Waziri chengerwa awadhihirishia Watanzania kuwa; kero za Wizara ya Utamaduni na Michezo zinaenda kuisha kupitia bajeti yake ya 2022/23

Acholile

Member
May 30, 2022
91
59
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa leo amewasilisha bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 ya zaidi ya shilingi bilioni 35.4

Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni jijini Dodoma Waziri Mchengerwa amesema kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni 8.2 ni Mishahara ,Bilioni 11.3 ni matumizi mengineyo na Bilioni 15.8 ni ya miradi ya Maendeleo.

Waziri Mchengerwa amesema kwa mwaka 2022/23 Wizara inatarajia kukusanya jumla ya Shilingi Milioni Mia Tisa (Sh.900,000,000) kupitia Idara ya Maendeleo ya Michezo ikiwa vyanzo vya mapato hayo ni pamoja na viingilio katika matukio ya michezo yanayofanyika katika viwanja vya Benjamin Mkapa na Uhuru, kukodisha kumbi na gym zilizopo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na ada za mafunzo kutoka Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya.

Aidha kwa upande wa Taasisi sita (6) zilizo chini ya Wizara hiyo kiasi kinachokadiriwa kukusanywa ni Shilingi Bilioni 5.3.

Waziri Mohd Mchengerwa ameongeza katika kuhakikisha Tanzania inakidhi vigezo vya kuandaa mashindano ya Kimataifa na Kikanda, Serikali katika mwaka 2022/23 imetenga kiasi cha Shilingi Billioni 10 kwa ajili ya Ukarabati wa viwanja na amesisitiza hatua ya kwanza vitaanza viwanja saba (7) vilivyopo katika Majiji, ambavyo ni Jamhuri – Dodoma, Sheikh Amri Abeid - Arusha, Sokoine - Mbeya, CCM Kirumba – Mwanza, na Mkwakwani - Tanga, ukarabati huo utavihusisha viwanja vya Uhuru na Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo ukarabati viwanja vingine ikiwa ni pamoja na kuweka nyasi bandia na majukwaa katika mikoa ya Kigoma, Rukwa, Mtwara, Iringa, Tabora na Shinyanga baada ya kujadiliana na wamiliki wa viwanja hivyo.

"Mkakati huu utaiwezesha kufanikisha Ndoto za Rais Samia Suluhu Hassan za Tanzania kuandaa mashindano makubwa ya mchezo wa soka ya Klabu Bingwa Afrika (AFCON) ambayo tayari Tanzania imependekezwa kuandaa kwa mwaka 2027". amesema Waziri wa Utamaduni , Sanaa na Michezo; Mohamed Mchengerwa.
VIVA MADAME President Rais SSH ; kwa kufanya chaguo sahihi

VIVA COMRADE mohamed Mchengerwa
06.06.2022
 
Hizo hela kuliko kukarabati viwanja vya CCM bora wajenge uwanja mmoja mpya Iringa, Mbeya au Songea huko ardhi ipo wadau wapo ila hakunaa kiwanja bora
 
Back
Top Bottom