigoma baada ya kigogo huyo kuondoka.
Mbunge huyo alilalamikia kuwa hali hiyo imekuwa ikitumiwa na viongozi wengi wa serikali na kumtaka waziri mkuu mizengo pinda kuwa makini kudhibiti matumizi ya aina hiyo kwa watendaji wake.
Mawaziri hao pia wamekuwa wakilalamikiwa kwa matumizi binafsi ya magari ya serikali kama vile kuyatumia kuwapeleka watoto wao shule katika safari nyingine binafsi ambazo hutumia mafuta ya serikali.
wakati yakitumika kwa shughuli hizo binafsi, magari hayo hung'olewa namba za uwaziri na kubandikwa zingine, jambo ambalo linaelezwa na duru za kisiasa kama ni aina nyingine ya ufisadi.
Habari za "kuchakachua" kura zishaanza kuwa boring kwa hiyo zinatafutwa habari zingine kinguvu. Kwani huko Dodoma alienda kwenye kitchen party ya mwanae hata mpige kelele kama wendawazimu?
Nauliza. Nikipewa posho. Sehemu ya posho nikalipia tiketi ya ndege au nikiwa nimepewa complimentary ticket ni kufuru kwa dereva wangu kwenda kunisubiri huko ninakoenda? Nauliza tu?
WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, amewashukia watendaji wa ofisi yake kwamba wanahatarisha maisha yake kwa kuvujisha siri za wizara hiyo.
Mkulo alitoa kauli hiyo baada ya gazeti hili hivi karibuni kuripoti kuwa alikodi ndege kwenda Dodoma na kumuagiza dereva wake amfuate kwa shangingi lake aina ya G8.
Waziri huyo alisema hayo jana wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi katika wizara hiyo kwenye ukumbi wa BZ, ulioko nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Bila kutaja majina, waziri huyo mwenye dhamana ya fedha, alisema utafiti wake umeonyesha kuwa wavujishaji wakuu wa siri katika wizara yake ni wakurugenzi, makamishina na watendaji wa kati.
Akitoa mfano na kulihusisha gazeti hili, Mkulo alisema umeibuka mtindo wa baadhi ya watumishi hususan makao makuu ya wizara hiyo kutoa siri za ofisi na wizara kwenye vyombo vya habari, kuwachafua mawaziri waonekane wafujaji fedha za umma ili wawajibishwe.
"Hivi karibuni gazeti moja (Tanzania Daima Jumatano), likaamua kufuatilia safari ya waziri na dereva wake toka Dar es Salaam kwenda Dodoma baada ya kukodiwa ndege kwa gharama ya dola 5,000 bila kufanya uchunguzi kwa sababu gani ilifanyika hivyo...lakini ilikuwa imesukwa na baadhi ya watendaji wetu, tena wamo humu ili wamchafue Mkulo," alisema.
Katika hotuba hiyo iliyokuwa fupi lakini iliyorefushwa na ufafanuzi wa taarifa hiyo iliyoonyesha kumkera sana Waziri Mkulo hivyo kumlazimu kutumia zaidi ya dakika 30 kutoa ufafanuzi juu ya mazingira ya kukodiwa ndege hiyo, Mkulo alisema hana mamlaka ya kujiamulia kukodi ndege na kuongeza kuwa tangu awe waziri, amekodiwa ndege mara nane tu.
Mkulo ambaye alionyesha kukerwa sana na taarifa hiyo, alisema wizara iliamua kumkodia ndege hiyo yeye na dereva wake kwenda Dodoma kutokana na majukumu yaliyokuwa yakimkabili likiwemo la kulazimika kukutana na baadhi ya mabalozi na mawaziri wa fedha toka nje ya nchi ambao walikuwa wanaliingizia taifa takriban dola za Kimarekani milioni 100.
"Akaandaliwa mwandishi uwanja wa ndege Dar es Salaam apige picha ndege anayopanda waziri na kule Dodoma akaandaliwa mwandishi kupiga picha ndege atakayoshuka waziri...ni hatari sana; hebu fikiria kama wangekuwa maharamia mimi si nigeuawa kwa dola 5,000 zinazodaiwa nimefuja!?" aliongeza.
Akitahadharisha juu ya kutokuwa na siri katika utumishi hususan serikalini katika wizara nyeti kama hazina ambayo ni roho ya nchi, Mkulo alisema kama hakuna usiri wa nyaraka katika serikali yoyote waelewe kuwa hakutakuwa na utawala.
Alisema nyaraka za serikali sasa zimezagaa mitaani hususan kwenye masoko likiwemo la Kariakoo jijini Dar es Salaam zikitumika katika matumizi yasiyo sahihi kwa wafanyabiashara ndogondogo wakiwemo wauza vitumbua na karanga.
Awali Naibu Waziri wa Fedha, Gregory Teu, akiwasalimia wafanyakazi katika mkutano huo jana alisema mbali na kulitumikia taifa kama mkaguzi na mdhibiti wa mali za serikali amebaini kuwa wizara hiyo inakabiliwa na tatizo la matumizi makubwa kuliko mapato jambo linalosababisha kushindwa kufikia malengo.
Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Waziri Mkulo alikodi ndege kwa fedha za serikali kwenda kuhudhuria mahafari ya Chuo cha Mipango mjini Dodoma, lakini bado aliliagiza gari lake la uwaziri limfuate kutoka jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kulitumia katika mji huo wakati Wizara ya Fedha na Uchumi ina ofisi na magari mjini Dodoma.
Waziri Mkulo mwenye dhamana ya fedha nchini, alikodi ndege ya Shirika la Tanzania Air, yenye namba za usajili 5HTZC na kuwasili katika uwanja wa ndege wa mjini Dodoma, majira ya saa nane mchana.
Wakati Waziri Mkulo akipasua anga la Dodoma kwa ndege ya kukodi, siku hiyo hiyo, dereva wake alilazimika kujaza mafuta shangingi la waziri huyo na kuweka kibindoni posho yake kumfuata bosi wake mjini Dodoma.
Taarifa hiyo ambayo ilimkera sana Waziri Mkulo, ilidai kuwa ndege hiyo ilikodishwa kwa dola za Kimarekani 5,000, sawa na sh milioni 7.5.
MY TAKE
Hapo kwenye nyekundu, sijui mheshimwa Mkulo alitaka kuwaambia nini Watanzania. Sikujua Wizara ya Fedha kuna biashara ya kullingizia taifa mabilioni, Mkulo anataka kusema kuwa kama asingekuwepo nchi isingepata hizo fedha. Na je hiyo inakuwaje excuse ya kukodiwa ndege? kwani alikuwa hajui kuhusu hiyo mikutano na wafadhili, kwani asingeweza kuwakilishwa huko Dodoma? Au Dodoma nako alikuwa anaenda kuliingizia taifa mabilioni? Ningemuelewa kama angekodiwa ndege kuwahi mikutano na wafadhili, but not other way round!!! Nimekuwa confused na the whole episode na sijui Mkulo anataka kusema nini, loh
Wakati Waziri Mkulo akipasua anga la Dodoma kwa ndege ya kukodi, siku hiyo hiyo, dereva wake alilazimika kujaza mafuta shangingi la waziri huyo na kuweka kibindoni posho yake kumfuata bosi wake mjini Dodoma.
Taarifa hiyo ambayo ilimkera sana Waziri Mkulo, ilidai kuwa ndege hiyo ilikodishwa kwa dola za Kimarekani 5,000, sawa na sh milioni 7.5.
Hiyo haina tofauti na double payment.Milioni 7.5 ni sawa na mishahara ya walimu wangapi kwa mwezi vile????....
Huo uharaka pekee unaonyesha jinsi gani watu wa serikali wasivyoweza kujipanga kutokana na priority zilizopo. Kila mtu anatumia fedha bila kujua athari zake kesho na bado wanasema eti nao wamesoma.Huko ndio kusomea nini? Kuubomoa uchumi?
Yaani Mbaha, hizo fedha ni sawa na Mishahara ya Walimu 30 kwa hesabu za haraka haraka. Shule ngapi zina mwalimu mmoja na hata hakuna madawati na mwalimu mwenyewe huyo mmoja hana motisha wowote?.Tunajenga Taifa au tunaandaa "Time Bomb" litakalolipuka huko mbeleni. Ninavyofahamu Mabalozi wa nje na other Diplomats huwa wana ratiba zao tena very systematic. There is no way kwamba Waziri alikurupushwa na hakuja hicho kikao. This is not an excuse Mhishimiwa Waziri.Awajibke :kev: :A S-fire1:
Huo uharaka pekee unaonyesha jinsi gani watu wa serikali wasivyoweza kujipanga kutokana na priority zilizopo. Kila mtu anatumia fedha bila kujua athari zake kesho na bado wanasema eti nao wamesoma.Huko ndio kusomea nini? Kuubomoa uchumi?
Kazi ipo , yawezekana mhe. hakujua kilichokuwa kinaendelea , RA aliconclude deal ikatakiwa sahihi ya waziri akaitishwa mara moja kwa misingi ya kutopoteza USD Mil 100 , hapa sijui kama yeye na wataalam wake walisoma Masharti yanayoambatana na hiyo USD Mil. 100 ; baada ya muda ni maumivu kwa walipa kodi.
mkulo ni mpumbafffffff kabisa,yeye anaona kwa vile alikuwa anaenda kuliingizia taifa dola mil 100 basi dola 5000 is nothing, shame on u mkulo!!!!!! na uyo dereva kukufata huko dodoma ni ni si wiziii huo??????????
watu wa Mlingotini huwa hawakosi vijisababu! si bure akaenda Mlingotini kumtafuta mbaya wake! Hivi si niliskia Precisionair inaenda Dodoma au mawaziri hawaruhusiwi kutembelea public flights?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.