Waziri Membe wakati ukisubiri kuoteshwa, kuna alama za kuuliza zinazojirudia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Membe wakati ukisubiri kuoteshwa, kuna alama za kuuliza zinazojirudia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hon.MP, Aug 6, 2012.

 1. H

  Hon.MP Senior Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hotuba ya Kamati ya Bunge na pia kwa namna fulani Kambi rasmi ya upinzani inayosimamia Wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa zimerejesha tena alama ya kuuliza katika yale maswali ya kila mwaka yanayohusu ubalozi mdogo nchini Uholanzi (The Netherlands) na ‘chenji’ ya rada.


  1. Alama ya kuuliza juu ya makusanyo ya fedha yapatikanayo tokana na uuzaji wa visa nje e.g Uholanzi n.k.
  2. Alama ya kuuliza juu ya uwezo na kuendelea (bila vigezo wala ukomo) wa huyo Honorary Counsul raia wa Uholanzi na ushauri wake mbovu juu ya kuuza jengo linalomilikiwa na Tanzania (pateni ukweli kutoka kwa mstaafu balozi Simon).  3. Alama ya kuuliza kwa nini Uholanzi isiwe na Ubalozi kamili kutokana na uzito wa mahusiano na michango ya Uholanzi katika utalii na uchumi wetu kwa ujumla.
  4. Alama ya kuuliza kwa kushindwa kuwaweka wazi wahusika katika wizi wa fedha ya Rada (wakati umeshasema kuwa unawafahamu). Watamke mara moja tu bila kurudia!  Mh. Membe, je ni kweli umeshindwa kushughulikia hizi alama za kuuliza? Wakati unasubiri kuoteshwa, hili ni moja ya doa kubwa sana katika utendaji wako na serikali kwa ujumla.  Hata jinsi mnavyoshughulikia suala la diaspora lina sintofahamu kubwa sana kwa kuwapa upendeleo wa kizamani nchi za Uingerenza na Marekani (msemo wa kuendelea kutafuta rangi ya paka badala ya uwezo wa kukamata panya) kuliko kuweka uwiano mzuri pia katika nchi nyingine katika mabara yote.
   
 2. M

  Mzee wa Usafi JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 634
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  "3. Alama ya kuuliza kwa nini Uholanzi isiwe na Ubalozi kamili kutokana na uzito wa mahusiano na michango ya Uholanzi katika utalii na uchumi wetu kwa ujumla." Hon.MP, kwa habari nilizo nazo Uholanzi wanataka kufunga kabisa ofisi yake ya ubalozi pale Dar na ile ofisi ndogo ya Arusha..Hii ni baada ya Kampuni moja ya Uholanzi kushinda tenda ya kazi ya ukimwi na serikali ikachakachua tenda hiyo na kuipatia uingereza. uholanzi inasema yenyewe inatoa sponsorship kwa wanafunzi zaidi ya 350 kwa mwaka watz inapokuja suala la biashara tz inawakimbili watoa rushwa...hii habari uliza mtu yeyote aliye rudi mwaka huu kutoka kwenye vyuo mbalimbali huko uholanzi anajua...balozi wa heshima wa tz nchini uholanzi ni shuhuda
   
 3. H

  Hon.MP Senior Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzee wa usafi kweli inabidi Waziri Membe katika kukamilisha hotuba yake ya bajeti azungumzie haya maswali ni aibu sana kama na hilo la tenda ni ukweli.
   
 4. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  "2. Alama ya kuuliza juu ya uwezo na kuendelea (bila vigezo wala ukomo) wa huyo Honorary Counsul raia wa Uholanzi na ushauri wake mbovu juu ya kuuza jengo linalomilikiwa na Tanzania (pateni ukweli kutoka kwa mstaafu balozi Simon)."

  Membe kajibu kuwa kuanzia sasa wataweka Consul Generals WATANZANIA. Haya ngoja tuone utekelezaji wake maana hiyo ni kauli inayopokelewa kwa mikono miwili lakini isipotekelezwa itakuwa ni hukumu yake mwenyewe!
   
Loading...