Waziri Maige amsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wanyamapori kupisha Uchunguzi!

Hongera kwa hiyo picha ya Master Sgt Thomas Sankara, mkuu. Unanikumbusha mbali.Back to the issue, jambo hili la Maige kumsimamisha Mkurugenzi ni maigizo tu kwani kiutawala Maige ni Waziri, a mere politician, Hana mamlaka ya kumteua au kubatilisha uteuzi achilia mbali kumsimamisha MKURUGENZI YEYOTE KATIKA WIZARA NZIMA. HE IS NOT THE APPOINTING AUTHORITY. Tunayo mifano mingi tuuuu hapa hapa Danganyika ya waliowahi kujidai eti wanayo mamlaka ya kusimamisha watendaji lakini Amri zao Ziliishia
kuwa nguzo za mipapai! Mkumbukeni Lowassa na issue ya maghorofa feki/fake chang'ombe, Diallo Anthony Ng'wandu akiwa hapo hapo Maliasili ya Yule jamaa sijui yuko wapi siku hizi. Wenye mamlaka hula ni Katibu Mkuu Luhanjo kwa mjibui wa ofisi yake na jakayaa mrishoo kikwete kwa mjibu wa ofisi yake

Mkuu hapo kwenye wekundu usije ukawa unachanganya na Master Sgt. Samwel Doe!! Turejee. Umenikumbusha habari za Tsere na Diallo. Diallo Alimsimamisha lakini Tsere akasema mimi na wewe ni wateuliwa wa Rais na huna mamlaka ya kunitimua. Tsere alibaki ila Diallo akang'oka. Nashangaa wabunge wetu walikuwa wakishangilia wakati Maige anasema amemsimamisha kazi Mkurugenzi. Hivi wabunge wetu hawajui nani ana mamlaka ya kumsimamisha mkurugenzi hadi washangilie uongo wa waziri? Pole pole ndio mwendo na hakika tutafika tu.

Wanyama hai 116 wanaibwa lakini waziri hachukui hatua za kinidhamu hadi bunge limkabe koo. Kumbe na Mkurugenzi alikuwepo Bungeni. Hii inaonyesha kwamba hana taarifa ya kusimamishwa kwake!!

Huyo mkurugenzi ni kondoo wa kafara tu wapo Vigogo wanaohusika. Wamemsimasha Mkurugenzi ili kuficha ukweli wa jambo zima! Hivi kitengo chetu cha Usalama wa Taifa Kimefia wapi? mbona kipindi cha miaka ya themanini kilikua maarufu sana Duniani pote? Nijuavyo mimi Airport zote watu wa usalama huwa wapo,kwanini na wao wasiwajibishwe?
Nchi yetu imekwisha! Hao ni wanyama ambao wanaonekana kwa macho,je visivyoonekana inakuaje?

Mkuu huyo ni bangusilo.

Anaongea point sana kama itafanyika kama anavoongea, nimempenda japo ni magamba naona ni bora zaidi ya Pinda, kwa mnaoangalia TBC Kasema ndege ya jeshi liyochukua wanyama ilikuwa na kibali cha diplomatic haikustahili kufanya uhalifu na anajirizisha na ushahidi kabla hajaituhumu nchii nyingine kufanya uhalifu kumbe kuna watu wamebariki document halali wakajikuta wanaishia kuomba radhi, ila amemsimamisha kazi mkugunzi flani na watu wawili chini yake sijamsikia jina vizuri ntawajuza zaidi huku umeme uko

Navyofahamu hakuna kibali cha ndege cha kidiplomasia. Kibali cha ndege kutua ni kimoja tu na kinatolewa na NGOME. Aidha aliyenukuu amekosea au Waziri muwasilishaji amejikwaa ulimi. Anayehusika na ulinzi wa anga la nchi na kuruhusu ndege yoyote kuingia nchini na kutua ikiwa ni pamoja na kutoa masafa (route) ni NGOME.

Jamani leo ume2 ume2tenda cjacheck bunge
Bt Maige anatakiwa akaze moyo kwenye skendo zote esp msekwa
Mwita ckuon leo?

Ningeelewa kama ungesema Katibu mkuu maliasili kamsimamisha Mkurugenzi. Km ndiye disciplinary authority na siyo Waziri.
Kama Waziri kasema yeye ndiye kamsimamisha kazi kalidanganya Bunge.

Hata mimi nilijiuliza hivyo mkuu,isije jamaa kakurupuka kwa kuliridhisha bunge
Kama Pinda hakuwa na mamlaka ya kumwajibisha Jairo itakuwaje kwa Maige kumsimamisha mkurugenzi wake?

Ule ni usanii mtupu ili kuwazubaisha CDM!
Kwa mfumo wa utawala TZ. Maige alijua wizi huo wa wanyama kabla hata bei haijajadiliwa isipokuwa huenda kuna mtu mwenye uchungu na mali za taifa hili aliliona hilo dili na kuamanua kulilikisha. ask yourself this question:-
1.Kwa nini atangaze leo bungeni kumsimamisha ilhali tukio lina miezi kazaa?
2. Diallo alimfukuza kazi mkurugenzi wa idara hiyo hiyo, badala yake Diallo ndo akaondolewa halafu yule mkurugenzi akarudishwa, why?

Mkurugenzi na Ma naibu wake wanateuliwa na rais. Waziri hawezi kuwasimamisha labda mmesikia vibaya. Inawezekana amesimamisha afisa wanyamapori wilaya, afisa maliasili mkoa au kamanda wa kikosi dhidi ya ujangili (APU)...

Tarimo alishatimuliwa zamani na kuteuliwa mwingine...

hawa watendaji wetu wamezidi usanii, ingekuwa nchi nyingine ambako huwa wana maamuzi magumu huyu waziri angekuwa ameshaachia ngazi na kupisha wengine, nchi kama za ulaya hata kuiba/ama kuvusha mbwa ni kazi kubwa sana na pengine ni jambo lisilowezekana, lakini Tanzania hakuna anayejali nini tutawaachia kizazi kijacho nao wajivunie kuwa watanzania.

Naendelea kuamini kuwa sisi watanzania tuna matatizo ya kifikira na hasa hao wawakilishi wetu (yaani WABUNGE). Hivi hawa wabunge wanaishi nchi gani? Mbona tumejua kashfa hii miezi kadhaa iliyopita na iweje huyo mkurugenzi asimamishwe sasa baada ya kelele za wabunge?

Wabunge wanadanganywa kama watoto? Kama kweli huyo mkurugenzi alitakiwa kusimamishwa ili achunguzwe hilo ni kosa kubwa la kumfanya waziri ajiuzulu manake muda wote huo alikuwa hajui nini cha kufanya. Bila aibu eti wengine wanampigia waziri makofi kwa kusema anamsimamisha mkurugenzi, kweli????

TAFAKARI

Mkurugenzi wa wanyama pori si kateuliwa mwezi wa 3 au wa 4 hapo jamani? Mbona wanambebesha zigo lisilo la kwake??? Au kuna mwingine??

Mkurugenzi wa wanyama pori si kateuliwa mwezi wa 3 au wa 4 hapo jamani? Mbona wanambebesha zigo lisilo la kwake??? Au kuna mwingine??

Kabla ya hapo alikuwa Deputy Director Utilization hivyo yeye ndie alikuwa msimamizi wa kitengo akimsaidia Erasmus. Kwa hiyo hoja iliyopo ni kwamba alipandishwa cheo badala ya kuwajibishwa!

ina maana sasa ivi imekuwa bajeti ikisua kupitishwa lazima m2 asimamishwe kama kafara kwasababu walianza na jairo ila mpaka sasa a2japata majibu kuhusu uchunguzi hua na sasa ni zamu ya wanyama pori

usanii kweli ni mgumu kuisha. Maige eti anamsimamisha mkurugenzi kuanzia leo! kwamba hakujua kuna wizi huu siku zote? halafu anasahau kuwa hata Diallo aliwahi kumsimamisha mkurugenzi wa wanyamapori akaonekana kituko. Usanii huu jamani, duh!

waziri anatuzuga

kajua juzi kuwa wanyama wanaibiwa?????????????? mbona hakumsimamisha kitambo??????

waziri ana mamlaka ya kumsimamisha mkurugenzi????????

Kwa huu utawala wa Jk, inabidi hata m/kiti wa kijiji ajivike mamlaka ya kumsimamisha DC maana akimtegemea rais kuchukua hatua tutajikuta hakuna urithi tunaowaachia vizazi vyetu vijavyo.

Mkurugenzi wa wanyama pori si kateuliwa mwezi wa 3 au wa 4 hapo jamani? Mbona wanambebesha zigo lisilo la kwake??? Au kuna mwingine??

Hao wanaonewa tu! Hata wabunge wetu ni vilaza sana, yani ndege ilikuwa na kibali cha ki-diplomasia kwa ajili ya kuja kufanya nini hapa Tanzania? kabla ya yote mbona sijasikia wakivunja uhusiano na hiyo nchni kwa kutumia vibaya kibali cha kidiplomasia?

Mbona harudishi twiga wanachunguza nini wakati twiga hawajarudishwa? wanachunguza nini kwa kusimamisha Mkurugenzi wa wanyamapori wakati siyo yeye anayetoa vibali vya kidiplomasia?

Mkuu hapo kwenye wekundu usije ukawa unachanganya na Master Sgt. Samwel Doe!! Turejee. Umenikumbusha habari za Tsere na Diallo. Diallo Alimsimamisha lakini Tsere akasema mimi na wewe ni wateuliwa wa Rais na huna mamlaka ya kunitimua. Tsere alibaki ila Diallo akang'oka. Nashangaa wabunge wetu walikuwa wakishangilia wakati Maige anasema amemsimamisha kazi Mkurugenzi. Hivi wabunge wetu hawajui nani ana mamlaka ya kumsimamisha mkurugenzi hadi washangilie uongo wa waziri? Pole pole ndio mwendo na hakika tutafika tu.Kweli mkuu hapo gololi zimepandana baina ya Master Sgt Samwel Doe, na mikasa yake na mzalendo Capt Thomas Sankara na Uzalendo wake. Africa, Africa! Naililia Africa.Hebu tulejee sakata Diallo na Tsere, sote tunatakiwa tukumbuke kuwa ile vita haikuwa kwa manufaa ya wadanganyika bali familia na magenge Yao. Kwani mara hii mmesahau Diallo alivyojimilikisha vitalu via misitu ya kukata mbao kule Mafinga? Wadogo zake wengine wakawekwa kwenye fishing industry mwanza kukusanya mafungu ya brother? Ya Tsere na wazungu wa hunting blocks naamini hayajawatoka kwenye memory zenu. Historia huwa inatabia ya kujirudia kwa wastani wa Kila baada ya miaka 15, lakini hapa kwetu inaonekana tumeasi natural phenomena maana velocity yetu ni kubwa mno. Maana history inajirudia Kila baada ya dakika tano. Naomba Mwongozo which laws of motion are we applying in this country. Kuna ile inayosema whatever goes high must come down na ile ingine ya Aerodynamics! Ninasubiri Mwongozo

Back
Top Bottom