Waziri Mbarawa atofautiana na Makonda, ataka Magari ya Serikali yatengenezwe na TAMESA

Mambo mengine daah...
Magari mmeka nayo kwenye yard za serikali miaka kibao hamjakumbuka kuyafufua..

Leo anaijtokeza mtu na kutafuta wadhamini wa kuyafufua, unaongea kwamba yanatakiwa yaende TAMESA, kama unalijua hilo ulichukua hatua gani kufanikisha hilo...


Cc: mahondaw
 
View attachment 621940

Akizungumza leo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa asema kuwa, Magari yote ya Serikali yanapaswa kutengenezwa na WAKALA wa ufundi wa umeme (Tanzania Mechanical and Electronics Service Agency (TAMESA), kwani ndio wenye kazi ya kutengeneza.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda Jumanne hii amekabidhi mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya DAR COACH LTD kwaajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa.

Mabasi hayo 10 chakavu yanatoka kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion moja fedha ya Serikali.

RC Makonda amesema kuwa gari hizo zitatengenezwa na kukamilika ndani ya siku 90 ambapo ameipongeza Kampuni ya DAR COACH LTD kwa kujitolea kukarabati Magari hayo bila kutumia pesa ya Serikali.

HABARI,
Napenda kumpongeza MH,MKUU wa mkoa kwa hatua madhubuti za kuimarisha uwezo wa majeshi yetu,Ila kwa JWTZ kutengenezewa magari hapo mimi sikubaliani nalo kama JESHI liliweza kutengeneza gari NYUMBU iweje kukarabati tu magari iwe shida.Hata nchi rafiki tulizofata mifumo yao kama china jeshi lake ndio lenye teknologia kubwa na vifaa vya kisasa na ndio linlofanya kazi kubwa ndani ya china hasa miradi ujenzi.
Kwa hilo JWTZ sidhani kama ni kweli.

LUMUMBA
 
Mnaolalamikia Wahindi wana ajenda sijui nini tabu ni hamjui kufanya biashara na kuangalia mbele. Hamuoni kuwa kazi hiyo ni bomba kwao kwa kupata kazi zingine nyingi mbeleni!?
Kuna watu wanasukumwa kwa chuki
Biashara mtu kuielewa inataka akili ya ziada
 
Mnaolalamikia Wahindi wana ajenda sijui nini tabu ni hamjui kufanya biashara na kuangalia mbele. Hamuoni kuwa kazi hiyo ni bomba kwao kwa kupata kazi zingine nyingi mbeleni!?
Wewe danganya hao lumumba wenzio unaona dar coach ni watu wa kukosa wateja
 
Shughuli za serikali zikiendeshwa kwa kutumia mapato halali ya serikali (kodi na tozo nyingine za kisheria) huondoa uwezekano wa upendeleo, serikali kuwekwa mfukoni mwa wafanyabiashara (hasa wale wasio na asili ya Afrika) na zaidi sana hueneza usawa miongoni mwa wananchi.
 
Hata kama ni bure lazima gari ulipeleke TAMESA walikague na wawavet kama wanaweza kutengeneza vyema magari ya serikali hata kama ni bure. The minister is right
Mdanganye rafiki yako,, lile toto lenye mtako likipeleka malalamiko kwa baba lazima mtu atumbuliwe!!
 
TAMESA my foot!hao ndiyo wale mawaziri wap...vu wanaodai kukosewa adabu,kwani hakujua kama yapo?na je huko mikoani yeye kama waziri amepeleka mangapi huko TAMESA?piga kazi dogo achana na hao wachovu..hata kama hujui kusoma hatuhitaji mwalimu dalisalama ,kwanza ukifika tu ubungo ni digrii tayari.

Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
 
Wahindi hawajawahi fanya crazy business ndg yangu. Lazima kuna kitu wametega
Sio kwa serikali hii,,,saivi ukiona mtu kafanya msaada huu ujue kna ma3
1.kapigwa biti
2.uzalendo tu
3.kujipendekeza
Hamna dili la kupga skuiz
 
Back
Top Bottom