Waziri Maghembe unachekesha-ongea huku ukijua wewe ni waziri

luckman

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,211
371
Katika pitapita yangu, jana nilibahatika kumuona mheshimiwa maghembe akizungumzia suala la sukari, akapiga mkwara kweli sukari isiuzwe nje ya mipaka ya nchi na akatoa namba yake ya simu with confidence yani ka hajui eti anayejua wanaotoa sukari nje wampigie kwa namba aliyoitoa, kali kuliko zote niliposema kweli mawaziri tunao na ni kweli hawazingatii sheria aliposema, ATAKAYERIPOTIWA KUFANYA VIVO HATA KAMA HAWANA USHAIDI WATAMFUTIA LESENI'' nikagundua kuwa mambo mengi yanafanyika na kuamuliwa hata ka hakuna ushaidi make mtu kutokeza na kudhubutu kusema hivyo hali nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria na katiba..pole sana mzee na nadhani ni uzee, sheria tanzania tunazo 415 na naomba zizingatiwe, siwatetei wanaouza sukari nje ila nashangaa kusikia waziri yaani public figure kama wewe unasema hata kama hauna ushaidi utafuta lesseni, inanipa wasiwasi kidogo na ubabe huu, na inanipa mwanga kuwa haya ndio mabavu yanayotumika kukandamiza walio wengi huku sheria zikitupwa pembeni!
 
Giddy Mangi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
831
184
Tumeshamwandalia mikakati huyo,UBUNGE atausikia kwenye vyombo vya habari tuu,ajafanya lolote jimboni kwake huyo.Kama nyumba yako inakushinda kwa jirani utapawezaje?
 
Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
3,839
628
Katika pitapita yangu, jana nilibahatika kumuona mheshimiwa maghembe akizungumzia suala la sukari, akapiga mkwara kweli sukari isiuzwe nje ya mipaka ya nchi na akatoa namba yake ya simu with confidence yani ka hajui eti anayejua wanaotoa sukari nje wampigie kwa namba aliyoitoa, kali kuliko zote niliposema kweli mawaziri tunao na ni kweli hawazingatii sheria aliposema, ATAKAYERIPOTIWA KUFANYA VIVO HATA KAMA HAWANA USHAIDI WATAMFUTIA LESENI'' nikagundua kuwa mambo mengi yanafanyika na kuamuliwa hata ka hakuna ushaidi make mtu kutokeza na kudhubutu kusema hivyo hali nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria na katiba..pole sana mzee na nadhani ni uzee, sheria tanzania tunazo 415 na naomba zizingatiwe, siwatetei wanaouza sukari nje ila nashangaa kusikia waziri yaani public figure kama wewe unasema hata kama hauna ushaidi utafuta lesseni, inanipa wasiwasi kidogo na ubabe huu, na inanipa mwanga kuwa haya ndio mabavu yanayotumika kukandamiza walio wengi huku sheria zikitupwa pembeni!

kwani unaogopa nini?
mimi nadhani wako sahihi kwa kuwa ndo biashara yao
kama tanzania hakuna faida waendelee kupata hasara??
mbona wao umeme,mafuta,madini vimewashinda wanafiki hoa waache siasa?????
 
PatPending

JF-Expert Member
Aug 17, 2007
490
81
Mheshimiwa waziri alikuwa akichangamsha genge tu. Toka tulivyoiua tume ya bei katika miaka ya 1980 na kuondoa vikwazo katika uhamishaji/usafirishaji wa mazao ndani ya nchi, soko ndilo limekuwa mwamuzi mkubwa wa bei na idadi ya bidhaa. Kwanza, wizara anayoiongoza mheshimiwa Maghembe haina mamlaka ya kufanya yale aliyokuwa akitishia, kwa hili aende Viwanda na Masoko. Pili, kuna chombo kinachoitwa tume ya ushindani (FCC) na sheria ya ushindani ya mwaka 2003, hivi ndivyo vyombo vyenye mamlaka kisheria ya kufanya yale ambayo Mh. Maghembe alikuwa akiyatamka. Labda nitoe angalizo pia, suala kama hili likipelekwa katika mahakama ya ushindani (Fair Competition Tribunal) maamuzi yatakayotoka yanaweza pia kuzuia kile ambacho Mh. Maghembe alikuwa anayazungumza.
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom