JIULIZE KWANZA
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 2,569
- 499
Anaongea point sana kama itafanyika kama anavoongea, nimempenda japo ni magamba naona ni bora zaidi ya Pinda, kwa mnaoangalia TBC Kasema ndege ya jeshi liyochukua wanyama ilikuwa na kibali cha diplomatic haikustahili kufanya uhalifu na anajirizisha na ushahidi kabla hajaituhumu nchii nyingine kufanya uhalifu kumbe kuna watu wamebariki document halali wakajikuta wanaishia kuomba radhi, ila amemsimamisha kazi mkugunzi flani na watu wawili chini yake sijamsikia jina vizuri ntawajuza zaidi huku umeme uko
..hata mimi niliuliza waziri Membe yuko wapi kuhakikisha wanyama hao wanarudishwa Tanzania?
..kama alikuwa na usongo wa kurudisha pesa za BAE basi lazima awe na usongo hawa wanyama warudishwe.
..ninavyoelewa mimi mizigo ya watu wenye hadhi ya Diplomat huwa haipekuliwi.
..pamoja na hayo kuna exception kwamba ikiwa kuna uhakika wa tendo la uhalifu kuwa limefanyika basi mzigo huo lazima upekuliwe.
..wa-Nigeria walijaribu kumteka nyara waziri wa zamani wa mafuta akiitwa Ummaru Diko na kumtia kwenye sanduku lenye hadhi ya mzigo wa kidiplomasia. Scotland Yard walisisitiza mzigo huo ufunguliwe na wakaweza kumuokoa Diko asifike mikononi mwa Gen.Muhammad Buhari.
..katika tukio la uwanja wa ndege wa Kilimanjaro mzigo ulikuwa ni wanyama walio hai wanaonekana kwa macho sasa sielewi kwanini hawakuzuiliwa.
Kibali cha kidiplomasia cha kuchukua hadi Twiga nembo ya NCHI? Kweli CCM ni sikio la kufa lisilosikia dawa............... Hata hao waliosimamishwa ni zuga tu, maana km walikua na kibali na kawasimamisha kwa kosa linaloendana na hiyo kashfa.... SWALI kwanini wafukuzwe? Atupe facts zaidi.... Je, walishiriki/ waliruhusu wanyama wachukuliwe wengi zaidi, walipewa mlungula? Kikubwa ushiriki wao ktk hiyo kashfa watanzania tunataka kuijua kabla ya hayo maamuzi aliyoyachukua kwanza.
tupo pamoja

Ningeelewa kama ungesema Katibu mkuu maliasili kamsimamisha Mkurugenzi. Km ndiye disciplinary authority na siyo Waziri.
Kama Waziri kasema yeye ndiye kamsimamisha kazi kalidanganya Bunge.
Hii charnel kuhusu uchunguzi kuhusiana na utoroshaji wa wanyama hata aliyekua waziri wa maliasili na utalii Shansa Mwangunga naye achunguzwe! Hii charnel ni ndefu.
Nimeipenda picha ya Thomas sankara
Huu ni ujanja tu kama wa TANESCO. Kwa maana hiyo Maige anataka kutuambia kwamba alikuwa hajui kuhusu wanyama wetu kunyakuliwa na kwa maana hiyo amejua jana na kuamua kumsimamisha Mkurugenzi ili aanze uchunguzi? Hata kama ndege zilikuwa na vibali vya kidiplomasia na wanyama wetu toka huko mbugani walikuwa na vibali vya kidiplomasia? Huyu Mkurugenzi anatumiwa tu kama Bangusilo!!
Ni ajabu na kweli kwamba Maige alikuwa hajui!! Mkurugenzi atatakaswa tu baada ya budget kupita au huenda amesema tu bungeni na hajamwandikia barua.