Waziri Mbarawa asimamisha kazi watendaji 4 wa kampuni ya huduma za meli Mwanza

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,768
3,621
Waziri wa uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewasimamisha kazi watendaji 4 wa kampuni ya huduma za meli Mwanza kutokana na kufanya kazi kinyume na sheria za utumishi.

Walio simamishwa ni Kaimu meneja mkuu Fabian Mayenga,Mwanasheria Josephat Mshumbusi Kaimu Meneja Ununuzi Abdallah Rumila pamoja na meneja miradi Alex Mchaura.
 
Waende Mahakamani, maana hii serikali inaendeshwa kimajungu na falsafa ya "Hapa ni Papala tu"

Fukuza fukuza zingine hazina kichwa wala miguu.

Wananchi wajiandae kulipa fidai za maamuzi yasiyo na kichwa wala miguu
 
Jifunze kwanza tofauti ya kusimamishwa na kufukuzwa.

Maisha ya kufanya kazi katika mazingira ya kimazoea ameondoka nayo Rais Kikwete.

Mtapiga kelele sana katika awamu hii ya tano.

Hakuna nafasi tena kwa siasa za kutetea wezi, wala rushwa, mafisadi na wazembe.

Ukisikia wanapiga kelele...

Kama kuondoa ndani ya serikali wafanyakazi ambao ni wezi na wazembe inakuwa ni majungu, basi ninataka majungu yawe zaidi ya speed ya sasa.
 
Alex Mchauru nakumbuka ndo alikuwa meneja mkuu akafukuzwa na Mwakyembe kama sikosei, lini tena amekuwa meneja miradi?
 
Waziri wa uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewasimamisha kazi watendaji 4 wa kampuni ya huduma za meli Mwanza kutokana na kufanya kazi kinyume na sheria za utumishi.

Walio simamishwa ni Kaimu meneja mkuu Fabian Mayenga,Mwanasheria Josephat Mshumbusi Kaimu Meneja Ununuzi Abdallah Rumila pamoja na meneja miradi Alex Mchaura.
Imekuwa kama fasheni sasa kwa Mawaziri wetu!
 
Back
Top Bottom