Una maana kati ya watu milioni 40 hakuna angalau watu 4,000 wenye uwezo wa kuongoza? Au wapo lakini hawapati nafasi? Na kama hawapati nafasi ni kwa nini hawapati nafasi?
MMMM twayib unajua humu ndani wapo wengine hawana tofauti na hao tunaowasema.sawa na nyani kucheka mkia wa mwenzane.Kweli Hapa JF we dare talk openly... Hata kama ni off point au pumba! Vidole, meno na meno ndio vinampa mtu merits za kuwa kiongozi bora? La Haula Wa Laku'wata!!
Lets focus on qualitites, kama anazo au hana
Tatizo la uongozi Tanzania haliko kwenye umri, elimu, sura, au kuvuta sigara. Liko kwenye uwezo.
Wakuu,
Nifahamisheni Ngeleja ana matatizo gani? Najua Masha kweli kazi imemshinda lakini Ngeleja mbona kama anajitahidi japo wizara yenyewe imejaa mizengwe.
Inatakiwa waziri apewe madaraka yote ya kuja na vision mpya juu ya energy. Huo umeme wa mafuta na maji pekee hautatutosha huko tunakoenda na itakuwa gharama kubwa.
Kuna haja ya kuwa na miradi midogo midogo ya umeme ya kiwilaya badala ya miradi mikubwa mikubwa ambayo kukiwa na tatizo nchi nzima inatikisika.
Kuongezea tu, Ngeleja na Wasira ni watu wa Rostam Aziz.Ngeleja wizara imemshinda hiyo. Mpaka hii leo hajafanya chochote kuandika mikataba mipya ya madini ili kuhakikisha Watanzania tunanufaika. Kiwira, mpaka leo anapiga kalenda tu badala ya kutwambia nini kilichojiri katika deal ya Mkapa kujiuzia mgodi huo kwa bei poa. Pia usisahau alishatoa ushauri wa kutaka TANESCO wanunue mitambo ya Richmond?Dowans kwa mabilioni, kama siyo wabunge kuja juu basi deal lingine la kifisadi lingepita bila matatizo.
Tatizo la uongozi Tanzania haliko kwenye umri, elimu, sura, au kuvuta sigara. Liko kwenye uwezo.
Mkuu unaweza kuwa na watu wenye uwezo,Qualifications kwenye uongozi/organisation fulani but if those people are not MANAGED CORRECTLY they will end-up being Liabilities tu!!
Una maana kati ya watu milioni 40 hakuna angalau watu 4,000 wenye uwezo wa kuongoza? Au wapo lakini hawapati nafasi? Na kama hawapati nafasi ni kwa nini hawapati nafasi?
hawana hela hawako kwenye system, watakutana wapi na kikwete wako huko olidonyo, na wengi wao sio sisiemu
Nimesikia kuwa sijui kama si kweli kuwa Slimu Ahmed atagombea Uraisi kwa tiketi ya Chadema ,naona Chadema kinakuwa Chama cha Waarabu.