Waziri Maghembe umedanganya umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Maghembe umedanganya umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by CHANGA, Nov 6, 2009.

 1. C

  CHANGA Member

  #1
  Nov 6, 2009
  Joined: May 26, 2008
  Messages: 95
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Waziri Maghembe umetangazia umma kuwa Mtihani wa darasa la Saba uliorudiwa katika baadhi za shule msingi za Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro haukuwa wa marudio bali ulikuwa ni kwa ajili ya utafiti ili kuliwezesha Baraza la Mitihani kutoa mithani mizuri mwakani. Waziri huu ni uongo Mkubwa eleza umma ukweli kuliko kuficha uozo na uchafu unaoendelea kwenye baraza hilo. Kama huwezi kueleza ukweli ambao unaufahamu basi wengine tutasema.

  1. Mtihani wa darasa la saba ulivuja katika maeneo mengi nchini lakini juhudi kubwa zilifanywa ili lisijulikane na umefanikiwa.
  2. Matokeo ya Mtihani huo kwenye shule zilizorudia mtihani huo ni mazuri sana katika masomo yote na alama zao zimerange kati ya 70 hadi 100.
  3. Chanzo cha kurudia mitihani hiyo kinatokana na patern ya perfomance iliyoko kwani majibu yao yanafanana sana jambo linloashiria watahiniwa walikuwa na majibu. Kwa hiyo baraza linataka lijihakikishiwe hilo na ikithibitka basi wafutiwe matokeo yao.

  Huo ndio ukweli wa marudio ya mitihani hiyo.

  Maghembe uozo unaoendelea Baraza la Mitihani unaufahamu fika na wewe ni sehemu ya uozo huo. Kumbuka ulivyonunuliwa mwaka jana kwa kupewa 200Milioni kutoka katika bajeti ya Baraza fungu la maendeleo ya 2008/09. Nasema haya kwa sababu nayafahamu na yanaumiza sana, ulafi wenu ndio unaoangamiza Elimu nchini.

  Maghembe unavyombeba Katibu wa Baraza Ndalichako mwisho wake upo lakini ni hatari sana wa watoto wetu na Taifa kwa ujumla, Lakini kumbuka kuwa mama huyu habebeki kwani nguvu unazotumia kumbeba ni nyingi sana na karibu utaishiwa nguvu hizo.
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Lakini uvujaji wa mitihani ulianza kabla ya Ndalichako kuingia NECTA, sema tu idara za serikali nyingi zimeoza na kila unayemweka hata kama ni mzuri ktk kazi anakuta shirika limeoza.
   
 3. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,731
  Trophy Points: 280
  Maskini, Ndalichako, Joyce, class mate wangu! Imekuwaje NECTA kuwa hivi chini yako?
  Nakumbuka vyema ulivyopata First Class UDSM, 1991, ukaendelea na msomo yako hadi PhD! Unashindwa nini kutumia unguli wako wa enzi hizo? Hivi na wewe unaweza kuwa umetekwa na mafisadi! Siamini. Salamu kwa Laurent.
   
Loading...