chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,388
- 24,947
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameipa miezi miwili kampuni ya usafirishaji mizigo ya viwanja vya ndege Swissport kujiangalia kama inaweza kuendelea kufanya kazi au aifutie leseni.
Alisema taarifa za kampuni hiyo siyo nzuri na utendaji wake umekuwa ukilalamikiwa.
Alifafanua kuwa mbali ya kutoa huduma zisizoridhisha, kampuni hiyo pia imekuwa ikiibania kampuni mpya iitwayo Nas Dar Airco na kuisabbisha ishindwe kufanya kazi.
Alisema aliingia mkataba na kampuni hiyo mpya tangu Desemba mwaka jana, lakini hadi leo imeshindwa kufanya kazi kutokana na kampuni kuingia mikataba na kampuni zote zinazofanya kazi katika viwanja vya ndege.
Chanzo: Mwananchi Online