Waziri Maige amsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wanyamapori kupisha Uchunguzi!

JIULIZE KWANZA

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
2,569
499
Anaongea point sana kama itafanyika kama anavoongea, nimempenda japo ni magamba naona ni bora zaidi ya Pinda, kwa mnaoangalia TBC Kasema ndege ya jeshi liyochukua wanyama ilikuwa na kibali cha diplomatic haikustahili kufanya uhalifu na anajirizisha na ushahidi kabla hajaituhumu nchii nyingine kufanya uhalifu kumbe kuna watu wamebariki document halali wakajikuta wanaishia kuomba radhi, ila amemsimamisha kazi mkugunzi flani na watu wawili chini yake sijamsikia jina vizuri ntawajuza zaidi huku umeme uko

Katika majumuisho yake Waziri Maihe amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Wanyamapori kupisha uchunguzi wa sakata la wanyama kusafirishwa hai!!

Ni sawa ila wasiwasi wangu hii isije ikawa ni njia tu ya kulainisha wabunge wapitishe bajeti ya wizara, pili maamuzi haya yanayochukuliwa ghafla baada tu ya wabunge kusema yaangaliwe. Ni ajabu waziri na raisi wake wanamteua mtu kipumbavu halafu wakikemewa wanamsimamisha! Lazima na wao wachukuliwe hatua kwa maamuzi ya kijinga!!

Safari inaendelea!

Kwani Maige ndo anajua leo hilo sakata la kusafirishwa Wanyama! Kwanini hakuwasimamisha hao watu kabla ya leo! Hii inaonyesha kama si wabunge kutishia kuikwamisha Bajeti ya Wizara yake, asingesimamishwa mtu.

Lakini bado tusisherehekee ushindi, kwani hata Ngereja aliwazuga hivi hivi Wabunge kwa kutuletea umeme kwa muda wa wiki mbili, lakini bajeti yake ilipopita tu, sasa Mgao ndo mara mbili ya ule wa mwanzo. (Waulize Mwanza).

Maana mkishangaa sana msije mkaanguka presha siku mtakaposikia Jairo mtu huru hana tatizo lolote.

Hii ndiyo serikali ya Magamba

Anaongea point sana kama itafanyika kama anavoongea, nimempenda japo ni magamba naona ni bora zaidi ya Pinda, kwa mnaoangalia TBC Kasema ndege ya jeshi liyochukua wanyama ilikuwa na kibali cha diplomatic haikustahili kufanya uhalifu na anajirizisha na ushahidi kabla hajaituhumu nchii nyingine kufanya uhalifu kumbe kuna watu wamebariki document halali wakajikuta wanaishia kuomba radhi, ila amemsimamisha kazi mkugunzi flani na watu wawili chini yake sijamsikia jina vizuri ntawajuza zaidi huku umeme uko

Kibali cha kidiplomasia cha kuchukua hadi Twiga nembo ya NCHI? Kweli CCM ni sikio la kufa lisilosikia dawa............... Hata hao waliosimamishwa ni zuga tu, maana km walikua na kibali na kawasimamisha kwa kosa linaloendana na hiyo kashfa.... SWALI kwanini wafukuzwe? Atupe facts zaidi.... Je, walishiriki/ waliruhusu wanyama wachukuliwe wengi zaidi, walipewa mlungula? Kikubwa ushiriki wao ktk hiyo kashfa watanzania tunataka kuijua kabla ya hayo maamuzi aliyoyachukua kwanza.

..hata mimi niliuliza waziri Membe yuko wapi kuhakikisha wanyama hao wanarudishwa Tanzania?

..kama alikuwa na usongo wa kurudisha pesa za BAE basi lazima awe na usongo hawa wanyama warudishwe.

..ninavyoelewa mimi mizigo ya watu wenye hadhi ya Diplomat huwa haipekuliwi.

..pamoja na hayo kuna exception kwamba ikiwa kuna uhakika wa tendo la uhalifu kuwa limefanyika basi mzigo huo lazima upekuliwe.

..wa-Nigeria walijaribu kumteka nyara waziri wa zamani wa mafuta akiitwa Ummaru Diko na kumtia kwenye sanduku lenye hadhi ya mzigo wa kidiplomasia. Scotland Yard walisisitiza mzigo huo ufunguliwe na wakaweza kumuokoa Diko asifike mikononi mwa Gen.Muhammad Buhari.

..katika tukio la uwanja wa ndege wa Kilimanjaro mzigo ulikuwa ni wanyama walio hai wanaonekana kwa macho sasa sielewi kwanini hawakuzuiliwa.

Hapa hata mimi nahisi kama ni propaganda ili bajeti ipite ila ki saikolojia jamaa alikuwa anaongea kwa hisia za uzuni kiasi kwamba ananipa ushawishi kwamba he will do something...ila tatizo ukiongea uongo mara moja ukijaongea ukweli mara elfu moja watu watajua ni uongo hiyo ndio tabia ya viongozi wetu

Hii charnel kuhusu uchunguzi kuhusiana na utoroshaji wa wanyama hata aliyekua waziri wa maliasili na utalii Shansa Mwangunga naye achunguzwe! Hii charnel ni ndefu.

Hapo kwenye red ndio hajajibu
..hata mimi niliuliza waziri Membe yuko wapi kuhakikisha wanyama hao wanarudishwa Tanzania?

..kama alikuwa na usongo wa kurudisha pesa za BAE basi lazima awe na usongo hawa wanyama warudishwe.

..ninavyoelewa mimi mizigo ya watu wenye hadhi ya Diplomat huwa haipekuliwi.

..pamoja na hayo kuna exception kwamba ikiwa kuna uhakika wa tendo la uhalifu kuwa limefanyika basi mzigo huo lazima upekuliwe.

..wa-Nigeria walijaribu kumteka nyara waziri wa zamani wa mafuta akiitwa Ummaru Diko na kumtia kwenye sanduku lenye hadhi ya mzigo wa kidiplomasia. Scotland Yard walisisitiza mzigo huo ufunguliwe na wakaweza kumuokoa Diko asifike mikononi mwa Gen.Muhammad Buhari.

..katika tukio la uwanja wa ndege wa Kilimanjaro mzigo ulikuwa ni wanyama walio hai wanaonekana kwa macho sasa sielewi kwanini hawakuzuiliwa.

Kibali cha kidiplomasia cha kuchukua hadi Twiga nembo ya NCHI? Kweli CCM ni sikio la kufa lisilosikia dawa............... Hata hao waliosimamishwa ni zuga tu, maana km walikua na kibali na kawasimamisha kwa kosa linaloendana na hiyo kashfa.... SWALI kwanini wafukuzwe? Atupe facts zaidi.... Je, walishiriki/ waliruhusu wanyama wachukuliwe wengi zaidi, walipewa mlungula? Kikubwa ushiriki wao ktk hiyo kashfa watanzania tunataka kuijua kabla ya hayo maamuzi aliyoyachukua kwanza.

Ningeelewa kama ungesema Katibu mkuu maliasili kamsimamisha Mkurugenzi. Km ndiye disciplinary authority na siyo Waziri.
Kama Waziri kasema yeye ndiye kamsimamisha kazi kalidanganya Bunge.

Huu ni ujanja tu kama wa TANESCO. Kwa maana hiyo Maige anataka kutuambia kwamba alikuwa hajui kuhusu wanyama wetu kunyakuliwa na kwa maana hiyo amejua jana na kuamua kumsimamisha Mkurugenzi ili aanze uchunguzi? Hata kama ndege zilikuwa na vibali vya kidiplomasia na wanyama wetu toka huko mbugani walikuwa na vibali vya kidiplomasia? Huyu Mkurugenzi anatumiwa tu kama Bangusilo!!

Ni ajabu na kweli kwamba Maige alikuwa hajui!! Mkurugenzi atatakaswa tu baada ya budget kupita au huenda amesema tu bungeni na hajamwandikia barua.

Ni sawa na Katibu mkuu wa wizara anapodai hajui kama wahasibu na wachumi wa wizara yake wanachukua rushwa ili idara za wizara zao zipangiwe bajeti kubwa.

Only in Tanzania!

Kwa hakika kabisa Maige angekuwa muungwana angeachia ngazi. Hii kashfa ni kubwa mno kuuhimili. Hakuna maelezo ya maana hapa wakati watu tuna uchungu na twiga wetu.

waziri anatuzuga
kajua juzi kuwa wanyama wanaibiwa?????????????? mbona hakumsimamisha kitambo??????
waziri ana mamlaka ya kumsimamisha mkurugenzi????????

• Thanks
Reactions: FJM
Anazuga tu ili bajeti ipite mambo yaende mbele.Maana siku zote yuko wapi!Nimemsikia eti atamuunda tume ya kumchunguza msekwa juu ua tuhuma za ngorongoro.Zote hizo ni propaganda za kisiasa na zitakuwa zimepangwa ili kuondoa aibu ya bajeti kukwama.

Huu ni ujanja tu kama wa TANESCO. Kwa maana hiyo Maige anataka kutuambia kwamba alikuwa hajui kuhusu wanyama wetu kunyakuliwa na kwa maana hiyo amejua jana na kuamua kumsimamisha Mkurugenzi ili aanze uchunguzi? Hata kama ndege zilikuwa na vibali vya kidiplomasia na wanyama wetu toka huko mbugani walikuwa na vibali vya kidiplomasia? Huyu Mkurugenzi anatumiwa tu kama Bangusilo!!

Ni ajabu na kweli kwamba Maige alikuwa hajui!! Mkurugenzi atatakaswa tu baada ya budget kupita au huenda amesema tu bungeni na hajamwandikia barua.

Ilishakuwa kawaida kudaganya mhimili mkubwa kama bunge Tanzania. Hakuna tena wa kumnyoshea kidole mwenzake zaidi ya wabunge wa upinzani.

..hata mimi niliuliza waziri Membe yuko wapi kuhakikisha wanyama hao wanarudishwa Tanzania?

..kama alikuwa na usongo wa kurudisha pesa za BAE basi lazima awe na usongo hawa wanyama warudishwe.

..ninavyoelewa mimi mizigo ya watu wenye hadhi ya Diplomat huwa haipekuliwi.

..pamoja na hayo kuna exception kwamba ikiwa kuna uhakika wa tendo la uhalifu kuwa limefanyika basi mzigo huo lazima upekuliwe.

..wa-Nigeria walijaribu kumteka nyara waziri wa zamani wa mafuta akiitwa Ummaru Diko na kumtia kwenye sanduku lenye hadhi ya mzigo wa kidiplomasia. Scotland Yard walisisitiza mzigo huo ufunguliwe na wakaweza kumuokoa Diko asifike mikononi mwa Gen.Muhammad Buhari.

..katika tukio la uwanja wa ndege wa Kilimanjaro mzigo ulikuwa ni wanyama walio hai wanaonekana kwa macho sasa sielewi kwanini hawakuzuiliwa.

Ukiona hivyo mkuu ata mpangaji wetu wa magogoni alihusika

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom