Baada ya Manji, sasa attention imehamia kwa Masha!
Kweli hivi vitakuwa vyombo vya habari? Ukigombana na mmiliki, wewe ndio unatengeneza habari!
Sipendi kutumia neno ujinga lakini kama ingekuwa anayesema maneno haya hajui kusoma na kuandika ningeweza kutumia maneno hayo lakini ukweli ni kwamba kuna juhudi za makusudi za kuthubutu kugeuza hoja nzito kuwa "ugomvi binafsi" na hiyo imekuwa ikitumika kama kinga na wahalifu wengi hapa nchini na kwa kweli wamefanikiwa sana kujilinda na kuokoka katika mikono ya dola na hata katika vyombo vingi vya habari.
Manji amefanikiwa kwa mtindo huu kwa kila uovu wake, anepenyeza rupia katika vyombo vya habari na kwa kuwa hawezi kupenyeza Thisday na KULIKONI wataandika na watu watasema, "si unaona, huo ni ugomvi wa Mengi na Manji".
Iko mifano mingi na hat hivi karibuni, Masha alitumia watu fulani kusema, matatizo yaliyotokea ni ugomvi wa wachaga dhidi ya Wasukuma, akatokea mtu akasema hata Masha mwenyewe si msukuma na miongoni mwa wanaoshangilia kuanguka kwake ni Wasukuma.
Wakati wa Mkapa magazeti ya RAI na Mtanzania na kipindi cha Jenerali On Monday kulikuwa na taarifa nyingi za kuikosoa serikali, baadhi zikiwa zinatoka hata bila ya Jenerali Ulimwengu kujua zinatoka wapi, lakini watu akiwamo mkapa na wafuasi wake wakawa wanasema ni "ugomvi wa Jenerali na Mkapa". HUU NI UJINGA AMA UPOTOSHAJI HATARI SANA.
Ni lazima tujadili HOJA kwa HOJA kwa kuangalia FACTS zilizopo. Ni UJINGA usio mfano kwa mfano Juma akigombana na Joni halafu Juma akiona Joni anaiba akawaita polisi, polisi waseme, "aaha Juma ana ugomvi na Joni".... huyo atakuwa polisi asiyejua kazi zake. Katika mafunzo ya upelelezi, moja ya watu muhimu wanaotoa taarifa za kweli za uhalifu ni watu wanaogombana kwa kuwa atatoa taarifa zote akijua mbaya wake atashughulikiwa.
Hizi hoja za kusema yaliyotokea kuhusu Masha yana uhusiano na ugomvi na Mengi, ama kama alivyoanza rafiki yangu Paparazimuwazi kwamba "Mengi amempata Masha" si sahihi kabisa tunapotoka na tutajikuta anaibuka Mramba anasema, "Hosea na Feleshi ni Wasukuma wana chuki na Wachaga na Wapare na sasa wanamuacha msukuma mwenzao Chenge"
Hapa Masha kaingilia zabuni na yeye mwenyewe anakiri kwamba hana mamlaka ya kuingilia lakini analazimika kutetea "maslahi ya umma". MAsha anaitetea kampuni ambayo imeenguliwa. Walioshiriki zabuni hiyo wote wanasema hawajajulishwa kampuni zilizoenguliwa na hivyo kushangaa kampuni anayoitetea Masha ilijuaje kwamba wameenguliwa kama si yeye aliyewaibia siri ya zabuni?
Kama alivyosema Dk. Slaa, taratibu za zabuni kwa sheria ya manunuzi zinaelekeza taratibu za kampuni kufuata isiporidhika na matokeo na Waziri hatajwi katika taratibu hizo, KUNA NINI hata Masha aingilie tena akiwa mwanasheria aliyebobea na ambaye miaka ya nyuma aliitetea kampuni nyingine iliyoishitaki serikali baada ya kuenguliwa katika zabuni ya vitambulisho na leo ni Masha huyo ambaye yuko Wizarani akiwa upande wa serikali.