Waziri Makamba awasimamisha kazi vigogo watatu wa NEMC

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA-NEMC

Katika kikao kilichoitishwa na Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira tarehe 24 January 2016, kuhusu kuimarisha utendaji ndani ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC maamuzi yaliyofikiwa ni kama ifuatavyo:

1. Kuhusu suala la kiwanda cha kusindika minofu ya punda mkoani Dodoma, imegundulika kulikuwa na ukiukwaji mkubwa, wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa NEMC walioshughulika na kiwanda hicho. Hivyo, Mhe. Makamba ameagiza watumishi wa NEMC wafuatao wasimamishwe kazi mara moja:

a. Dkt. Eladius Makene -Afisa Mazingira Mwandamizi,
b. Wakili Heche Suguta Manchare - Mwanasheria Daraja la II
c. Mhandisi Boniface Benedict Kyaruzi, Afisa Mazingira.Hatua nyingine za kinidhamu na kisheria zitafuatia

2. Vilevile, imebainika kwamba usimamizi wa watumishi wa NEMC siyo makini na thabiti na kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza.

Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Mhandisi Bonaventura Baya apewe barua ya onyo kali na la mwisho kwa udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa Baraza.

3. NEMC kama chombo muhimu nchini kilichopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira inatarajiwa kazi zake zifanyike kwa ufanisi wa kiwango cha juu kulingana na majukumu yaliyoko kwenye Sheria.

Hivyo, kwa mapungufu yanayojitokeza Mhe. Makamba, ndani ya wiki moja ataunda jopo la wataalamu wasiozidi watano ili kutathmini utendaji wa NEMC na changamoto mbali mbali katika usimamizi wa hifadhi ya mazingira na kuishauri Serikali ipasavyo.

4. Ili kuimarisha ufanisi na udhibiti wa utendaji wa NEMC, ndani ya wiki moja litatolewa Tangazo litakalokuwa na mambo yafuatayo:

Anwani ya barua pepe (email), Nukushi (fax), Namba ya simu, Namba ya Whatsapp ili mtu yeyote mwenye malalamiko au aliyewahi kuombwa rushwa chochote na watumishi wa NEMC ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yao atoe taarifa mara moja ili uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe.

5. Kutokana na mapungufu yanayojitokeza katika utekelezaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ndani ya wiki moja, NEMC ipitie upya orodha ya wataalamu na taasisi elekezi zilizosajiliwa na kufuta wataalamu na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao likiwemo suala la kuwasilisha taarifa zilizo chini ya viwango, kuchelewesha kazi za wateja wao na kutowasiliana na wateja wao kuhusu hatua za utekelezaji wa maombi yao.

6. Ndani ya wiki tatu uitishwe mkutano wa dharura wa Bodi ya NEMC kujadili na kufanya maamuzi juu ya changamoto za utendaji katika Baraza.

IMETOLEWA NA
IDARA YA MAZINGIRA,
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
TAREHE 24.01.2016​
 
NEMC ilipaswa kufutwa kabisa, tumepeleka malalamiko mengi kuhusu uchafuzi wa mto uliopo mjini Morogoro ambao unachafuliwa na viwanda na pia unaingiza maji yenye sumu mto Ruvu, lakini ni kama vile wao TOR zao ni kushughulikia mambo ya nchi za nje
 
Vizuri. Ila ikumbukwe kuwa wengine ni wazuri isipokuwa uongozi uliopita ulitoa kila nafasi ya watumishi kuwa mafisadi....nani hatachukua nafasi hiyo? It is a human nature!
 
Taasisi za umma na vitengo/idara za serikali zilizo na wajibu wa kusimamia utekelezaji wa sheria, viongozi wake ni wala rushwa waliokubuhu ili sheria zisitekelezwe na waharifu/mafisadi. Zote zitizamwe na majipu yakamuliwe.

CHAMBUA CHUBGUA AMUA CHUKUA HATUA
 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, amewasimamisha kazi maofisa watatu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Wanatuhumiwa kukiuka miiko ya kazi katika kusimamia kiwanda cha kusindika minofu ya punda kilichopo mkoani Dodoma.
Maofisa hao ni Ofisa Mazingira Mwandamizi Dk Eladius Makene, Mwanasheria Daraja la II Wakili Heche Suguta Manchare, na Ofisa Mazingira, Boniface Benedict Kyaruzi.
Aidha, Waziri huyo ameagiza Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo, Bonaventura Baya, aandikiwe barua ya onyo kali na la mwisho kwa tuhuma ya udhaifu wa usimamizi wa watumishi wa NEMC, hivyo kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza hilo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, January alithibitisha kuchukua hatua hiyo dhidi ya maofisa hao wa NEMC.
Taarifa ambayo gazeti hili linayo kutoka Ofisi ya Wizara hiyo ya Muungano na Mazingira, ilibainisha kuwa uamuzi wa waziri huyo ulitolewa baada ya kikao kilichofanyika Januari 24, mwaka huu kuhusu kuimarisha utendaji ndani ya Baraza hilo.
Kuhusu kiwanda cha kusindika minofu ya punda mkoani Dodoma, taarifa hiyo ilisema imegundulika kuwapo kwa ukiukwaji mkubwa, wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa NEMC walioshughulika na kiwanda hicho.
Aidha, taarifa hiyo ilisema “Imebainika kwamba usimamizi wa watumishi wa NEMC siyo makini na thabiti na kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza. Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Mhandisi Bonaventura Baya apewe barua ya onyo kali na la mwisho kwa udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa Baraza”.
Ilieleza kuwa NEMC kama chombo muhimu nchini, kilichopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, inatarajiwa kazi zake zifanyike kwa ufanisi wa kiwango cha juu kulingana na majukumu yaliyoko kwenye sheria.
Waziri huyo alisema kutokana na mapungufu yanayojitokeza, ndani ya wiki moja ataunda jopo la wataalamu wasiozidi watano ili kutathmini utendaji wa baraza hilo na changamoto mbalimbali katika usimamizi wa hifadhi ya mazingira na kuishauri serikali ipasavyo.
January alisema ili kuimarisha ufanisi na udhibiti wa utendaji wa NEMC, ndani ya wiki moja pia litatolewa tangazo litakalokuwa na anwani ya barua pepe, nukushi, namba ya simu, namba ya whatsapp ili mtu yeyote mwenye malalamiko au aliyewahi kuombwa rushwa na watumishi wa NEMC, ama kufanyiwa jambo kinyume na maadili ya kazi yao, atoe taarifa mara moja ili uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe.
Aidha, alisema kutokana na mapungufu yanayojitokeza katika utekelezaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ndani ya wiki moja NEMC ipitie upya orodha ya wataalamu na taasisi elekezi, zilizosajiliwa na kufuta wataalamu na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao.
Alitaja baadhi ya ukiukwaji unaofanywa na baadhi ya taasisi hizo kuwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa zilizo chini ya viwango, kuchelewesha kazi za wateja wao na kutowasiliana na wateja wao kuhusu hatua za utekelezaji wa maombi yao.
Pia, January alilitaka baraza hilo kuitisha mkutano wa dharura wa Bodi ya NEMC ndani ya wiki tatu, kujadili na kufanya maamuzi juu ya changamoto za utendaji katika baraza hilo.
 
Huu ndo ulikuwa mwanzo wa makosa, yakafuata mengine na mengine baadaye sasa, CHALI!
 
Back
Top Bottom